DOKEZO Serikali iangalie vizuri mfumo wa ajira portal, kuna dalili za wahuni kusimamia mfumo huu

DOKEZO Serikali iangalie vizuri mfumo wa ajira portal, kuna dalili za wahuni kusimamia mfumo huu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
SERIKALI IANGALIE VIZURI MFUMO WA AJIRA PORTAL, KUNA DALILI ZA WAHUNI KUSIMAMIA MFUMO HUU WA AJIRA.

Tarehe 13 Desemba, 2024 Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa imekaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi elfu tatu mia sita thelathini na tatu (3633).

Lakini baadhi waombaji wamekuwa wakiangaika na mfumo wa uombaji tangu siku ya kwanza mpaka leo.Baadhi ya changamoto katika uombaji wa ajira hizi ni ;

  1. :4Shrug: KUTOFAUTIANA SIFA ZILIZOAINISHWA NA WIZARA NA SIFA ZILIZOAINISHWA KWENYE AJIRA PORTAL

MFANO: Katika nafasi ya MWALIMU DARAJA LA III C - (FIELD CROP PRODUCTION) NAFASI 20
SIFA ZILIZOAINISHWA KWENYE PDF KWENYE WEBSITE YA WIZARA👉 MWOMBAJI Kuajiriwa mwenye Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo la kufundishia la Somo la Kilimo cha Bustani (Horticulture Production ’Agriculture general au Crop Production)

AU Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo la kufundishia la Somo la Kilimo cha Bustani (Horticulture Production, Agriculture general au Crop Production) pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vinavyotambulika na Serikali.

🔕 AU Wenye Stashahada isiyo ya Ualimu katika fani ya ‘’Horticulture Production ‘’Agriculture general au Crop Production’’. Waombaji ambao hawana somo la UALIMU ni lazima wawe tayari kupata mafunzo ya UALIMU baada ya kuajiriwa.​

TANGAZO HILO HILO KWENYE AJIRA PORTAL

Kuajiriwa mwenye Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo la kufundishia la Somo la Kilimo cha Bustani (Horticulture Production ’Agriculture general au Crop Production)

AU Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo la kufundishia la Somo la Kilimo cha Bustani (Horticulture Production, Agriculture general au Crop Production) pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vinavyotambulika na Serikali.​

🔕 AU Wenye Shahada isiyo ya Ualimu katika fani ya ‘’Horticulture Production ‘’Agriculture general au Crop Production’’. Waombaji ambao hawana somo la UALIMU ni lazima wawe tayari kupata mafunzo ya UALIMU baada ya kuajiriwa.

2. BAADHI YA WAOMBAJI WANAKUTANA NA MABADILIKO YA TAARIFA ZAO JAMBO LINALOASHIRIA MFUMO UNACHEZEWA.

👉Baadhi ya waombaji wanakutana na baadhi ya vyeti vyao kuondolewa au kupishanishwa taarifa za uzoefu kubadilishwa miaka.Mfano unakuta mtu Sehemu ya uzoefu unakuta imebadilishwa mwaka alioanza ni 2024 na kumaliza 2006.Na ikiwa hivi maana yake utakapotaka kuapply itakugomea.

👉Baadhi akaunti zinaondolewa picha.
Baadhi ya akaunti referees mmoja ameondolewa na kusababisha kubakia wawili na kwa maana hiyo mfumo hauwezi kukubali kuomba ajira.

3. UNAKUTA BAADHI YA NAFASI ZINAKUGOMEA HATA KAMA UNA SIFA ZOTE ZA KUOMBA KAMA ILIVYOAINISHWA.

Mfano katika nafasi ya MWALIMU DARAJA LA III C - SOMO LA BIASHARA (BUSINESS STUDIES) moja ya sifa iliyoainishwa ni uwe mWenye Shahada isiyo ya Ualimu katika fani ya Biashara/usimamizi wa biashara/Commerce/ Bookkeeping/ Business Administration/Business studies’’. waombaji ambao hawana somo la UALIMU ni lazima wawe tayari kupata mafunzo ya UALIMU baada ya kuajiriwa.

Chakushangaza mfumo unakataa kukubali maombi ya mtu ambaye hajasomea ualimu lakini amesomea kozi ya bachelor's degree of Business Administration in Marketing Management.

👉Serikali iweke muda wa kuruhusu waombaji kubadilisha baadhi ya taarifa za kitaaluma tofauti na sasa, jambo hili limekuwa na usumbufu mkubwa kwa watu waliokosea baadhi ya taarifa za kitaaluma.

👉Namba za simu zilizowekwa kutusaidia hazipokelewi kwa hivyo kuwa na ugumu katika kupata utatuzi wa haraka

MWISHO

Tunaomba serikali ifanyie kazi haraka changamoto zilizojitokeza ili watu wengi zaidi waweze kuomba

SERIKALI iangalie vizuri mfumo huu na kuusimamia vizuri kwa sababu unadalili ya kuwa na wahuni wenye lengo la kukwamisha wengine makusudi lakini pia hauwatendei haki watu wengine kulingana na jinsi walivyouseti.

Serikali iweke kitengo maalumu customer care ambao watapatikana wakati wote na wenye weledi wakuweza kuwasaidia waombaji wanapokwama.
 

Attachments

Back
Top Bottom