Serikali ichunguze mauzo ya tiketi mechi ya Simba na Azam ya 17/9/2016.

Serikali ichunguze mauzo ya tiketi mechi ya Simba na Azam ya 17/9/2016.

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,703
Reaction score
1,724
Katika kipindi cha michezo cha Clouds FM mchana mchambuzi Ali Mayai alilalamika uwingi wa watu wakiwa nje na tiketi ilhali ndani ya uwanja hakuna nafasi. Kama tulivosikia serikali ya Uganda inachunguza mauzo ya tiketi kati ya timu ya taifa ya nchi hiyo na Comoro hivi majuzi kuwa mauzo hayakuzingatia idadi halisi ya uwezo wa uwanja. Ni jambo la hatari kama mchezo huu wa kuwauzia tiketi watu bila kujali idadi halisi inayotakiwa kiwanjani utaendeleo na serikali kufumbia macho!
Kama uwanja unaruhusu watu kumi basi ziuzwe tiketi kumi na si vinginevo.
Naomba serikali ichunguze jambo hili na kuwawajibisha wahusika.
 
Hapo tatizo ni hao watu wanaowaamini na kuwaweka milangoni, hii inawahusu na polisi pia wanaokaa mlangoni.
Hawa wanachukua hela kwa watu ambao hawana tiketi na kuwaruhusu kuingia ndani, hapa lazima idadi itazidi uwezo wa uwanja.
 
Back
Top Bottom