Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Hii kauli ya bure iliyoanza katika elimu awamu ya tano na sasa imeshika kasi haifai kabisa, imekaa kisiasa zaidi, kilaghai na kipropaganda. Inazua tafrani kubwa kama zilivyotokea kwa kauli ya Chalamila na mama mjamzito aliyempigia simu.
Huko kwenye Elimu inaposemwa ni bure ukweli ni kwamba ada tu ndio hailipwi ila wanafunzi wanachangia michango mingine mingi sana. Sasa hapo elimu inakuaje bure?!
Katika hospital pia huduma haziwezi kuwa bure, zinaweza kuwa nafuu ila haiwezekani zikawa bure, lazima tu kuna sehemu mtu au mgonjwa atahitajika kuchnagia au kulipia.
Ukweli ni kwamba tangu enzi za Mwinyi kupitia mageuzi ya uchumi ya sera za World Bank na IMF za Structural Adjustments Program(SAPs) serikali ilifikia muafaka na wakopeshaji na wafadhili wake kuachana na sera za bure katika huduma za jamii. Tangu wakati huo hakuna tena huduma za bure nchi hii.
Bure sio uhalisia, ni kauli ya kupumbaza, inayotoa matumaini hewa na pia huduma zisizo na ubora wa kuridhisha. Serikali iondokane nayo, watu waishi katika uhalisia.