lusajoaida
New Member
- Jul 27, 2023
- 2
- 2
Vipaji imekuwa ni ajira inayolipa katika inchi zilizoendelea,inchi nyingi zilizoendelea duniani zimewekeza kwenye kutambua na kuibua vipaji vya watoto.
Andiko hili linaelezea umuhimu wa Serikali kuibua vipaji mbalimbali vya watoto kupitia vipengele vifuatavyo
1.UTANGULIZI.
2.TATIZO LIKO WAPi?
3.NINI KIFANYIKE
4.MATARAJIO
1.UTANGULIZI.
Serikali imekuwa ikiweka mkazo wa michezo mashuleni na kumekuwa na michezo kama vile UMISETA na UMITASHUMITA.
Michezo hii imekuwa ikifanyika kila mwaka kuanzia ngazi ya Shule hadi ya Taifa.Ni kweli usiopingika kwamba michezo hii inaleta umoja lakini pia ni afya kwa jamii.
Matokeo ya michezo hii yamekuwa ni madogo sana kulingana na gharama ambazo Serikali imekuwa ikiwekeza.
Ni ukweli usiopingika kuwa Serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa katika sekta ya michezo na burudani lakini uibuaji wa vipaji kuanzia chini umekuwa duni sana.Wanamichezo wengi wajitafuta wenyewe na inchi huwatambua baada ya mafanikio fulani.
Picha na Mwananchi Media
3.TATIZO LIKO WAPI?
Tatizo kubwa la michezo hii ya UMISETA na UMITASHUMTA lipo kwenye ufuatiliaji wa vipaji vya wanafunzi vilivyo ibuliwa tujiuli, Je ? ni nani anayehusika kufatilia maendeleo ya wanafunzi waliofanikiwa kufuzu hadi hatua ya kitaifa pindi wanaporudi Shuleni.
Je, ni taasisi gani inayowafuatilia wanafunzi hawa pindi wanaporudi Shuleni na kumaliza Elimu yao ya msingi au Elimu ya Sekondari. Ni kweli michezo hii ni kama mabonanza ya kujenga afya na kuleta Umoja katika jamii.
Dunia ya sasa tunatakiwa kuwaza zaidi ya hapo kwani vipaji vimekuwa ni ajira kubwa sana kwa vijana
Mara nyingi wanafunzi hawa baada ya kumalizika michezo hii hurejea Shuleni ambako hata miundombinu ya michezo husika haipo mfano; wanafunzi wenye vipaji vya kuimba hurudi mashuleni ambako hata vifaa vya Muziki hakuna.
Wanafunzi wengi humaliza Elimu ya Sekondari na kuendelea na shughuli zingine huku vipaji vyao vikipotea taratibu.
3. NINI KIFANYIKE?
(i) Serikali kuunda mtaala maalumu wa michezo utakaojumisha vipaji mbalimbali.
Kwa sasa vipindi vya michezo mashuleni vipo kama sehemu ya ziada kwa ajili ya kujenga afya tu. Ni vuzuri Serikali kupita Wizara husika kuhakikisha vifaa mbalimbali kwa mahitaji ya michezo vinapatikana Shuleni.
(ii)Kuanzisha Shule maalumu kwa wenye vipaji.
Kumekuwa na Shule za wenye vipaji maaalumu kwa upande wa Taalumu peke ya kwa maana ya masomo ya darasani mfano; Tabora boys,Iliboru, Kibaha na nyinginezo.
Napenda kuishauri Serikali kuanzisha Shule maalumu zitakazo kusanya wanafunzi wenye vipaji mbalimbali , kumekuwa na Shule hizi za michezo mfano;Fountain Gate na alliance laikini ni Taasisi binafsi na zimejikita kwanye vipaji vya mpira pekee.
Tunahitaji kuwa na Shule maalumu zitakazo kuwa na miundombinu kamilifu na michezo ya aina zote.Shule hizi zitasajili wanafunzi wenye vipaji na wanaohitaji kuendeleza vipaji vyao.
Shule hizi zinaweza kujengwa kikanda au katika kila Mkoa kuwa na Shule moja ya Vipaji.
(iii) kusuka upya Mashindano ya UMISETA na UMITASHUMTA.
Serikali kupitia michezo hii kwa Shule za msingi na Sekondaari haina budi kuangalia upya muundo wake.Mnufaika namaba moja wa michezo hii lazima awe ni mwanafunzi na sio wasimazizi wala waandaaji
(iv) Ufuatiliaji wa vipaji mara baada ya Mashindano kumalizika
Kwakuwa mashindano haya ni mchujo unaoanzia ngazi ya Shule ,wilaya,Mkoa,Taifa hadi Afrika Mashariki kuwepo na timu maalumu ya wataalamu ambyo iatafanya kazi ya kukusanaya wanafunzi wote wanaofika hatua za juu
(v)Kuwepo kwa walimu wa Michezo Shuleni (waliosomea)
Uwepo wa mwalimu maalumu wa michezo Shuleni kutasaidia kuibua Vipaji vya wanafunzi tangu wanapoandikishwa darasa la Kwanza kwa upande wa Elimu ya Msingi au wanaposajiliwa kidato cha Kwanza kwa upande wa Elimu ya Sekondari.
Kumekuwa na uteuzi wa walimu wa michezo mashuleni wengine hata hawana hamasa ya Kupenda Michezo hali inayowakitisha tamaa watoto wenye vipaji.
Picha na mwananchi media
4. MATARAJIO
Kama Taifa tukitekeleza mambo haya tutakuwa tumefanikiwa mambo yafuatayo
(i) Kuibua vipaji kivitendo
(ii)Kukuza na kuendeleza vipaji vya watoto
(ii)Kutangaza inchi kupiti Timu zetu za Taifa na vipaji vya mtu mmoja mmoja mafno Muziki na Ngumi
Michezo imekuwa ni nyenzo muhimu Duniani katika kutangaza inchi.Hili itatokea kwasababu tutakuwa na wanamichezo bora watakao iwakilisha inchi kimataifa.
(iv)Kukuza Uchumi wa inchi.
Kupitia michezo Sekta ya Utalii itakuwa na kuingizia inchi mapato, Lakini pia michezo ni biashara Serikali itaingiza mapato kupitiaa Ukusanyaji Kodi.
(v)Ongezeko na Ajira.
Michezo mabalimbali na Muziki viataongeza Ajiara kwa vijana na Kuipunguzia Serikali mzigo ambapo kwa sasa hata wenye vipaji wanapamabana kupata kazi za Maofisini.
(vi)Michezo huleta Umoja na Mshikamano
Michezo huleta Undugu
Michezo huleta Amani.
Picha kwa msaada wa Matukio Leo
Kama Taifa tuna watoto wenye Uwezo tofauti tofauti Ni vizuri tutengeneze mfumo Mzuri wa kuchunguza Uwezo wa watoto hawa tangu wakiwa wadogo na si kulazimisha wote waende upande mmoja.

Upvote
2