Mwamba 777
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 2,055
- 3,535
Ili kukuza uchumi wa viwanda nchini na ili viwanda viendelee kuwepo, kuzalisha na kutengeneza ajira kwa watanzania ni lazma yafuatayo yatekelezwe;
Kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji, kama chanzo cha malighafi za kwenda viwandani
Tanzania ni nchi kubwa sana na sehemu isiyoishi watu (mapori) ni makubwa kuliko sehem waishizo watu. Serikali iuze ndege inunue matrekta ya kilimo, ndege za kumwagilia na kuunganisha mabomba na pamp za maji kutoka ziwa victoria, tanganyika na bahari ya hindi kwaajili ya umwagiliaji mashambani vijana wachape kazi. Hii itasaidia viwanda kukua na kuzalisha masaa 24 bila kupungukiwa malighafi na kusafirisha bizaa zizalishwazo nje ya nchi ambapo kiwanda kitapata faida na kuajiri watu wengi hadi kupelekea ongezeko la pato la taifa. Mfano wa nchi zinazofanya kilimo cha umwagiliaji na zinaongoza kwa uchumi wa viwanda duniani ni Israel, Cuba, USA na China.
Kilimo cha Ufugaji
Hapa wafugaji wapewe vipaumbele na wahamasishwe kwa kupewa madawa ya mifugo bure na watengewe maeneo maalum kwaajili ya ufugaji na machungio. Pia iandae na kutengeneza mashamba makubwa ya mifugo (ranches) za serikali yatakayo sapoti ufugaji wa mifugo mbalimbali kama; ng'ombe, punda, ngamia, kuku, nguruwe, nyuki, mbuzi, kondoo n.k, hivi vyote vitazalisha malighafi kama ngozi, maziwa, mayai, nyama na asali, ambapo vitapelekwa viwandani na kuzalisha bidhaa mbalimbali na zitauzwa ndani na nje ya Tanzania na kuingiza faida kubwa kwa kiwanda hatimae ajira kuongezeka. Mfano wa nchi zinazoongoza kwa viwanda vinavyotokana na malighafi za ufugaji duniani ni India; ambao wanafuga kondoo aina ya merino wanaotengeneza sufu, USA; ambao wanafuga ng'ombe wengi wa nyama na maziwa.
Kutafta wawekezaji na kuandaa mazingira mazuri kwa wawekezaji watakao wekeza katika viwanda
Mfano; kuwapunguzia gharama za uwekezaji kama kodi ili kuwahamasisha wawekeze kwa wingi na wawe wengi zaidi na kuongeza idadi ya viwanda nchini, ambapo serikali na wakulima watawauzia malighafi kwenye viwanda vyao na bado kutokana na viwanda hivyo watanzania watapata ajira na pesa.
Kwa kutekeleza hayo pato la nchi na mtu mmoja mmoja litaongezeka kwakua ajira zitakuwa nyingi na nchi itatoka kwenye uchumi wa kati daraja la I na kuwa uchumi wa kati daraja la II au kuwa uchumi wa viwango vya juu hatimae maendeleo na kuitwa nchi iliyoendelea.

Upvote
4