cyrax
Senior Member
- Mar 12, 2017
- 110
- 109
Wakuu salam,
Nisiwapotezee muda.
Kwa muda mfupi niliokuwa Tunduru hasa maeneo ya mpakani na nchi ya Msumbiji nimejifunza mengi ambayo naona kama chanzo cha jamii za maeneo haya kuwa chini kimaendeleo.
Kwanza niweke wazi kuwa jamii za mpakani tunduru zina mwamko mdogo sana wa kielimu, watu wengi wanajikaza kusomesha watoto wao kwa shule Za msingi tu na hawana mpango wa kusomesha watoto wao shule za sekondari.
Hii hali kwa uchunguzi wangu nimeona mojawapo ya sababu ni kukosekana kwa shule za sekondari za kutosha kwenye vijiji vingi. Unakuta vijiji vinne ambavyo vipo mbalimbali vinategemea shule moja ya sekondari ya kata.
Sio rahisi kwa watu wengi kusomesha watoto kwa kukaa boarding ambapo kunakuwa na gharama za kulipia pia sio rahisi kulipa nauli zaidi ya elfu 5 kila siku watoto wasome day kwa kwenda shuleni kila siku.
Mimi ninaamini kuwa ili kuleta mwamko wa maendeleo ya jamii fulani ni lazima angalau asilimia 50 ya wakazi wa eneo hilo wawe na elimu ya sekondari.
Hakuna namna ya kuleta maendeleo kama hadi leo kuna zaidi ya asilimia 30 ya wakazi kwenye maeneo niliyotaja hawajui kusoma na kuandika.
Kuna haja ya serikali kuamua kujenga shule mpya za sekondari angalau iwepo moja kwa vijiji viwili ili iwe rahisi kwa wakazi hawa kusomesha watoto wao shule za sekondari bila kuwa na gharama kubwa.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.