Ulitakiwa ujue kuwa Tanzania ni nchi iliyojengwa kwa msingi wa kutegemea huruma ya mungu kuleta mvua. Mgao wa umeme leo unaupta kutokana na kukosekana kwa mvua ya kutosha. Kilimo cha Tanzania pia kinategemea mvua. Sasa kama hakuna mvua, na nchi yetu haina utaratibu wa kutunza nafaka, huwezi kumalumu mkulima huko kijijini kuwa kwa nini hakutunza nafaka za mwaka jana ili zimsaidie mwaka huu. Madai ya mito na maziwa kuwapo nisimplistic sana kwa sababu mtu wa Dodoma hawezi kulima kwa kutegema maji ya mto au ziwa lolote. Hakuna infrasrutcture yoyote ya irrigation. Na kwa taarifa yako, hata kwenye nchi zinazotumia irrigation, bado huwa wakulima wanalalamika iwapo kutakuwa na kiangazi kikubwa sana kwa sababu maji yote wanayomwagilia mashambani yatakuwa yanayeyushwa na jua.
Katika dunia ya kisasa, majanga ya kiasili yanasimamiwa na serikali, na ukosefu wa mvua ni mojawapo ya majanga ya kiasili ikiwa ni pamoja na vumbunga na kunyesha kwa mvua nyingi za kusababisha mafuriko.
La kushangaza, utaiona serikali yako inatoa pesa za kufidia wafanyabisahara eti "bail out" kutokana na mtikisiko wa mfumo wa fedha duniani, lakini serikali hiyo hiyo haina akiba ya kukabililina na mtikisiko wa asili, kama ukosefu wa mvua na mafuriko.