Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Amani iwe Kwenu
Benki kuu (BOT) imeshatoa takwimu kuonesha mfumuko wa bei umeongezeka kwa zaidi ya asilimia 1 ndani ya miezi michache. Sasa mfumuko unafikia asilimia 4 na ushei.
Dunia nzima sasa inaputia wakati mgumu kiuchumi hususan kipindi hiki cha mtanange wa kule Ukraine.
Kwa serikali inayojali ustawi na hali bora za raia wake inawajibika kuangalia kwa tahadhari mwenendo wake wa matumizi hasa kuweka umhimu kwenye kukabilii ukali wa maisha unaozidi kupanda kila siku. Kuna mambo ambayo tunaweza kuyazingatia au kuyafanyiakazi katika kuikabili hali hii ngumu
1. KUBANA MATUMIZI
Serikali ibadili vipaumbele vya matumizi yake hasa izingatie ununuzi wa bidhaa kutoka nje hususani usafiri, samani na mahitaji ya kiteknoljia yazingatie ukwasi uliopo na kupunguza kutumia sana dola ili iweze kuwa na hifadhi ya kutosha
2. DHAHABU
Serikali itunge sheria ya kuiwezesha BOT kuanzisha hazina ya dhahabu ambapo iweze kuwa na hifadhi yake ya dhahabu ambayo itatumika rasmi kama kigezo cha ukwasi sambamba na foreign currency
3. MISHAHARA NA POSHO
Serikali iboreshe mishahara ya wafanyakazi wake iendane na uhalisia wa kukabili mfumuko wa bei ambao imeshindwa kuudhibiti kwa sababu ya kuwafuta machozi wafanyabiashara wa mafuta ambao walibanwa vilivyo na regime iliyopita
Serikali iondoe utitiri wa masurufu na posho kwa shughuli za kiofisi za watendaji wake na kupunguza msururu wa idadi ya delegates wanaosafiri nje. Mabalozi watimize wajibu wao kwa sababu itasaidia kubana matumizi
4. MIRADI
Serikali itathmini miradi yake ya kimkakati iendane na mahitaji makuu ya kimsingi. Kwa mfano ujenzi wa moundombinu ni muhimu sana kutokana na jiographia ya nchi yetu lakini kununua ndege mpya sidhani kama mradi huo una umuhimu mkubwa kwenye kipindi hiki. Pesa ipelekwe kwenye kununua chakula,mafuta na madawa ili kuhakikisha taifa halitetereki kwenye kipindi hiki kigumu
5. TRADE
Serikali ipeleke muswada wa dharura bungeni unaohusu masuala ya exports ambapo sheria iweke unafuu na kuwapatia ruzuku wafanyabiashara wanaosafirisha bidhaa nje.
Serikali iimarishe ulinzi wa sheria za kibenki ambapo akaunti za wafanyabiashara zisigeuke fimbo za kuwachapia na wanasiasa. Wataalam wa fedha hapa waumize kichwa kuhakkkisha usalama wa wawekezaji nchini unaanzia kwenye mazingira hadi ulinzi wa mitaji yao benki.
Muswada wa uanzishaji wa viwanda na biashara nchini uendane na hitaji ya soko la dunia. Kwa mfano hivi leo mitishamba ama tiba mbadala zina demand kubwa duniani hivyo uchakataji, uhifadhi na usafiri wake uzingatie I.S.O. na serikali kisheria ifabikishe hilo ili kuongeza forex ndani ya nchi
6. KODI
Serikali irekebishe sheria ya kodi kwa kuondoa msururu wa kodi kwa muda ili kussidia startups na kodi hizi zihusu startups peke yake lakini iweke kiwango nafuu kwa kodi ili wananchi walipe kwa ufahari ambapo tofauti na sssa kodi inawabana koo Watanzania na Wafanyabiashara
7. VITUO VYA UTAFITI
Serikali ianzishe vitengo vya utafiti aina mbalimbali ndani ya majeshi yetu na iruhusu raia kupeleka mawazo ama tafiti zao huko ili kufanikisha uvumbuzi ama maboresho ya bidhaa zenye tija kwa jamii...