Dan Zwangendaba
JF-Expert Member
- Apr 25, 2014
- 5,814
- 8,118
Binafsi nikiri kwamba sijauona huo unaoitwa Mkataba au MOU (Intergovernmental Agreement, IGA) hivyo siwezi kutoa hoja zozote za kitaalam ikiwa mkataba au hiyo MOU ni nzuri au mbaya. Hata hivyo, kwa kuzingatia watanzania hawa wa leo, ambao walikaa miaka 10 chini ya uongozi wa Mhe. Jakaya Kikwete, kisha wakaishi miaka takribani 6 chini ya uongozi wa Mhe. John Magufuli, na "public outcry" iliyopo huko mitandaoni na mitaani, mimi nadhani BUSARA KUU kwa Serikali kwa Sasa ni kuachana na uwekezaji unaotarajiwa uufanywa na DP World kwenye bandari ya Dar es Salaam, hata kama uwekezaji huo una FAIDA kwa nchi.
Bila shaka, nchi itaendelea kuwepo pasipo uwekezaji wa DP World au pasipo uwekezaji wowote bandarini, lakini imani ya wananchi kwa Serikali yao ndio msingi wa Umoja, Amani na Mshikamano wa Taifa lolote duniani. Kwa sasa, approval rate ya serikali ya Samia kwenye jambo hili ni mbaya sana.
Kinachojadiliwa mitandaoni na mitaani, bila kujali kama ni kweli au sikweli, lakini ukweli unabaki kuwa havina afya kwa Serikali, havina afya kwa Rais Samia, na havina afya kwa Umoja wetu kama Taifa. Approval rate ya wananchi kwa Serikali na kwa Rais wao ni jambo muhimu sana. Ndiyo maana, kila pahali kuna mabango ya kusifu uongozi Rais, au matukio mubashara na recorded ya kusifu uongozi wa Rais, ni vipi tunaruhusu Serikali kufanya action kubwa yenye kushusha imani ya wananchi kwa Mhe. Rais na Serikali yake kwa kiwango hicho?
Na bahati mbaya, wanaoendesha mijadala ya kutoelewa na kutokubaliana na mkataba au uwekezaji huo huku mitandaoni na majukwaani si kundi dogo, au la wasiosoma. Karibu watanzania wote bila kujali kiwango chao cha elimu au makabila yao wameonyesha kutokubaliana na uwekezaji wa DP World, maana haueleweki na serikali imeshindwa kutoa maelezo yenye ushawishi kwa wananchi.
Nimalizie kwa kusema, pamoja na uchumi kuonekana kufunguka, lakini bado hali za wananchi ziko duni na makundi mengi yana makovu kwa sasa. Si vema kwa Serikali kufanya matendo ambayo yanaamsha hisia za wenye njaa, hata kama matendo hayo yataleta chakula baadaye kwa makundi hayo. Hakuhitaji tukio kubwa sana ili kusababisha kuvunjika kwa amani kwenye nchi yoyote, na infact, viongozi husika huwa hawaamini kama tukio fulani linaweza kubadilisha historia ya nchi hiyo. Mkataba au ushirikiano huu ni wazi haujaeleweka na umekuja wakati si muafaka, Serikali iachane nayo kwa sasa HATA KAMA UNA FAIDA kwa nchi.