Serikali iache kutoa taarifa za covd 19 ,inaleta taharuki isiyo na sababu ,tulishakubali kuishi nao mtafukuza watalii kwa mambo ya hovyo!

Serikali iache kutoa taarifa za covd 19 ,inaleta taharuki isiyo na sababu ,tulishakubali kuishi nao mtafukuza watalii kwa mambo ya hovyo!

Mganguzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
1,604
Reaction score
3,715
Huu ugonjwa hebu upotezeeni kabisa ,tulishakubali kuishi nao .kutuletea taarifa za covd ni kututisha na kuleta taharuki isiyo na tija hata inaweza kufukuza watalii kuja nchini achaneni na hizo stori tafadhali
 
Mkuu, serikali ilifaidika kwa mabilioni ya shilingi kutokana na suala la UVIKO 19 ambayo kuja kwake kuliambatana na vigezo, kanuni, na masharti ambavyo iliyaridhia.

Kwa hiyo basi vigezo, kanuni na masharti vya kimkataba ni lazima kuzingatiwa. Siku zote maskini hana uchaguzi kwa kile anachopewa na tajiri wake.

Hakuna ubishi wowote kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi ziizokuwa maskini, na imeingia mikataba mingi yenye masharti ya hovyo sana. Wajukuu wetu watakuja kuwadharau mno viongozi wetu wa sasa waliotuingiza humo. Kwa kifupi kabisa CCM ni laana kwa taifa letu.
 
Kwa hiyo ukiwa unatembea njiani iwapo mbele kuna simba inafaa ujue ukweli ili uchukue tahadhari au usiambiwe ukweli ili ujiendee kizembe ukaliwe na simba ?
 
Waachane na huu upuuzi tena kwa haraka sana!! Nchi yenyewe inachechemea then waharibu tena hata pale penye ahueni utakuwa ni ujinga wa kiwango cha lami!!

Hao wenye mamlaka ya kutangaza waachane na hiyo upuuzi kwanza haisaidii hata ukitangaza!!
 
Back
Top Bottom