Serikali iangalie kwa ukaribu suala la Bima ya Afya. Mzigo ni mkubwa sana kwa Mtu kama Mimi

Mtanikumbuka RIP Chato boy
Rais Samia na Waziri Ummy Mwalimu Watanzania mnaowaambia walipe BIMA ya afya shilingi 488,000 kwa baba na mama, 120,000 kwa kila mtoto, na kama wanaishi na wazee wao, basi Kila mmoja wawalipie shilingi 360,000.

Hamuoni kama BIMA yenu ni kejeli kwa Watanzania walio wengi, tena wa hali ya chini kama Mimi?

Njoo katika uhalisia wa hali yangu halafu uniambie je, nitaweza?

Tulio wengi hatuna kazi rasmi ambazo zenye kunihakikishia maokoto yangu ya uhakika yanakuwepo. Nikisema nijihakikishie kuzipa leo ili nifanye maajabu nyumbani kwa kupambana aswa aswa ni kulibahatisha liten nite (elf 10).

Nimeweka elf 10 ili iwe raisi kueleweka. Pia naomba nifanye hiyo elf ni Kila siku pasipo kukosa hata siku moja kwenye kutafuta hata kama unaumwa haijalishi katika kuipata liteni lako.

Tunachukulia hakuna kupumzika, kwa mwezi tunategemea kukusanya laki 3. Kama tusipo igusa hata shilingi 10

Matumizi kwa siku kwa mwenye familia ya mke na watoto kama watoto 2 tu Kwanza. Kwa kujibana sana juu ya matumizi ili tuone tunatengeneza balance kiasi gani ili tuweze kukitumia kwenye kuwekeza juu ya Afya ya familia.

Matumizi
1) Michele kg 1 ule Mchele wenye mawe kama yote ni elf 2000

2)unga kilo moja ya Dona shilingi 2000

3)
Maharagwe kg 1 3200/= ili yatumike siku nzima

4) Mboga za majani zilizo katwa katwa ni sh. 500

5) Mkaa kopo 500 kwa elf 1000

6) Fujo ndogo ndogo kama vile mafutta vitungu nyanya n.k labda tuseme itumike elf 1000

7) Kuna nshu ya maji ya kutumia, sabuni ya kutumia, kama vile kuosha vyombo kufua nguo n.k labda tuseme elf 2000

Tuje kwenye macalculation sasa
2000+2000+3200+500+1000+1000+2000= 11,700/=

Inazidi hadi pesa unayipata kwenye maokoto yako kwa siku. Hapa ninazungumzia wale wote wenye kuingiza elf 10 kwa siku na Wala si wale wenye kuingiza chini ya hapo. 😂😂😂

Hivi kweli kabisa Mh.Rais hii serikali yako inamfikilia mwananchi wa hali ya chini kama Mimi ama mnatuona wote tupo sawa na nyinyi katika maokoto yenu?

Je, kwa mtazamo wa harakaharaka huyu mtu ataweza kumudu gharama za BIMA yako kweli Mh. Rais wangu?

Kumbuka anao watu Wanao mtegemea nje ya familia yake inayomzunguka kama vile baba mama na ndugu zake wengine wapembeni wasio na uwezo. Pia Kuna mawifi mashemeji na wakwe zake.

Mh. Rais katika hili mnaleta masihala kwa watanzani wa hali ya chini, hapa ndipo tunasema aliyenacho hataki kumkumbuka asiyenacho.
 
Uwenda wamekuficha ukweli,tunaomba sana mh. Rais tupunguzie mzigo wa bima ya afya ikibidi gharama za kuchangia ziwe ndogo ili ikibidi watu wengi tunufaike nayo. Shukrani kama maombi yangu yataonekana na kukufikia mbele yako.
Hakuna muheshimiwa humo,pigia simu mama yako au hata dada yako muite hivyo utakuwa umefanya la maana zaidi.

By the way,huko ulipo huna mbunge?kama unae basi haya maombi yako kampe huyo mbunge wako then atayawasilisha kwake haya ndiyo maagizo aliyoyatoa mama yenu.
 
Duh....hahaha
 
Kule X republic nimeikuta hii
 
Attachments

  • Screenshot_20230916-201932.png
    Screenshot_20230916-201932.png
    46.8 KB · Views: 17
Rais Samia na Waziri Ummy Mwalimu Watanzania mnaowaambia walipe BIMA ya afya shilingi 488,000 kwa baba na mama, 120,000 kwa kila mtoto, na kama wanaishi na wazee wao, basi Kila mmoja wawalipie shilingi 360,000.

Hamuoni kama BIMA yenu ni kejeli kwa Watanzania walio wengi, tena wa hali ya chini kama Mimi?

Njoo katika uhalisia wa hali yangu halafu uniambie je, nitaweza?

Tulio wengi hatuna kazi rasmi ambazo zenye kunihakikishia maokoto yangu ya uhakika yanakuwepo. Nikisema nijihakikishie kuzipa leo ili nifanye maajabu nyumbani kwa kupambana aswa aswa ni kulibahatisha liten nite (elf 10).

Nimeweka elf 10 ili iwe raisi kueleweka. Pia naomba nifanye hiyo elf ni Kila siku pasipo kukosa hata siku moja kwenye kutafuta hata kama unaumwa haijalishi katika kuipata liteni lako.

Tunachukulia hakuna kupumzika, kwa mwezi tunategemea kukusanya laki 3. Kama tusipo igusa hata shilingi 10

Matumizi kwa siku kwa mwenye familia ya mke na watoto kama watoto 2 tu Kwanza. Kwa kujibana sana juu ya matumizi ili tuone tunatengeneza balance kiasi gani ili tuweze kukitumia kwenye kuwekeza juu ya Afya ya familia.

Matumizi
1) Michele kg 1 ule Mchele wenye mawe kama yote ni elf 2000

2)unga kilo moja ya Dona shilingi 2000

3)
Maharagwe kg 1 3200/= ili yatumike siku nzima

4) Mboga za majani zilizo katwa katwa ni sh. 500

5) Mkaa kopo 500 kwa elf 1000

6) Fujo ndogo ndogo kama vile mafutta vitungu nyanya n.k labda tuseme itumike elf 1000

7) Kuna nshu ya maji ya kutumia, sabuni ya kutumia, kama vile kuosha vyombo kufua nguo n.k labda tuseme elf 2000

Tuje kwenye macalculation sasa
2000+2000+3200+500+1000+1000+2000= 11,700/=

Inazidi hadi pesa unayipata kwenye maokoto yako kwa siku. Hapa ninazungumzia wale wote wenye kuingiza elf 10 kwa siku na Wala si wale wenye kuingiza chini ya hapo. 😂😂😂

Hivi kweli kabisa Mh.Rais hii serikali yako inamfikilia mwananchi wa hali ya chini kama Mimi ama mnatuona wote tupo sawa na nyinyi katika maokoto yenu?

Je, kwa mtazamo wa harakaharaka huyu mtu ataweza kumudu gharama za BIMA yako kweli Mh. Rais wangu?

Kumbuka anao watu Wanao mtegemea nje ya familia yake inayomzunguka kama vile baba mama na ndugu zake wengine wapembeni wasio na uwezo. Pia Kuna mawifi mashemeji na wakwe zake.

Mh. Rais katika hili mnaleta masihala kwa watanzani wa hali ya chini, hapa ndipo tunasema aliyenacho hataki kumkumbuka asiyenacho.
Yote hii ni kuwatoa watu kwenye mjadala wa DP World! Tuache kupiga kelele kuhusu waarabu na bandari zetu na tujadili bima. Walianza na katiba ni kijitabu na Sasa wameleta bima. Pumbavu sana!
 
Yani ni mara elfu wangeweka bima ya afya iwe bure kisha waingize tozo ya bima kwenye line za simu. Walau hapo wangekuwa wamefikiria kikubwa.

Maumivu ya Tozo yangekuwepo ila mtu akienda hospitali anapata huduma bure bila kuchajiwa haileti ukakasi. Kupitia tozo za miamala serikali ilikuwa ina raise hela ya kutosha sana kwa mwaka kuliko hizo rates za kinyonyaji. Sijui wamefikiriaje ila kama matibabu yakiwa kupitia tozo za miamala.
Naunga mkono hoja na infact hiyo tozo ingewekwa maeneo mengi kama bima ya afya mfano kwenye bili ya maji, petrol, diesel, ushuru wa mazao, line za simu, luku, nk ila mtu akatibiwe Bure hospital. Ccm ni laana
 
Wenzao Ulaya ndio wanafanya hivyo.

Hulipishwi mlima kama wanavyotaka kutufanyia bongo ila unailipa in aggragates. Tatizo lingine bongo ni wizi na ufisadi. Wakati nyie mnakusanya maokoto kwa ajili ya huduma za afya. Kuna msenge atakuwa anachota sehemu ya hizo hela ananunua Apartments Dubai.
 
Naunga mkono hoja na infact hiyo tozo ingewekwa maeneo mengi kama bima ya afya mfano kwenye bili ya maji, petrol, diesel, ushuru wa mazao, line za simu, luku, nk ila mtu akatibiwe Bure hospital. Ccm ni laana
Mh. Ummy Mwalimu hii ni point ya kuichukua kwa maslai mapama na njia moja ya kukusanya maokoto mazuri pasipo kuwaumiza wachache Ila kwa manufaa ya kuwa na bima ya afya kwa wote.
 
Yote hii ni kuwatoa watu kwenye mjadala wa DP World! Tuache kupiga kelele kuhusu waarabu na bandari zetu na tujadili bima. Walianza na katiba ni kijitabu na Sasa wameleta bima. Pumbavu sana!
Inshu ya bandali ipo palepale tunasubili siku 30 zitimie. Tuna Imani na kina mdude na wengine katika kutuongoza siku ikifika
 
Maneno kutoka MMM wa X republic :-

UMMY, afya ya watoto wetu siyo biashara ya serikali.

Takwimu za uchumi wa Taifa zilizotolewa Juni (2022), zilionyesha 2021 jumla ya watanzania milioni 41 (41,448,117) walikuwa wagonjwa wa nje kwenye Hospitali, vituo vya Afya na zahanati nchi nzima. Hii ina maana 71.8% ya watanzania waliugua mwaka 2021.

Katika nchi ambayo raia wake 71.8% wanaugua kwa takwimu rasmi za serikali suala la Afya linatakiwa kuwa kipaumbele cha Serikali na kuchukuliwa kwa uzito mkubwa. Kitendo cha Serikali kujiondoa kwenye kuhudumia raia wake kwenye afya kwa namna yoyote ni kuumiza wananchi. Ni UKATILI.

#TotoAfyaKadi ni msaada mkubwa kwa watoto wengi wa Tanzania ambao familia zao hazina uwezo wa kugharamia matibabu. #TotoAfyaKadi ni kifurushi maalum watoto walipatiwa huduma kwa mwaka nmoja kwa gharama ya Sh50,400 lakini mfuko umesitishwa na wizara ya afya ya @ummymwalimu

NHIFTZ wanataka watoto wasajiliwe kama wategemezi kupitia vifurushi vya Bima ya afya au kupitia au kupitia shule wanazosoma. Ukweli ni kwamba ni idadi ndogo ya wazazi na walezi waliopo katika mfumo rasmi wa ajira na wenye uwezo wa kumudu gharama za vifurushi vilivyopendekezwa.

Wizara ya afya chini ya @ummymwalimu imeamua kuwaua watoto wa kitanzania wasiokuwa na uwezo wa kugharamia kifurushi cha Sh120,000 kwa ajili ya kupata matibabu. Huu nu UKATILI mkubwa sana kwa mtoto wa Tanzania.

NHIFTZ wanataka watoto wasajiliwe kama wategemezi kupitia vifurushi vya Bima ya afya au kupitia au kupitia shule wanazosoma. Ukweli ni kwamba ni idadi ndogo ya wazazi na walezi waliopo katika mfumo rasmi wa ajira na wenye uwezo wa kumudu gharama za vifurushi vilivyopendekezwa.

Ni kilio kikubwa sana, baada ya NHIFTZ kufuta kifurushi cha #TotoAfyaKadi na kulazimisha mzazi au mlezi kukata bima ya afya ya pamoja na watoto wao na gharama kupanda kutoka Sh50,400 hadi kufikia Sh120,000 kwa mtoto mmoja.

Kwanini mtoto alazimishwe kukata bima ya afya pamoja na mzazi au mlezi wake? Kama mzazi au mlezi sitaki kuwa na bima ya afya, mtoto wangu naye anapoteza haki na sifa za kuwa na bima ya afya kwa watoto?

Sehemu kubwa ya watanzania wamejiajiri katika kilimo kisichokuwa na faida kubwa au wapo kwenye sekta isiyo rasmi ambayo inachukua 52% ya nguvu kazi yote Tanzania. Watu walio katika ajira rasmi (kwenye sekta ya umma na binafsi) ni watu milioni 3.5 sawa na 14.2% pekee.

Kama sababu za kuondoa #TotoAfyaKadi ni NHIFTZ kukusanya Sh5 bilioni; fedha inayolipwa kwa watoa huduma (Matumizi ni Sh40 bilioni) kama anavyotueleza waziri wa afya, suala lingekuwa kuongeza wachangiaji kuwa wengi na siyo hao wachache wafutiwe huduma. Kosa.

Ushauri!

Unganisheni mfumo wa hifadhi ya jamii kwa kila mtanzania ili anapochangia hifadhi ya jamii awe anapata huduma ya afya moja kwa moja. Watanzania waunganishwe na NSSF ili kupanua fao la matibabu kutoka idadi ndogo ya sasa .

Serikali kupitia wizara ya fedha na mipango ihakikishe mikopo inayodaiwa kupitia mashirika ya Umma na Wizara kurudishwa haraka ili kuupa uwezo Mfuko wa Taifa wa Bima wa Afya (NHIFTZ) kujiendesha wenyewe.

Serikali isimamie uwekezaji unaofanya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuhakikisha unaleta tija katika mapato yake, kuimarisha misingi ya kulinda uhai wake na kuwafikia wananchi wengi zaidi ili kunufaika na huduma za matibabu bila kikwazo cha fedha.

Wananchi wapewe umuhimu wa kuwa na bima ya afya kabla ya kuugua hii itasaidia sana wao kuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu. Wananchi wapate elimu ya kutosha itakayowasaidia kufanya maamuzi ya kujiunga na kutumia huduma.

Wekeni mikakati mbalimbali ya kuelimisha wananchi kuelewa dhana ya bima ya afya na kuona umuhimu wa kujiunga na bima ya afya kwa usalama wa afya zao.

MMM, Martin Maranja Masese
 
Attachments

  • Screenshot_20230917-005955.png
    Screenshot_20230917-005955.png
    39 KB · Views: 11
  • 20230917_010130.jpg
    20230917_010130.jpg
    83.9 KB · Views: 2
Yani ni mara elfu wangeweka bima ya afya iwe bure kisha waingize tozo ya bima kwenye line za simu. Walau hapo wangekuwa wamefikiria kikubwa.

Maumivu ya Tozo yangekuwepo ila mtu akienda hospitali anapata huduma bure bila kuchajiwa haileti ukakasi. Kupitia tozo za miamala serikali ilikuwa ina raise hela ya kutosha sana kwa mwaka kuliko hizo rates za kinyonyaji. Sijui wamefikiriaje ila kama matibabu yakiwa kupitia tozo za miamala.
Tatizo sio upatikanaji wa ela tatizo ni ufujaji wa ela.Kwasababu ata uko Nhif pesa zimeliwa nakupeshana kiholela ndo maana mfuko umepasuka.
 
Mkuu achana nae,sembuse Kula kulala
Hao wajinga ndio wanaofanya nchi inadorora kila siku.Dawa sio kuwaacha maana wakiachwa wanazidi kua wengi,ndo hivyo nchi unakuta ina wajinga wengi werevu wachache.Tukatae ujinga popote tunapokutana nao.
 
Alisema lema anawaombea nyinyi wananchi muwe maisha magumu zaidi ili mpate akili ya kufanya mabadiliko
 
Back
Top Bottom