SoC04 Serikali ichukue hatua madhubuti kudhibiti utengenezaji na usambazaji wa pesa bandia

SoC04 Serikali ichukue hatua madhubuti kudhibiti utengenezaji na usambazaji wa pesa bandia

Tanzania Tuitakayo competition threads

shalanie

New Member
Joined
May 24, 2024
Posts
1
Reaction score
1
Kumekuwa na utiriri wa pesa nyingi za bandia mtaani noti pamoja na sarafu za mia tano serikali inatakiwa kufanya yafuatayo ili kuondokana hali hii

I) KUELIMISHA UMMA
Uhamasishaji unatakiwa kufanyika ili kuwaelimisha wananchi jinsi ya kutambua pesa halisi na pesa bandia hii ni pamoja na vipindi maalumu kwenye vyombo vya Habari, mashuleni, masoko mbalimbali pamoja na mafunzo kwa wafanya bihashara.

ii) KUTUMIA MALIPO YA KIELETRONIKI
Kuhamasisha matumizi ya malipo ya kieletroniki kama vile kadi za benki, malipo kupitia simu. Hii inaweza kupunguza utegemezi wa pesa taslimu, hivyo kupunguza nafasi ya pesa bandia.

iii) UBORESHJI WA TEKNOLOJIA YA USALAMA WA NOTI
Serikali kushirikiana na benki kuu wanatakiwa kuhakikisha kuwa noti zina vya juu vya teknolojia ya usalama kama vile alama za maji, mchanganyiko maalumu wa rangi. Hii itafanya iwe vigumu zaidi kwa wahalifu kuzalisha pesa bandia.

iv). USHIRIKIANO KATI YA BENKI, SERIKALI NA VYOMBO VYA USALAMA
Ushirikiano kati ya baenki, vyombo vya usalama na mamlaka za serikali ni muhimu ili kichukua hatua za kisheria dhidi ya watengenezaji na wasambazaji wa pesa bandia. Operesheni na mipango ya pamoja inaweza kusaidia kukamatwa kwa wahusika na kufunga mitandao yao.

v) KUKAGUA MASHINE ZA ATM NA POS
Mabenki na watoa huduma za kifedha wanatakiwa kukagua mara kwa mara mashine hizi ili kuhakikisha kuwa hazitumiki kusambaza pesa bandia. Bali mashine hizi zinatakiwa kuwa na uewezo wa kutambua pesa bandia na kuzikataa.

NB: kwa kuchukua hatua hizi kwa pamoja, inaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la pesa bandia na kuhakikisha usalama wa mfumo wa fedha.
 
Upvote 1
NB: kwa kuchukua hatua hizi kwa pamoja, inaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la pesa bandia na kuhakikisha usalama wa mfumo wa fedha.
Kuna wakati nilikaa kuwaza hivi ni kwa nini pesa bandia ziwe ni kitu kibaya kwa nch🤔i!?

Nikagundua sababu kuu ni kwamba haipaswi mtu kupata fedha bila kusambaza huduma au bidhaa ya thamani kwa taifa. Fedha ni kama vyeti kuthibitisha mtu huyu amelichangia taifa thamani hivyo anaruhusiwa naye kutendewa vema.

Basi tuikuze tafsiri ya pesa bandia iwe hata; Kulipwa mshahara wa huduma fulani na haujaitoa ni pesa bandia, kulipwa posho ya kikao ambacho hata hamjatolea uamuzi wa kueleweka kuwa ni pesa bandia. Pesa na ubashiri nazo sijui tuziweke humo!???🤫🤔. Kwani afisa ubashiri amezalosha nn cha kulipwa??? Anyway ubashiri ni kama upatu, aliwachangia wenzie naye leo amechangiwa.

AHsante mdhibiti pesa bandia, naomba mawazo yako katika mawazo yangu bro. Ukipata wasaa
 
00 hizi kubwa kabla ya hizi mpya 15 shilingi laki na 50

nina 5000 hizi kubwa kabla ya hizi mpya 2 shilingi 10000

nina 2000 hizi kubwa kabla ya hizi mpya 1 shilingi 2000

nina 1000 hizi kubwa kabla ya hizi mpya 1 shilingi 1000
jumla =======163000
nipeni utaratibu ni bahasha yangu ya 2007 nimezikuta nipokilimanjaro now
 
Back
Top Bottom