Serikali iachane na wazo la kwenda kujenga nchi za nje kwa kisingizio cha uwekezaji, tujikite kuijenga nchi yetu iwe na hadhi ya kimataifa

Kampuni zote za China zinazojenga barabara na reli nk Tanzania ni kampuni za serikali asilimia 100 na hutengenza faida ya kufa mtu ili faida itumike kuendesha serikali sio tu kutegemea kodi za raia wa china
 

Ushauri mzuri sana, lakini kwakuwa hiyo ni fursa nzuri ya upigaji ambao utakuwa rahisi sana. Na wameshapanga na kukubaliana hiyo dili, hakuna mtu atakubali kukusikiliza. Hilo ni dili na limeshawekwa sawa. Mbaya zaidi ni hela za NSSF, wanajua hilo ndio shamba la bibi.
 
Kampuni zote za China zinazojenga barabara na reli nk Tanzania ni kampuni za serikali asilimia 100 na hutengenza faida ya kufa mtu ili faida itumike kuendesha serikali sio tu kutegemea kodi za raia wa china
Yaani wewe jamaa ndo maana nikakwambia hujui unaongea nini! Huo ni uwekezaji ambao nchi nyingi tu makini zinafanya hivyo, shida ya huu wetu ni kwenda kujinga migorofa kwenye nchi za watu na kujidai eti huo nao ni uwekezaji. Kwanza pesa yetu tu madafu, pesa ambayo unaenda kujenga tower mbili Nairobi au South Afrika hapa Tanzania unajenga tower kama hizo 7 hadi 10 na majiji yetu yakapendeza
 
Kuna majengo pacha (tower) serikali imesema itajenga Nairobi Kenya, na nchi nyinginezo duniani
Doooo! Hi nchi kweli inachekesha

Kwahiyo wameshamaliza kuwekeza ndani na Sasa wanataka kwenda kuwekeza nchi za nje?

Hilo wazo ni la bi mkubwa au ndio anapelekwa pelekwa Ili watu wapige pesa
 
Huo ni mchongo wa wizi wa ndugu huyu January Makamba, wazuri hawafi.Ndugu huyu ni mtu mwizi, fisadi na hasiye na uwezo wa kufikiri kwani kichwani ni mweupe kabisa.
Nchi yetu kwa bahati mbaya, watu wengi wasio na uwezo wa akili za, kufikiri ndio viongoz. Watu hawa ni wezi wa mali ya umma na kila muda wanafikiria na kuiba . Watu hawa wanafikiria kuwa kuwa, kiongoz ni kuiba mali ya umma na kujilimbikizia mali.
 
Ni kweli kabisa hao jamaa calculation zao ni kuvuna tu wasipopanda
 
Kwa kweli inasikitisha sana
 
Tanzania inahitaji mabadiliko makubwa sana kwenye sheria za nchi namna ya kudhibiti wizi wa namna hii
 
Hapo lengo ni rushwa na siyo uwekezaji, pale Kigamboni kuna mradi umetelekezwa wa mabilioni ya watanzania hakuna anayejali sababu aliyeanzisha kavuta rushwa kubwa na kukaa pembeni
 
Hapo lengo ni rushwa na siyo uwekezaji, pale Kigamboni kuna mradi umetelekezwa wa mabilioni ya watanzania hakuna anayejali sababu aliyeanzisha kavuta rushwa kubwa na kukaa
Yaani nchi za wenzetu wenye akili wavumbuzi na professional kama akina Elon Musk, Bill Gates ndio matajiri wakubwa ila bongo bahati mbaya wanasiasa with zero brain ndio matajiri wa kupindukia
 
Kabisa!
 
nadhani tungeaza kuweka mipango miji vizuri nyumba zikae kwa mitaa, kupunguza shughuli za kimaskini kama kila nyumba genge njee au fremu. makazi yabakie makazi na sio makontena, uuzwahi wa beer kila sehemu. Nimeshtushwa sana nimepita Bunju B hivi karibuni pale stendi ya zamani kumekuwa ni uswahili tandale hapafai. mbona Mtwara watu maskini lakini wanaishi kwenye mitaa iliyopangiliwa sio hapa mishikaki mara muuza mkaa yaani hatuna ustaarabu kabisa.
sisi watu wa Tanzania nani katuloga tunakuwa kama nigeria na wao walishatoka kwenye uholeholela. Hata goba, au mpiji kuna uwezekano watu wakaa kimitaa.
sehemu kama madale inasikitisha sana kuwa holela holela na mji ni mpya.
 
U
Uholela na umaskini wa kutengenezewa ndio kete ya ushindi kwa chama chakavu
 
Safi sana
 
Naona kaliwa kichwa mwenye wazo hili la kujenga nchi za watu
 
Kampuni zote za China zinazojenga barabara na reli nk Tanzania ni kampuni za serikali asilimia 100 na hutengenza faida ya kufa mtu ili faida itumike kuendesha serikali sio tu kutegemea kodi za raia wa china
Jee hizo kampuni zipo chini ya wizara ya mambo ya nje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…