Unapovaa barakoa ili kuziba mdomo na pua ina maana unazuwia virus wa corona wasikuingie mwilini mwako kwa njia ya mdomoni au puani,hii ina maanisha kua hao virus wanaweza kutua kwenye sehemu zako zingine za usoni,mfano virus wanaweza wakawa kwenye kidevu,paji la uso au shingoni,
Sasa unapoishusha Barakoa yako kidevuni,kwenye shingo au kwenye paji la uso kisha ukaja kuivaa tena mdomoni ina maana umewachukua wale virus waliokua kwenye sehemu hizo za usoni na kuwapeleka ndani ya mwili wako kwa kupitia puani na mdomoni kwani watakua wamechukuliwa na hiyo barakoa iliyokua imeshushwa kidevuni!
Kama unataka kuivua barakoa ,ni bora ukaiweka kwenye mfuko wa nguo uliyoivaa bila kuichanganya na vitu vingine,kama vile funguo,simu,au karatasi ya aina yeyote ile ambayo imepita kwenye mikono ya watu wengi,
Kama hutokua muangalifu basi hiyo barakoa inaweza kugeuka na kua kifaa cha kukuletea hao virus!