Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Naunga mkono asilimia 100% mgomo wa wafanyabiashara. Tena ningependa kuona ukienea nchi nzima!
Sababu ni kwamba uongozi wa Tanzania huwa unajifanya kiziwi pale Watanzania wanapoonyesha kutopendezwa na jambo fulani, na kutoa madai yao kwa njia ya vyombo vya habari au maandamano. Serikali imejengea tabia sugu ya kutosikiliza wananchi.
Wananchi wamefikia hatua ya kudai haki zao hata kwa kutukana, na kwa kuwa hawasikilizwi wanamtukana hadi Rais wakidhani labda kwa njia hiyo watasikilizwa. Ndio kwanza waambia mimi chura siwasikilizi.
Sasa iliyobaki ni migomo. Lazima tuweke mfumo wa kugoma, iwe ni mishahara au huduma. Tukiiambia serikali BRT iboleshwe wasisikie, basi tugome kutumia BRT. Tukiseme TRA wanatuumiza wasisikie, basi tutafute namna ya kugoma!
Tuanzishe mifumo ya ushirika iliyo na nguvu ya kusimamia migomo, iwe ni biashara au vyama vya wafanyakazi katika ngazi mbalimbali. Tuanze kugoma hadi kieleweke.
Tukiwaambia Poilisi msitusumbue barabarani kutufanya tusubiri muda mrefu ili kiongozi apite, kama hawasikii, siku nyingine tugome kuupisha msafara wa kiongozi. Tuanzishe umoja wa watumiaji wa magari barabarani.
Tugome, tugome, tugome hadi serikali iwe na masikio ya kutusikiliza tunapotoa kero zetu
Pia, soma=> Nguvu ya Umma: Bunge lalazimika kubadilisha Muswada wa Sheria ya Fedha baada ya maandamano ya Wananchi