Serikali ianzishe mara moja biashara ya kusafirisha abiria mikoani

Serikali ianzishe mara moja biashara ya kusafirisha abiria mikoani

jitombashisho

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2020
Posts
667
Reaction score
2,245
Naitaka Serikali ifufue na ianzishe upya Shirika la mabasi ili gharama za usafishirishaji ziwe rahisi.

Kwa kuliacha soko la usafirishaji abiria kuwa huru ndipo sasa gharama za kusafiri zimekuwa juu! Eti leo ili nifike kwetu IMALASEKO inanibidi niwe na kiasi kisichopungua elfu sabini (70000) hii ni hatari!

Waziri Kamwelwe shughulikia hiyo agenda na Watanzania wa kawaida watakuhifadhi katika vitabu vyao vya kumbukumbu.
 
Serikali na biashara? Hata huko nyuma iliishajaribu. Cha muhimu itengeneze mazingira wezeshi kwa wananchi wafanyabiashara wafanye biashara ya kiushindani na yenyewe ijikite kusimamia na kukusanya mapato. Biashara ambayo serikali itamudu ni biashara ya isiyokuwa na ushindani kama hii ya TANESCO na Rail.
 
Usafiri wa ndege uliofufuliwa na serikali gharama zake ziko juu kuliko ulivyokuwa binafsi wa fastjet.
Mashirika ya serikali hayana ufanisi. Sio kila kitu serikali ifanye. Soko huru ndio linaweza kuamua bei kama kukiwa na ushindani mzuri sokoni.
 
Serikali na biashara? Hata huko nyuma iliishajaribu. Cha muhimu itengeneze mazingira wezeshi kwa wananchi wafanyabiashara wafanye biashara ya kiushindani na yenyewe ijikite kusimamia na kukusanya maato. Biashara ambayo serikali itamudu ni biashara ya isiyokuwa na ushindani kama hii ya TANESCO na Rail.
Nchi nyingi tu zimeweza kufanya biashara hiyo kwa ufanisi mkubwa;Rwanda kwa mfano.

Hoja hapo ni usimamizi tu.
 
Je, serikali ilipofufua ATCL na kununua ndege zake bei za usafiri wa ndege nchini zimeshuka au zimepanda?
 
Dar Dodoma iwe elfu kumi,dar Moro elfu mia tano, dar arusha elfu kumi na mbili,dar bukoba elfu ishirini. Dar mbeya elfu kumi na tano.
 
Zile bei elekezi za usafiri kwa Kilometer moja (km 1) Serikali izisimamie badala ya kufanya Biashara. Japo huwa ngumu Transporter kutekeleza ikiashiria kunatatizo.

LATRA (now) sijui huzingatia nini huku magari yanatofautiana ulaji wa mafuta kulingana na utofauti wa barabara hasa za vumbi zenye kiwango kimoja cha nauli kwa Km. Hii hufanya gari liendane na barabara husika
 
Nadhani badala ya serikali kuu kuingia moja kwa moja watumie shirika la posta ambalo tayari lina uzoefu kupitia basi walizo nazo kutoka songea kwenda njombe mpaka makambako.
 
Naitaka Serikali ifufue na ianzishe upya Shirika la mabasi ili gharama za usafishirishaji ziwe rahisi.

Kwa kuliacha soko la usafirishaji abiria kuwa huru ndipo sasa gharama za kusafiri zimekuwa juu!Eti leo ili nifike kwetu IMALASEKO inanibidi niwe na kiasi kisichopungua elfu sabini (70000) hii ni hatari!

Waziri Kamwelwe shughulikia hiyo agenda na Watanzania wa kawaida watakuhifadhi katika vitabu vyao vya kumbukumbu.
Wazo lako mbona serikali imetekeleza? Serikali imeanza na ndege kapande Kama usafiri wa serikali ni nafuu.
Kuhusu mabasi subiri sekta binafsi wakishindwa serikali itanunua mabasi Yake kwasasa endelea na hiyo 70K.
 
Nchi nyingi tu zimeweza kufanya biashara hiyo kwa ufanisi mkubwa;Rwanda kwa mfano.

Hoja hapo ni usimamizi tu.
Rwanda siyo nchi. Hata bashite ukimkatia kipande Cha dar chenye ukubwa Kama Rwanda awe rais anaweza kuanzisha mabasi ya serikali.
Pia kwa ukubwa wa Rwanda wanahitaji daladala tu.
 
Serikali tayari ina shirika la posta, linaweza kutoa hiyo huduma ya kusafirisha abiria, mizigo na vifurushi..
 
Mbona nimepanda Basi dogo kuokea Songea kuja hapa Makambako linamilikiwa na Posta?
 
Back
Top Bottom