Serikali iatamie wahitimu wenye ujuzi kwa rasilimali wezeshi mtu mmoja mmoja na si vikundi chini ya usimamizi ya timu ya wataalamu wa halmashauri.

Jerry Farms

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
202
Reaction score
167
Vijana na kinamama wameonekana kuwa na kusitasita kujiunga na vikundi kutokana na takwa la kulipa deni la mtu yoyote atakae tokomea mara baada ya kupatiwa mkopo toka katika pesa ya kikundi. Hivyo n wakati sahihi sasa kwa serikali kuja na mpango kabambe wa yenyewe kuwa msimamizi mkuu wa vijana, kinamama na watu wenye mahitaji maalumu wanaowezeshwa na mifuko ya halmashauri.
Mpango mkakati ni kwa serikali yenyewe kuwa ndie muajili wa mnufaika wa pesa ya kuendeshea shughuli yake.
Serikali itakua muajiri na msamimizi kwa kupitia timu ya wataalamu wake walioko katika halmashauri zetu kwa kufanya yafuatayo:
Kupitia nyaraka zote za andiko la mradi lililowasilishwa na mtu anaehitaji usaidizi wa rasilimali katika kutimiza lengo/mradi wake.
Kutoa mapendekezo yao ya kitaalamu juu ya mradi.
Kutoa rasilimali wezeshi kwa awamu awamu kwa mnufaika. Mfano mnufaika amekuja na mradi wa kilimo; Pesa itatoka kwa mtiririko ufuatao;
A:Awamu ya kwanza
1-Pesa ya maandalizi ya shamba, upimaji udongo n.k
2- Ripoti ya kazi toka kwa mnufaika wa rasilimali wezeshi kwenda halmashauri.
3- Kaguzi ya wataalamu wa halmashauri( bwana/bibi shamba).
B:Kuidhinisha fedha na rasilimali zingine wezeshi kwa awamu ya pili katika mradi.
Hapa wataalamu watatoa tena rasilimali hizi kwenda kwa mnufaika na kuendelea na taratibu kama zilivyoorodhesha juu.
Kwa kufata mtiririko huu, wenye ujuzi na wanufaika wa rasilimali fedha toka halmashauri wataweza kuenda sawa na miradi na hivyo kurejesha pesa kwa wakati katika halmashauri zetu.
Malalamiko ya wenye ujuzi kukaa na ujuzi wao pasipo kuufanyia kazi yatakoma.
Watendaji watatumia kwa ukubwa( maximum), zoea la kukaa ofisini litakoma, sasa tutakua na watumishi wa site.
Utoaji wa ujuzi pasipo rasilimali wezeshi zingine ni "sawa na kukimbiza mmbwa huku unacheka", katu hutompata( msemo maarufu saana wa kisukuma). Utolewaji wa elimu- ujuzi uambatane na rasilimali wezeshi ambazo zitasimamiwa na wataalamu na waajiriwa wa kudumu toka halmashauri.
Wataalamu hawa wapimwe kwa matunda ya kazi zitakazokua zikionekana toka kwa wanufaika wa rasilimali wezeshi toka halmashauri/ kwenye mashirika ya wahisani.
Rasilimali wezeshi zitolewe kwenda kwa wanufaika awamu kwa awamu. Mnufaika asipewe pesa yote kwa mkupuo na kuenda kujisimamia( wengi wanashindwa) hivyo kukwamisha adhima nzuri ya serikali katika kuwakwamua wananchi wake katika umaskini.
Ujuzi uendane na uwezeshaji unaosimamiwa kikamilifu na wataalamu wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…