SoC03 Serikali ianzishe utaratibu wa kuwashughulikia viongozi wa dini wanaohatarisha maisha ya watu

SoC03 Serikali ianzishe utaratibu wa kuwashughulikia viongozi wa dini wanaohatarisha maisha ya watu

Stories of Change - 2023 Competition

SEMBOJE

Member
Joined
Aug 31, 2017
Posts
7
Reaction score
11
Kutokana na madhara yanayoendelea kuwapata watu kutokana na mafundisho au maelekezo ya baadhi ya Viongozi wa Dini kwa ajili ya kutimiza haja zao au kutimiza mahitaji yao na matamanio ya mioyo yao, imepelekea kuathiri maisha ya watu kwa namna moja au nyingine.

Kutokana na athari hizo zinazo jitokeza nachukua nafasi hii kuishauri serikali kwamba ianzishe mfumo wa kuwashughulikia na kuwajibisha Viongozi hao wa Dini wanao pelekea watu kupata madhara katika maisha yao.

Kuna baadhi wa viongozi wa dini wametumia shida na matatizo ya watu kama magonjwa, nyota ya pesa na maswala ya ndoa pamoja na upungufu wa mahitaji ya mwanadamu kumnasa Mtu na kumpatia vitu vinavyoathiri maisha yake.

Mfano; kuna baadhi ya Viongozi wa Dini wanawashawishi na kuwajaza watu maneno kwamba ili kutoa Mikosi au Laana au Nuksi au kurudisha nyota iliyoibiwa au kuondokana na ufukara na ili upate pesa na utajiri lazima kunywa mafuta yao kwamba ameyaombea na tayari yana upako na kibali kwa Mungu, yaani mafuta ya kujipaka nje ya mwili ndio anayo wanywesha ili kutoa balaa hizo, ambavyo baadhi ya watu imewapelekea kupata matatizo na magonjwa mbalimbali katika afya zao; kama kansa pamoja na matatizo mengine. Jamani kwa namna hii tutapataje kupona tusipojali wokovu mkuu.

Si hilo tu pia kuna viongozi wengine wanatumia njia ya kumwaga mafuta kwenye viwanja vya mikutano na viwanja vya kufanyia semina viongozi hao wachache wa dini wanawahakikishia watu na kuwaeleza kuwa atakaye fanikiwa kukanyaga alama ya mafuta yalipopita wakati anayamwaga kwa kunyunyizia atakuwa tayari amefanikiwa kupata majibu ya mahitaji yake, yaani kama ni mgonjwa atapata uponyaji, kama nyota iliibiwa itakuwa imerudi na maisha yake yatabadilika kabisa pia Laana au Mikosi au Shida zake au Matatizo yaliyokuwa yamemsonga pamoja na kuwa na Maisha magumu ndio itakuwa kwa heri hawatayaona tena.

Sasa kutokana na msongamano wa watu au mrudikano wa watu na wingi wa watu na kila mmoja ana shida zake pia anatamani apate wanaamua kukimbilia sehemu ya ardhi iliyoangukiwa au kumwagikiwa na mafuta hayo kwa lengo ya kuyakanyaga. Sasa kutokana na ile “spidi” ya kukibilia eneo lililoangukia mafuta na kutofautiana kwa “pawa” wanajikuta wanasukumana na kuanza kukanyagana wao kwa wao. Matokeo yake wanaanza kuumizana wao kwa wao na baadhi yao wanapoteza maisha yao kabisa. Jamani kwa namna hii tutapataje kupona tusipojali wokovu mkuu.

Lingine pia ni kwamba kuna baadhi ya viongozi wa dini hutoa maelekezo juu ya kufunga swaumu, maelekezo yao yanakuwa kwamba inatakiwa kila mmoja afunge siku arobaini ( 40 ) bila kula chochote wala bila kunywa chochote siku 40, Kwamba tufuate kielelezo alichotuachia Bwana wetu Yesu Kristo naye alifunga siku siku 40 au anasema tufunge bila kula chochote wala kunywa chochote hadi tumuone Mungu au Yesu, waumini wake nao wanaanza kutekeleza tamko la kiongozi wao wanaanza kufunga bila kula wala kunywa matokeo yake watu wanaanza kudhoofika na wengine wanapoteza maisha yao kabisa. Jamani hii ni hatari kabisa kwa namna hii tutapataje kupona tusipojali wokovu mkuu.

Pia tukio lingine la baadhi ya viongozi wa dini ni kwamba huwafundisha waumini wao kuwa wakila nyasi watapata yale wanayohitaji; yaani mtu kabisa anakula nyasi kama wanyama yaani kama mbuzi au ng’ombe na n.k Jamani kwa namna hii tutapataje kupona tusipojali wokovu mkuu.​

NAMNA YA KUFANYA ILI KUTHIBITI JANGA HILI LINALO ZIDI KUWA NA NGUVU​

Serikali pamoja na wataalamu wa afya watoe wito wa dharula kwa Viongozi wote wa dini ili kuwakutanisha na kuanza kutoa elimu juu ya madhara ya kunywa mafuta yaliyotengenezwa kwa ajili ya matumizi ya nje ya mwili afu wao wanawanyesha watu wawaelezee madhara ya kunywa mafuta hayo.

Serikali ipige marufuku na kutoa onyo kali juu ya viongozi wa dini wanaotumia kuwanywesha watu mafuta ya kujipaka na kuchukuliwa hatua.

Serikali iwaamulishe viongozi wa dini wanao tumia kumwaga mafuta chini, watumie utaratibu mzuri hata kwa kuwapanga mstari ili wasikanyagane au serikali iondoe kabisa matumizi ya kukanyaga mafuta.

Au serikali pamoja na viongozi wa dini wanao husika kusajili makanisa wakae kwa pamoja na wajadili namna gani ya kufanya au waanzishe mfumo mpya wa kusajili madhehebu, huku wakianzisha sheria au katiba ya kusajili makanisa.

Na ndani ya katiba hiyo ziwemo sheria za kutokutumia vitu kama mafuta au vitu vingine vinavyoweza kuleta madhara kwa binadamu, ili pia Kuepuka kuwaingizia watu gharama na kuepuka madhara yatakayotokea katika afya zao kwa mda mfupi au baadae.​
 
Upvote 6
Back
Top Bottom