A
Anonymous
Guest
Mimi ni Mkazi wa Kijiji cha Makurunge kilichopo Kata ya Kiluvya, Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, kero yangu ni uendeshaji mbaya wa Shule ya Sekondari Makurunge.
Shule inaendeshwa kikatili sana kwa wanafunzi na wadau waishio karibu na Shule. Vijana waishio hostel wanalazimishwa kubeba chakula kutoka hostel wakalie shule, kitu ambacho hakina uhakika wa usalama wa hicho chakula njiani.
Watoto wanachangishwa elfu mbili-mbili kwa madai ya usimamiwaji prepo, hivi kusimamia prepo napo kunahitaji mchango wa kumhamasisha Mwalimu?
Mbaya zaidi wamewapiga marufuku wale wa mama wanaouza vitafunwa shule wakati wa mapumziko, hii ni sawa kweli?
Wao ndiyo ilikuwa sehemu yao ya kujipatia kipato na umewapiga marufuku bila sababu za msingi. Kiufupi Wilaya ya Kisarawe ni kama hii shule wameitenga hawaifuatilii, na kama wanaifuafilia basi, kuna namna wanaogopa kuamua.
Shule ina mwalimu mkuu wa kike lakini maamuzi ya shule yanafanywa na makamu na mtaaluma tu na wanajisifia kabisa kuwa wao ndio shule.
Huyo mtaaluma ana madudu mengi anayafanya hadi wakazi wa karibu na shule wanajua lakini hakuna hatua zozote amewahi kuchukuliwa. Wanafunzi waliomaliza wakienda kuchukua vyeti vyao anawaomba ngono tena kwa madai kuwa ana hela.
Hivi Watoto waliopo hapo shuleni kuna imani gani kwamba hawatongozi au hawanyanyasi kingono? Kuna namna Serikali ya Wilaya ya Kisarawe wanahaja ya kushughulikia hili suala. Walimu wengi wanaikimbia shule wanakuja na kuhama kwasababu ya watu wachache wenye kujimilikisha shule kwa matakwa yao binafsi.
Mimi hili nimeshindwa kulifumbia macho kwasababu tusipolisemea ipo siku usaha utavuja na kutakuwa tumechelewa kulitibu jipu.
Mwalimu Mkuu yupo lakini ni kama hana say yoyote pale, kila kitu kinaamuliwa na makamu na mtaaluma. Mtaaluma ndio chanzo ha migogoro mingi pale shuleni. Anahaja ya kuhamishwa kabla hajaimaliza shule. Anamiliki hosteli mbili pale shule, ya kike na kiume.
Kiufupi yupo kimaslahi sana kuliko taaluma yake. Wanafunzi wanalalamika anafundisha matusi darasani, mifano anatoa ya yeye na mke wake.