Serikali iamuru Vyuo Vikuu vyote kuvaa sare maalumu

Serikali iamuru Vyuo Vikuu vyote kuvaa sare maalumu

Vyuo vikuu vinabeba vijana waliotoka famila za kitajiri, kimaskini na vijana wanaotoka kwenye famila za kawaida (sio maskini na sio matajiri).

Ni asili ya mwanamke kupenda mambo mazuri, walioishi kota wanalijua hili.

Sasa Binti katoka familia za mboga moja, na chuoni analupiwa na serikali au mdhamini, huyu binti anaona wenzake kila weekend wanapiga pamba mpya, lazima ageuze mwili wake kuwa kitegauchumi.

Vyuo vikuu vingi au vyote nchini kando yake kuna madanguro ya kisasa. Na wajasiriamali wenyewe ni mabinti waliotoka famila za kimaskini na wachache ni wale wa familia za kati.

Uniform kwa wanafunzi wa vyuo vikuu ndio mwarobaini wa tabia chafu vyuoni.

Hata wizi wa laptop na simu vinafanywa na vijana wanaotoka familia za kimaskini ili waonekane wako vizuri. Mostly pesa wanazopata kwa kuuza laptop za wizi wananunua nguo.
Hell no! wazazi/walezi wafundishe watoto ku kukubaliana na maisha wanayoyakuta na wasiwe na tamaa.
Chuo wanasoma watu wazima pia sio vijana tu mkuu.
 
Mleta mada,pole sana,tatizo la maadili ya watoto,linaanzia kwenye familia na jamii inayomzunguka mtoto husika.Mtoto huharibika mapema kabisa,asipowekewa misingi imara ya tabia njema,angali bado mdogo kabisa,huku chuoni huja kuishi tabia zake alizofunzwa toka utotoni na familia au jamii aliyokutana nayo.Kutatua hayo matatizo ya watoto yahusuyo tabia kwa kuwashonea uniform,haitasaidia,kama misingi ya malezi ya watoto hawa,isiporekebishwa.Waache waende vyuoni,tena most of them,hawataki kukaa hostel hasa wadada,hivyo hupendelea kukaa maghetoni,wainjoi sex to the fullest,inshort wanaolewa temporary,wakimaliza masomo yao,hurudi uraiani ambapo baadhi yao huolewa,na wengine hubaki kama single mothers hasa kama mume wa chuo,alifanikisha kumpa ujauzito.
 
Vyuo vikuu vinabeba vijana waliotoka famila za kitajiri, kimaskini na vijana wanaotoka kwenye famila za kawaida (sio maskini na sio matajiri).

Ni asili ya mwanamke kupenda mambo mazuri, walioishi kota wanalijua hili.

Sasa Binti katoka familia za mboga moja, na chuoni analupiwa na serikali au mdhamini, huyu binti anaona wenzake kila weekend wanapiga pamba mpya, lazima ageuze mwili wake kuwa kitegauchumi.

Vyuo vikuu vingi au vyote nchini kando yake kuna madanguro ya kisasa. Na wajasiriamali wenyewe ni mabinti waliotoka famila za kimaskini na wachache ni wale wa familia za kati.

Uniform kwa wanafunzi wa vyuo vikuu ndio mwarobaini wa tabia chafu vyuoni.

Hata wizi wa laptop na simu vinafanywa na vijana wanaotoka familia za kimaskini ili waonekane wako vizuri. Mostly pesa wanazopata kwa kuuza laptop za wizi wananunua nguo.
Kwenye jamii ya wajinga wewe ndo mjanja wao. Jomba hakuna kitu umeandika hapa. Ni ujinga mtupu umeuwaza. FUTA HII
 
Kuna wanaojiuza ambao sio wanachuo, hao pia tuwavalishe sare ili wasijiuze?

Kujiuza ni tamaa tu, kuna watu kwao wana pesa na bado wanajiuza.

Pia kuna watu kwao maskini ila hawajiuzi,
Na hata wakijiuza, kama wewe hununui, kuna shida gani?
Mbona zipo biashara nyingi tu na bidhaa nyingi zipo sokoni na sio wote tunanunua?!?
 
JF hakika ni jukwaa huru hivyo kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake na maoni pia.
 
Back
Top Bottom