Thailand
JF-Expert Member
- Nov 15, 2019
- 275
- 795
Yaani nchi maskini kama Tanzania yenye uchumi mdogo wa kumudu changamoto za nyumbani kwake mwenyewe, unatoa tena hicho kidogo na kukipeleka nje kuzijenga na kuendeleza nchi za wenzetu. Hii sio akili!
Kuna mambo mengi hapa nchini tunaweza kuyafanya na yakatuvutia uwekezaji mwingine mkubwa tu, na pia kusaidia taifa kuondokana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa baadhi ya vijana wa kitanzania.
Baadhi ya uwekezaji unaoweza kufanywa na fedha hizo na tukapata matunda makubwa kama taifa ni:
1. Ujenzi wa kiwanja standard kitachochukua michezo yote ya olimpiki kwa mfano kile cha Budapest kilicho host mashindano ya Track world championship mwaka 2023. Kiwanja hiki kikijengwa karibu na bichi zetu kubwa kwa ajili ya kuvutia uwekezaji na utalii wa baharini au ziwani kitakuwa na manufaa sana kwa taifa hili. Kwa sababu siku moja kama taifa tunaweza tukajikuta tumepewa hadhi ya kuandaa mashindano ya olympiki na dunia nzima ikaja Tanzania kushiriki mashindano hayo.
2. Ujenzi wa masoko ya kisasa yenye vizimba kila wilaya Tanzania kwa ajili ya kurasimisha biashara ndogo ndogo za machinga Tanzania. Hapa kama nchi tutakuwa tumeongeza tax base kwa wafanya biashara wadogo wadogo ambao wengi wao sio walipa kodi wazuri.
3. Ujenzi wa bandari kavu kubwa na ya kisasa mkoani Morogoro kwa ajili ya kontena zote zinazoingia kwa wingi pale bandarini Dar es salaam. Kwa kuwa tumekamilisha reli yetu ya SGR, sioni haja ya mizigo kulundika bandarini Dar. Hivyo wateja wetu wa hapa ndani hawatakuwa na sababu za kuwacheleweshea kuchukua mizigo yao kwa sababu, mteja mwenyewe ataamua kuchukulia mzigo wake kwenye bandari ya Dar au Morogoro. Kwa bandari hii kavu mkoani Morogoro uchumi wa nchi hauwezi lala kamwe na mizigo haitazidi kwenye bandari yetu ya Dar.
4. Kwa pesa hizo zinazoenda kuteketezwa huko nje, ni bora serikali iende ikajenge chuo kikuu mkoani Mara (Musoma) wakiite MUSOMA UNIVERSITY OF SPORTS AND ATHLETICS (MUSA) hiki chuo kitakuwa mahususi kwa ajili ya kukuza sekta ya michezo na riadha Tanzania ukizingatia mkoa wa Mara umepakana na nchi ya Kenya na Uganda ambazo ni mahususi na maarufu katika michezo ya riadha. Kwa kukijenga chuo hicho tutakuwa tumefungua uchumi mkubwa wa kanda ziwa kwa sababu chuo cha namna hiyo hakipo huko. Wanafunzi wengi kutoka nchi za Afrika mashariki pia watakuja kusoma michezo na kuongeza utalii kwa mbuga ya Serengeti iliyo hapo karibu.
Hayo ni baadhi ya fursa ambazo tunaweza kufanya hapa nchini kwetu Tanzania kwa pesa ambazo wizara ya mambo ya nje inataka ikateketeze huko nje kwa kisingizio eti kujenga majengo. Serikali tuonee huruma watu wa taifa hili, pesa hizo wekezeni hapa nyumbani kukuza ajira na uchumi wa vijana wa kitanzania na taifa kwa ujumla kwa baadhi ya miradi niliyoianisha hapo juu.
Pia soma