Serikali iangalie kuhusu kufukuza wamachinga walemavu

sinza pazuri

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
3,344
Reaction score
9,066
20211018_111053.jpg

Kama Mama Samia ameamua kuondoa watafutaji wa mitaani yani wamachinga. Ni sawa. Ila nafikiri angewatzama kwa jicho la huruma wamachinga wenye ulemavu ambao hawawezi kubeba mizigo wala kulima. Kuwaondoa watu wa namna hii ni ukatili mkubwa sana.

Naiomba serikali ya Mama Samia iwawekee utaratibu mzuri kama vibanda local vinawachukiza machoni mwao basi wawekee hata vibanda vinavyopendeza nao wapate rizki zao na familia zao.

Nawasilisha!
 
Machinga ni machingas tuu, hakuna ubaguzi wa hali yoyote ile. Mwishoni mtasema machinga wanawake na wajane waachwe. Fagio lipite kwa wote.
 
Machinga ni machingas tuu,hakuna ubaguzi wa hali yoyote ile. Mwishoni mtasema machinga wanawake na wajane waachwe. Fagio lipite kwa wote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kuna machinga inatakiwa waangaliwe tuache siasa kuna watu wanaitaji kutega mjini ili wapate wateja kutokana na hali zao za ulemavu.

Sasa ukishapitisha fagio kwa mlemavu bado utajisifu umefanikiwa nini?
 
Mleta mada huwezi tutajia nchi ambayo walemavu huwa hawafuati sheria na taratibu. Hata mahakamani hakuna sheria za walemavu tu na wasio na ulemavu. Hakuna excuse katika hili
 
Nchi zote duniani zina wamachinga...sisi basi tuonee huruma hata walemavu

images (6).jpeg

images (5).jpeg
 
Sheria ifuatwe na wote sio kujifichia kwenye unyonge.
Walemavu waende ustawi wa jamii
Majiji yetu yanatakiwa kuwa inclusive yasibague maskini na walemavu.

Ustawi wa jamii watapewa ugali wa familia zao?
 
Kama Mama Samia ameamua kuondoa watafutaji wa mitaani yani wamachinga. Ni sawa. Ila nafikiri angewatzama kwa jicho la huruma wamachinga wenye ulemavu ambao hawawezi kubeba mizigo wala kulima. Kuwaondoa watu wa namna hii ni ukatili mkubwa sana.

Naiomba serikali ya Mama Samia iwawekee utaratibu mzuri kama vibanda local vinawachukiza machoni mwao basi wawekee hata vibanda vinavyopendeza nao wapate rizki zao na familia zao.

Nawasilisha!
Sasa serikali ichukue lipi mwananchi huyo huyo anadai njia ya kupita kwa kuwa njia yake ya miguu imezibwa,mwanchi huyo huyo anasema miji yao haipendezi tena,mwananchi huyo huyo anasema upikaji holela ukiachwa kama ulivyo sasa kuna hatari ya kipindupindu mbeleni.Je ni kweli ukiwa mlemavu hupaswi kufuata taratibu? Jibu ni hapana.Walemavu wanadai eneo au wasitolewe barabarani?Mtakumbuka pale karume walemavu waliandamana barabarani pale karume wakitaka kupewa eneo pale wajishughulishe wakapewa mwisho maeneo yale wamewauzia watu wasio na ulevu yamejengwa maduka ya mabegi ya bei kubwa yanapaswa kuitwa duka lenye vigezo vya kusajiriwa.Hoja isiwe ni ulemavu au jinsia suala ni sheria inasemaje kuhusu eneo husika.
 
Majiji yetu yanatakiwa kuwa inclusive yasibague maskini na walemavu.

Ustawi wa jamii watapewa ugali wa familia zao?
Itungwe Sheria ambayo itawapa kipaumbele Wamachinga Walemavu kwenye maeneo ambayo yametengwa na Serikali, ila sio kuwahurumia huku wanavunja Sheria za Nchi.
 
Sasa serikali ichukue lipi mwananchi huyo huyo anadai njia ya kupita kwa kuwa njia yake ya miguu imezibwa,mwanchi huyo huyo anasema miji yao haipendezi tena,mwananchi huyo huyo anasema upikaji holela ukiachwa kama ulivyo sasa kuna hatari ya kipindupindu mbeleni.Je ni kweli ukiwa mlemavu hupaswi kufuata taratibu? Jibu ni hapana.Walemavu wanadai eneo au wasitolewe barabarani?Mtakumbuka pale karume walemavu waliandamana barabarani pale karume wakitaka kupewa eneo pale wajishughulishe wakapewa mwisho maeneo yale wamewauzia watu wasio na ulevu yamejengwa maduka ya mabegi ya bei kubwa yanapaswa kuitwa duka lenye vigezo vya kusajiriwa.Hoja isiwe ni ulemavu au jinsia suala ni sheria inasemaje kuhusu eneo husika.
Serikali isiweke matabaka ya watafutaji mijini....wenye mitaji mikubwa na wenye mitaji midogo wote wana haki ya kutafuta rizki mijini.
 
Itungwe Sheria ambayo itawapa kipaumbele Wamachinga Walemavu kwenye maeneo ambayo yametengwa na Serikali, ila sio kuwahurumia huku wanavunja Sheria za Nchi.
Hakuna sheria inayokataza wanachagua mjini
 
Back
Top Bottom