KwetuKwanza
Member
- Mar 13, 2023
- 82
- 150
Pamoja na maboresho ambayo yamefanyika uwanjani hapo lakini bado changamoto ni suala la moshi unaotokana na mapishi unaotawala eneo hilo mara nyingi hasa mida ya jioni.
Uwanja huo uliozungushiwa ukuta kwenye upande wake wa Kusini kuna shughuli za Wafanyabiashara wa dagaa ambao wanakaanga dagaa kwa nishati za kuni, hivyo kusababisha moshi mwingi kusambaa hewani na kuwa kero kwa watu wanaopita na kufanya shughuli zao kuzunguka eneo.
Kuna kipindi waliondolewa eneo hilo kwa kuwa ni karibu na reli lakini waliporejea hali imekuwa changamoto kwa watu wengine, kwani mbali na Uwanja pia ni karibu na Shule ya Msingi Nyamagana.
Mamlaka zinafahamu kuhusu tatizo hilo lakini zimekuwa kimya kutokana na hulka za Kisiasa kwasababu kundi hilo la Wafanyabiashara waliondolewa kwenye eneo hilo ili kupisha upanuzi wa eneo la ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR lakini watu hao walirudi kimyakimya na kufanya eneo hilo ambalo linazungukwa na ofisi nyeti zikiwepo za Uhamiaji, TANROADS, TTCL na Posta.
Nashauri jambo hilo litafutiwe utatuzi, kuna watu watakuwa hawaendi uwanjani kutokana na moshi kuwa mwingi na hivyo ama kuwakera au kuwaumiza.