Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Habari zenu!
Ofisini kwetu kuna utaratibu wa semina elekezi kwa watumishi wanaanza kazi na wanaotaka kustaafu.
Kwa hii ya wanaoanza kazi iko vizuri maana hata Mimi nimeipata na kuona iko vizuri. Maana inabase kumjenga mtumishi mpya kiuzalendo zaidi na kuijua serikali yake. Imeanza wapi, iko wapi na inaelekea wapi.
Sasa hii ya wastaafu naiona ina kasoro although sijawahi kuhudhuria.
Imejaa vitisho, kuna mstaafu mmoja alinisimulia kuwa huko walikokwenda semina kuna mwanafunzi (mstaafu) mwenzao alizimia baada ya kupigwa masomo makali na waelimishaji. Alipozinduka akaeleza kuwa yeye hajajenga nyumba na hana kitega uchumi cha maana mpaka anastaafu. Utumishi wake wote alikuwa akilipwa mshahara mdogo uliomsaidia kusomesha watoto mpaka chuo kikuu na bado hawajaariwa.
Nimeona wastaafu kama 3 hivi baada ya kustaafu wanaanza kihangaika na kilimo, nilipowahoji kwanini wakimbilie kilimo ambacho hawakuwa wanakifanya tangu zamani wanasema waelimishaji kwenye semina wamewaelekeza pesa wakazitumie kulima na si njia nyingine kama kujenga nyumba za kupangisha na kufungua maduka.
Nijuavyo Mimi kilimo si cha kuingia kichwakichwa, mtu ana milioni 150 unamwambia akalime huku hajawahi kulima hapo possibility ya kuzika pesa ni kubwa sana kuliko anayekwenda kujenga nyumba za kupangisha.
Nimeona pia trend ya wastaafu wanaokuja kuomba mikataba ya muda mfupi imekuwa kubwa sasa. Sasa hizi seminar zinawasaidia nini huku hali za wastaafu zinazidi kuwa mbaya?
Wengine hata nguo mpya wanashindwa kununua bado wana mashati ya zamani. Mwingine nilimsikia akilalamika kuwa mezeshaji wa semina kawaambia wasinunue magari huku wao wamepark magari nje.
Hizi semina zifumuliwe au zifutwe.