HOJA Serikali ichunguze utendaji wa Uongozi wa Walimu wa Halmashauri ya Mji Korogwe, Walimu hatutendewi haki

HOJA Serikali ichunguze utendaji wa Uongozi wa Walimu wa Halmashauri ya Mji Korogwe, Walimu hatutendewi haki

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Walimu wa Halmashauri ya Mji Korogwe tunaomba kuwasilisha malalamiko yetu kwa umma labda yanaweza kufikia mamlaka za juu na kufanyiwa kazi kuhusu baadhi ya maamuzi yanayodaiwa kufanywa na Ofisi ya Afisa Elimu Msingi.

Kwanza ugawaji wa baadhi ya nafasi za uongozi na majukumu unafanyika kwa upendeleo, jambo ambalo limekuwa likiwakatisha tamaa walimu wengi wanaoamini kuwa vigezo vya haki na uwazi havizingatiwi.

Walimu waalihamishwa uhamisho wa ndani shule Moja kwenda shule nyingine zoezi hilo alilifanya mwezi wa tano 2026 na walilipa flat let milion Moja Moja kwa baadhi ya waallimu ilihali standing order inataka Mtumishi anapohamishwa alipwe disturbance allowance, Substence allowance na transport allowance.

Kupitia ujumbe huu, tunaomba Ofisi ya Rais – TAMISEMI, pamoja na mamlaka nyingine zinazosimamia utumishi wa umma, kulichunguza suala hili ili kubaini ukweli wa malalamiko haya na kuhakikisha walimu wote wanaostahili wanalipwa haki zao kwa mujibu wa sheria na taratibu za utumishi wa umma. Tunahitaji mazingira ya kazi yanayozingatia haki, uwazi na usawa kwa walimu wote.
 
Kule umesema huna kazi una depression ya mikopo huku unawalalamikia tamisemi which is which mkuu?
 
Back
Top Bottom