Serikali idhibiti uuzwaji holela wa Barakoa nje ya Hospitali

Serikali idhibiti uuzwaji holela wa Barakoa nje ya Hospitali

mzee wa mazabe

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2016
Posts
843
Reaction score
627
Nimepita pale KCMC barakoa zinauzwa kama nyanya pale getini, nimepita Benjamini Mkapa napo hivyo hivyo na sijajua kama na Mwanza pale Bugando hali ipo hivyo, hivi leo hii Serikali inafumbia macho wauza barakoa nje ya Hospitali halafu mnatafuta mitungi ya gesi, hivi mnajua ubora wa hizo barakoa zinazouzwa nje ya Hospitali zenu? Au mmetumwa kutumaliza kabisa?

Haiwezekani barakoa ziuzwe getini kama KCMC halafu ndani kuwe kumechafuka wagonjwa wa Corona, lazima kuna uhusiano. Wizara ya Afya embu toeni tamko mara moja tutaisha aisee.

1625734178432.png

Hizo barakoa zinaleta mafua si mchezo, ni Bora ufunge kitambaa puani kuliko kuvaa hizo barakoa.
Ila wabongo sometimes tunazingua Sana Kwenye maisha yetu
 
Barakoa zenyewe zunauzwa kama nguo yaani mteja anaishika na kuchagua

Wengine wana corona au hata TB sasa anapoishika na kuirudisha na kuchagua nyingine hapo ndio mtihani unapoanzia

Barakoa zote lazima ziwe zimefungwa na plastic ili mteja aifungue mwenyewe

Yaani zimemwagwa kama chupi
 
Feri ukienda kupanda pantoni wapo wengi tena wanatisha watu eti wanazuia kupanda pantoni kama usipovaa barakoa zao, maskini na wengine wana nunua kwa fujo,

Nadhani kuna ulazima wa kuangalia kwa jicho la tatu hizo Barakoa zinaleta mafua kwa wengi sijui ni zile nyuzi nyuzi zake au kuna lipi kubwa, sijuiiii.
 
Barakoa zenyewe zunauzwa kama nguo yaani mteja anaishika na kuchagua

Wengine wana corona au hata TB sasa anapoishika na kuirudisha na kuchagua nyingine hapo ndio mtihani unapoanzia..
Aisee Serikali waingilie hili mara moja tutakuwa tunatafuta mchawi bila kujua kumbe mzigo unakuwa upo getini tunauamishia ndani hospitali, Waziri wa Afya tafadhali tunaomba majibu ya jambo hili mara moja au mtuambie wanazipata wapi hawa watu wanaouza hizi barakoa nje ya Hospitali
 
Taratibu ni zile zile zilizotolewa na wizara ya afya.

-Vaa Barakoa
-Nawa kwa maji tiririka na sabuni
-Tumia "Santaiza".
-Epuka misongamano isiyo ya lazima.
 
Feri ukienda kupanda pantoni wapo wengi tena wanatisha watu eti wanazuia kupanda pantoni kama usipovaa barakoa zao, maskini na wengine wana nunua kwa fujo,

Nadhani kuna ulazima wa kuangalia kwa jicho la tatu hizo Barakoa zinaleta mafua kwa wengi sijui ni zile nyuzi nyuzi zake au kuna lipi kubwa, sijuiiii.
Mimi nikivaaga nahisi kama kuna tuvitu vitu vinaingia kwenye pua kwahiyo inaniradhimi nifunike mdomo niache pua wazi😁😁
 
Taratibu ni zile zile zilizotolewa na wizara ya afya.

-Vaa Barakoa
-Nawa kwa maji tiririka na sabuni
-Tumia "Santaiza".
-Epuka misongamano isiyo ya lazima.
Kwahiyo tununue zile za getini Hospitali kama walizifua usiku wakazianika kisha wakazipiga pasi wakatuletea kutuuzia getini unaona itakuwa sawa mkuu???
 
Barakoa zenyewe zunauzwa kama nguo yaani mteja anaishika na kuchagua

Wengine wana corona au hata TB sasa anapoishika na kuirudisha na kuchagua nyingine hapo ndio mtihani unapoanzia

Barakoa zote lazima ziwe zimefungwa na plastic ili mteja aifungue mwenyewe

Yaani zimemwagwa kama chupi
Tuliza mshono Dada
 
Kwahiyo tununue zile za getini Hospitali kama walizifua usiku wakazianika kisha wakazipiga pasi wakatuletea kutuuzia getini unaona itakuwa sawa mkuu???

Kwahiyo wanaonunua zile za getini wote wanapata korona? Msome Darwin Survival of the fittest - Only The string will survive.
 
Nimepita pale KCMC barakoa zinauzwa kama nyanya pale getini, nimepita Benjamini Mkapa napo hivyo hivyo na sijajua kama na Mwanza pale Bugando hali ipo hivyo...
Wewe unalipwa mshahara....wao ndo wanajitafutia mshahara hivyo.
 
Aisee Serikali waingilie hili mara moja tutakuwa tunatafuta mchawi bila kujua kumbe mzigo unakuwa upo getini tunauamishia ndani hospitali,Waziri wa Afya tafadhali tunaomba majibu ya jambo hili mara moja au mtuambie wanazipata wapi hawa watu wanaouza hizi barakoa nje ya Hospitali

Yaani ni ya kujitafutia halafu unaambiwa bila mask huingii inabidi ununue hata iliyojaribiwa
Haya ni majanga
 
Kama ni necessary nunua barakoa ambayo ni disposable na ilokuwa sterile(imepakiwa kwenye pakti na ipo sealed.Watu wanapaswa kunawa mikono kabla haijavaliwa na usiguse katikati mwa barakoa bali kwenye vishikizio vya masikio tu.

Ukinunua ya kitambaa na haiko sealed inatakiwa kufuliwa kwanza.Ikisha ipikwe kwenye maji moto yanayochemka ili kuua vijidudu na kukaushwa(air dried) ndio ipo salama.Barakoa ya kitambaa inapaswa kusafishwa/kubadilishwa kila siku ni muhimu ukiwa na zaidi ya moja!
 
Unapovaa barakoa ili kuziba mdomo na pua ina maana unazuwia virus wa corona wasikuingie mwilini mwako kwa njia ya mdomoni au puani,hii ina maanisha kua hao virus wanaweza kutua kwenye sehemu zako zingine za usoni,mfano virus wanaweza wakawa kwenye kidevu,paji la uso au shingoni,

Sasa unapoishusha Barakoa yako kidevuni,kwenye shingo au kwenye paji la uso kisha ukaja kuivaa tena mdomoni ina maana umewachukua wale virus waliokua kwenye sehemu hizo za usoni na kuwapeleka ndani ya mwili wako kwa kupitia puani na mdomoni kwani watakua wamechukuliwa na hiyo barakoa iliyokua imeshushwa kidevuni!

Kama unataka kuivua barakoa ,ni bora ukaiweka kwenye mfuko wa nguo uliyoivaa bila kuichanganya na vitu vingine,kama vile funguo,simu,au karatasi ya aina yeyote ile ambayo imepita kwenye mikono ya watu wengi,

Kama hutokua muangalifu basi hiyo barakoa inaweza kugeuka na kua kifaa cha kukuletea hao virus!
 
Barakoa zenyewe zunauzwa kama nguo yaani mteja anaishika na kuchagua

Wengine wana corona au hata TB sasa anapoishika na kuirudisha na kuchagua nyingine hapo ndio mtihani unapoanzia

Barakoa zote lazima ziwe zimefungwa na plastic ili mteja aifungue mwenyewe

Yaani zimemwagwa kama chupi
Tena wateja wana jaribisha kabisa [emoji25][emoji25] eee Mungu tusaidiye siye viumbe

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom