Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
- Thread starter
-
- #21
mi naona kitu muhimu ni kurahisisha njia ya usafirishaji wa chakula kutoka mahali kilipo na kukipeleka sehemu ambayo wanashida ili kupunguza ulanguzi kama sasa hv ukienda magengeni unaambiwa pilipili moja tsh 50 yaan maeneo ya mjni hali ni mbya sana
Halafu wakuu hivi baada ya miaka 50 ya uhuru still a measure ya uwepo wa chakula ni the ol equation ya uwepo wa MAHINDI??????? yaani mahindi maharage mpaka lini?
Nina uhakika kuwa watanzania wanauza sana nafaka nje ya nchi,zaidi ya tani laki tano.Tatizo ni bei,serikali ikishusha,wafanyabiashara wata-export.Nyie subirini tu.. watu watasema ooh mnaombea mambo mabaya yatokee n.k ili mpate cha kusema; kweli kabisa watu wakianza kupata shida kweli ya chakula hatutaki watu kuanza kusema "hatukujua", "hali ya chakula duniani iko nje ya uwezo wetu"
Ompunga pia!
Kwa nini njaa iwe ni ya kujitakia, au jibu lako linatoka mdomoni mwa mtu yule yule kuwa "NI KIHEREHERE CHAO"Huo mgawo wa chakula ni kosa kubwa sana. Watu watakuwa wavivu. Tanzania ardhi ipo, mito ipo, maziwa yapo. Njaa Tanzania ni ya kujitakia
Kwa nini njaa iwe ni ya kujitakia, au jibu lako linatoka mdomoni mwa mtu yule yule kuwa "NI KIHEREHERE CHAO"
acha kejeli, nimekupa sababu ni kwa nini njaa bongo ni ya kujitakia
Mkuu naona umelewa na Ujamaa na legacy ya mwalimu Nyerere.Ulitakiwa ujue kuwa Tanzania ni nchi iliyojengwa kwa msingi wa kutegemea huruma ya mungu kuleta mvua. Mgao wa umeme leo unaupta kutokana na kukosekana kwa mvua ya kutosha. Kilimo cha Tanzania pia kinategemea mvua. Sasa kama hakuna mvua, na nchi yetu haina utaratibu wa kutunza nafaka, huwezi kumalumu mkulima huko kijijini kuwa kwa nini hakutunza nafaka za mwaka jana ili zimsaidie mwaka huu. Madai ya mito na maziwa kuwapo nisimplistic sana kwa sababu mtu wa Dodoma hawezi kulima kwa kutegema maji ya mto au ziwa lolote. Hakuna infrasrutcture yoyote ya irrigation. Na kwa taarifa yako, hata kwenye nchi zinazotumia irrigation, bado huwa wakulima wanalalamika iwapo kutakuwa na kiangazi kikubwa sana kwa sababu maji yote wanayomwagilia mashambani yatakuwa yanayeyushwa na jua.
Katika dunia ya kisasa, majanga ya kiasili yanasimamiwa na serikali, na ukosefu wa mvua ni mojawapo ya majanga ya kiasili ikiwa ni pamoja na vumbunga na kunyesha kwa mvua nyingi za kusababisha mafuriko.
La kushangaza, utaiona serikali yako inatoa pesa za kufidia wafanyabisahara eti "bail out" kutokana na mtikisiko wa mfumo wa fedha duniani, lakini serikali hiyo hiyo haina akiba ya kukabililina na mtikisiko wa asili, kama ukosefu wa mvua na mafuriko.
Mkuu naona umelewa na Ujamaa na legacy ya mwalimu Nyerere.
All in all narudia tena, Tanzania hakuna njaa, njaa yetu ni ya kujitakia. Serikali kuanzisha mgawo wa chakula ni kuendeleza uvivu na umaskini.
you don't give a man fish, you train him how to fish
Mkuu, naona wewe unaishi katika dunia ya ndoto kiasi kuwa unaamini kuwa kila atakayekosa serikali ya leo Tanzania ni kwa sababu ya Ujamaa na Legacy ya Mwalimu Nyerere. Je ni kweli kuwa serikali yetu ya Tanzania ya leo imeshtrain watu wake namna ya kufish? ( kwa maana ya kujenga infarastructure za muhimu kwa watu kujifanyia mambo unayoota). Na je hata umeshajiuliza tena kwa nini kuna mgao wa umeme Tanzania? Je unajua kuwa wakulima wa USA hulipwa fidia na serikali yao iwapo hali ya hewa itakuwa mbaya?
ba
Yaani huyo mkulima ambae anakaa karibu na bonde la mto ama ziwa unataka akae aisubiri serikali imletee vifaa vya umwagiliaji? sio kila kitu tusubiri serikali ifanye kuna vingine ni sisi wenyewe twahitaji tuchaji akili zetu na maarifa. Nina shamba la eka80 karibu na mto nimenunua pump na singojei mvua. Saa nyingine mnaionea serikali, yote hii ni legacy za ujamaa. Wake up people
Naona mwenzangu unaongea mambo hypothetical sana. Jibu lako hilo ni exactly sawa kabisa na lile la Kikwete kuwa "SIJUI kwa NINI NCHI YANGU NI MASKINI WAKATI INA KILA KITU." Inaelekea hujui kuwa injini ya maendeleo ya nchi ni serikali. Umeshasoma kwa kina historia ya maendeleo ya dunia? Unajua kwa nini Marekani uchumi ukiaharibika rais waliyepo madarakani anahaha? Je unadhani kuwa nchi zilizioendela ziliamka siku moja tu na kuwa hivyo? Umewahi kupima tofauti kati ya maendeleo ya nchi kama Botswana na Tanzania na ukajiuliza kwa nini Botswana iko mbele ya Tanzania kiuchumi?
Swala hapa siyo legacy za Ujamaa. Mimi ninafanya biashara katika nchi ambayo ni baba wa ubeprai, na ninajua role ya serikali katika kuendesha uchumi wa raia mmojammoja na nchi nzima kwa jumla. Nimekuuliza kama unajua kuhusu serikali ya Marekani kuwalipa wakulima wake wakati hali ya hewa ikiwa mbaya, hujanijibu.