BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Mimi ni mwananchi wa kawaida leo nimeamua kuweka hili suala wazi ili jamii ione wazi kuliko kuendelea kulalamika chinichini kila siku.
Naamini kupitia hapa Jamii Forums ujumbe huu utawafikia Watanzania wengi na vyombo vya Serikali kuweza kuelewa ninachokiandika hapa.
Hoja yangu ni kwenye zile boti ndogo za Kigamboni pale Kivukoni wanazoziita SeaTaxi kwa jina maarufu boti za mwendokasi.
Pale Kivukoni kuna zile boti za Azam zinazoitwa SEATAXI zinabeba watu kuanzia 120 kwa kuhesabu Seat ila nafikiri idadi inaweza kufika 150 hadi 200 kwa kuwa kuna wengine wanasimama.
Nianze na pongezi ili nisie onekana nipo negative tu, kwanza natoa heko kwa kuwa zimepunguza foleni ya watu au msongamano uliokuwepo awali eneo hilo.
Boti hizo zina kasi na zinaweza kwenda hadi round 3 wakati zile boti kubwa zenyewe zikawa na round moja, kwa hapo bila shaka wahusika au mamlaka zimefanya kazi nzuri.
Lakini upande wa pili kwa uchunguzi wangu wa harakaharaka hakuna maboya incase emergency yoyote itatokea.
Ujumbe huu uwafikie Watanzania na Serikali kwa ujumla ili wafanyie kazi haraka kabla madhara makubwa hayajatokea.
Nimekuta zina maboya yale madogo 6 tu, hilo ni jambo la hatari kwa kuwa kwa kiwango cha watu wanaokitumia kwa wakati mmoja na idadi ya maboya ni machache mno.
Hata hayo machache yaliyopo yamefungwa katika njia ambayo ikitokea dharura inakuwa ngumu kuyatoa kirahisi. Pia sijaona kama kuna life jacket hata chache za akiba.