The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 6,147
- 20,080
Serikali iendeshe inchi kwa usawa. Isipendelee. Najua hakuna usawa kamili ila angalau kua na usawa kiasi.
Hii serikali inaonekana iko selective, baadhi ya makundi ya watu inayapenda wengine hawapendwi.
Tukianza na watumishi wa umma. Toka serikali hii imeingia haijawahi kuongeza mishahara wala kupandisha watu madaraja ila kuna baadhi ya taasisi zimependelewa kuongezewa mishahara.
Wafanyakazi wa TRA wameongezewa mishahara karibu 300% huku watumishi wa halmashauri na serikali kuu na mashirika ya umma mengine wakiendelea na misahara ile ile aliyowaacha nayo Kikwete. Hii maana yake ni kua watumishi wa TRA ni bora sana kuliko watumishi wengine.
Ukiajiriwa serikali kuu au halimashauri unaanza na mshahara wa TGSD-720,000 kwa mtu mwenye shahada ila TRA 2,300,000 kutoka 800,000. Meneja wa TRA wa wilaya au mkoa mshahara ni sawa na mishahara ya baadhi ya wakurugenzi wa mashirika ya umma. Huo ni mfano mmoja tu.
Njoo kwa wakulima, serikali inawaambia wakulima wauze mazao kwa bei wanayotaka wao, yaani watutwange sisi walaji kwa bei waayotaka wao. Leo mkulima akiuza gunia la mahindi 🌽 laki 5 kutoka 60,000 hakuna wa kumuuliza maana karuhusiwa kujipangia bei. Cha ajabu wafanyabiashara wa sukari juzi hapa walijipangia bei kututwanga wanavyotaka wakafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi.
Unajiuliza je wenye nyumba na wao watutwange kodi ya nyumba? Wenye usafiri nao watutwange nauli? Utaambiwa hao hawaruhusiwi. Sasa kama hawaruhusiwi inakuaje wakulima wao waruhusiwe kujipangia bei ila watu wengine wenye bidhaa zao wakataliwe?
Serikali iache kuendesha nchi kwa upendeleo. Hii nchi watu wote tuna mchango wa maendeleo. Huwezi kubagua watumishi hawa ukawaona ndio wa muhimu ukawaongezea mshahara ukawaacha wengine wana-suffer.
Pesa yote inayokusanywa na TRA inapelekwa halmashauri kwa matumizi lakini watumishi wa halmashauri wamepigwa na maisha wengi wanauza vitumbua, kashata, kahawa, uji, na wengine kuchoma mahindi. Hawa watu kwa nini wasiibe?
Kuna jamaa ananiambia hata takukuru mishahara ni ya kulenga kwa manati halafu wanaambiwa wapambane na rushwa. Yaani wewe una njaa unakuja kunikamata mimi nimeshiba na chakula kiko hapo, cha kwanza nakupa ule uache mdomo mdomo.