Mimi neno langu ni moja tu watumishi mnaoshikilia CCM hamtajenga nyumba kwa ujinga wenu ni hivi katiba hii inampa nafasi ya afisa elimu ,mkurugenzi,Rais na wengine kuwanyonya watumishi kwenye muda wenu,akili zenu ,inakuwaje Rais anastaafu anajengewa nyumba huku wewe polisi ,mwalimu ,mwanajeshi ,nurse,ukilia wakati wa kustaafu wakati wote ni watumishi wa umma(watu) ?Kwa nini rasilimali kubwa wale watawala ?Kwa nini kila mtumishi asipewe pesa yake ajengee hiyo nyumba? Mbona mbunge Kama raia anapewa fedha zake zote?Huyu mtumishi ni raia wa wapi?Pale kigamboni fedha za wastaafu zimeliwa Kwa kununuliwa kiwanja kimoja shs milioni mianane halafu kuna mjinga anasema wakakope yaani mtumishi akatwe miaka 12 humu akila dagaa wanaotoka funza?Sasa kuna Raha gani ya kusoma?Yaani nchi imejaa viongozi wenye Roho za mamba .Watumishi popote ulipo Tanzania pigania katiba mpya maana katiba itajenga taasisi za kusimamia maslahi na mishahara yenu iliyobora na manufaa Kwa vizazi vyenu .