Hakuna kitu kinaumiza kama msomi na mwalimu aliyesomea na kufuzu mafunzo ya ualimu na kwenda kufanya kazi katika shule za serkali kwa kujitolea bure
Hakika hii haikubaliki, ni unyonyaji wa kiwango kisichoelezeka. Mtu kufanya kazi bure ndani ya nchi hii ni kinyume na haki za binadamu kwamba kila mtu anahaki ya ajira na kulipwa
Ni vema serkali kupitia TAMISEMI ikaanzisha mfumo rasmi wa kuwataka walimu waihudumie serkali kwa malipo kidogo ndani ya mwaka mmoja.
Hii itasaidia kujenga uzoefu kwa walimu na kupunguza uhaba wa walimu, pia hakutakuwa na ukanjanja katika kada hii
Hoja yako ni ya msingi Sana mkuu,ajira zinatangazwa na kigezo kikubwa Cha kupata uwe unajitolea kiukweli hapo wanaumiza Sana unajitoleaje bure ,mda huo unakula kwa Nan,familia yako inaishije,kiukweli hapo serikal bado inahji kubadili mfumo huo..
Pamoja kwamba baadhi ya maneno yamenichekesha ila nakuunga mkono 100% kwa hoja yako .Na hii ingekuwa pia kwa fani nyingine zenye upungufi wa watumishi kama kilimo/ mifugo nk