PAZIA 3
JF-Expert Member
- Jan 30, 2018
- 1,102
- 1,919
Naandika kwa kujiamini kwasababu ni mzima wa afya, na natumai hata msomaji wangu u mzima.
Pamoja na changamoto nyingi za maisha, lakini yatupasa kumshukuru M /Mungu maana yeye ndiye atupaye akili za kufikiri.
Baada ya UTANGULIZI huo, ngoja nijikite kwenye mada.
Bila shaka, Kama wewe no mfuatiliaji mzuri wa pesa inayoachwa na serikali kupitia harimashauli zetu, 10% ya mapato kwa ajili ya vijana na wanawake , imekuwa ikitumika sivyo kwa kipindi kirefu sasa. Lakini pia kusema ukweli pesa hii inapotea jumla baada ya kutoa mikopo, hii nikwasababu ya namna inavyotolewa. Sijawahi kusikia serikali ikizungumzia mrejesho wa pesa hizo. Pesa hiyo haina usimamizi mzuri ndiyo maana wanaoifaidi ni watendaji wa harimashauli hizo.
Kila mwaka pesa inatolewa na bado mwamko wa vijana kuikopa hiyo pesa ni mdogo. Hata wanaofanikiwa kuchukua mkopo huu bado hawarejeshi, pesa hii imekuwa Kama pesa ya TASAF. Serikali imekosa wazo mbadala la namna bora ya utoaji wa pesa hii. Mpango huu unazidiwa na ule wa Bodi ya mikopo ya wanafunzi, wao angalau wanaipata pesa kadhaa kutoka kwa wanufaika kuliko hii ya kwenye harimashauli. 10% inatolewa kwa interests za kisiasa kufurahishana lakini ukweli ndiyo hivyo, wachache ndiyo wanaifaidi pesa hii na viongozi wote wanajua hilo.
NINI KIFANYIKE
1. Tuachane na mpango huu kwa maana ya kufurahishana huku tukinufaisha wachache na kuumiza wengine. Ikumbukwe pesa hii inatokana na Kodi,too, michango mbalimbali inayokusanywa na harimashauli kutoka kwa Vijana haohao na wanawake haohao.
2. Pesa hii ikusanywe Kama kawaida Kupitia harimashauli, Kisha irudi kwa namna nyingine tofauti na kuwakopesha vijana au wanawake ambayo tumekwisha kuona uhuni uliopo, badala yake irudi kwenye masoko yetu hayohayo au minada yetu kwa namna hii;-
- Baada ya makusanyo au kutengwa kwa pesa hii, itungiwe sheria ndogo ili isipotee bure
- Sheria hiyo iongoze harimashauli kuboresha masiko yake ikiwemo kuyawekea Rami katikati ya soko kwenye barabara zake, kujenga mitalo ya maji, maeneo ya kutunza taka nk.
- Pesa hiyo itumike kugharamikia uendeshaji wa masoko hayo ili kuondoa ushuru mdogo mdogo Kama vile ushuru wa walinzi, wafagiaji, wazoa taka , vyoo vya kulipia nk. Pesa hii itasimamia vyote hivi. Haiwezekani soko nilakwetu, choo kijengwe na harimashauli yetu Kisha tuwe tunalipia. Pesa hii ikirudi, iondoe aibu ya masoko yetu kuwa na TOPE kipindi Cha mvua, iondoe aibu ya masoko kuwa na VUMBI la kutupwa, iondoe aibu ya wajasilia Mali kupanga vitu kwenye tope na VUMBI Badala yake waandaliwe vichanja au meza nzuri.
10% ikayapambe masoko yetu na minada yetu ili vijana wengi na wanawake wanufaike na masoko yao.
FAIDA ZINGINE ZA KUBADILISHA MATUMIZI YA 10%
MWISHO
Viongozi wachukue ushauri wetu huku kwenye mitandao lakini wafanye tafiti vizuri kabla ya kuchukua maamzi, isije wakafanya Mambo yanayoteteresha jamii Kama ilivyotokea kwenye suala la TOZO.
- Pia niwaombe viongozi wa jamiiforum kupitia mada zote Kisha zile zinazokidhi vigezo, mziweke hadhalani, mzitangaze kuwa hizo ni makala pendekezwa kupitia kurasa zenu mitandaoni, zichapishwe kwenye magazeti na watu wapewe nafasi ya kupiga kura kuliko kuangalia tu VOTES za hapa ambapo Nina uhakika mtaacha makala nzuri zenye faida zaidi.
Ahsanteni

- Vijana wengi watajiongeza kufanya ujasiliamali kwasababu uhakika wa masoko utakuwepo
- Harimashauli zitaheshika na kuvutia watu wengi kufanya biashara
- Mzunguko wa pesa utaongezeka kwasababu pesa hii itarudi kwenye Harimashauli kuliko kuwaachia watu wachache waifaidi
- Pesa hii itaboresha hata viwanja vya mipira nakuwafanya vijana hao kujifanya mazoezi na kutengeneza team nzuri zitakazoibua vipaji vyao
- Usafiri utakuwepo wa kutosha kwasababu ya kuwepo kwa miondo mbinu mizuri hivyo kuwavutia wafanyabiashara kuleta daladala kwenye harimashauli hizo, itasaidia kupunguza kusafiri kwa gharama kubwa maeneo ya karibu kwa gharama za bodaboda

Upvote
1