Kwa kipindi hiki Cha bajeti serikali Ijiepushe na kutumia faini za barabarani kama mojawapo ya vyanzo vya mapato. Nakumbuka hii iliwahi kujadiriwa bungeni lakini mpaka sasa hivi bado kuna tetesi kuwa serikali inapohitaji hela ya ziada huwabana trafiki wa barabarani kutumia nguvu nyingi kukusanya hela za makosa ya barabarani.
Kama wewe ni dreva utajua hii. Kuna siku unakutana na matrafiki wamechachama kupiga faini hata makosa madogo ambalo hata magari ya serikali na matrafiki wenyewe wanayo. Chukulia mfano gari lako taili zake zinaelekea kuchoka, utapigwa faini. Ila ukiangalia Hali ya taili lako ni Bora zaidi kuliko zao.
Lakini pia faini kubwa za barabarani zinasababisha rushwa kwa matrafiki. Unapofikiria kulipa faini ya 30,000 unaona Bora umpe trafiki hata 10,000 ukamalizana naye.
Kwa rushwa ya namna hiyo hata wenye magari mabovu wanatoa rushwa na kuachiwa na baadae kuwa chanzo Cha ajali.
Tujadiri.