DOKEZO Serikali ifuatilie utendaji Idara ya Ustawi wa Jamii - Hospitali ya Muhimbili, ngazi ya juu hakuna Uwajibikaji

DOKEZO Serikali ifuatilie utendaji Idara ya Ustawi wa Jamii - Hospitali ya Muhimbili, ngazi ya juu hakuna Uwajibikaji

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kwanza nianze kwa kuwapongeza JamiiForums kwa kazi nzuri mnayofanya ya kubadilisha mwenendo wa nchi yetu, kazi kubwa inafanyika na mabadiliko yanaonekana, pongezi kwa hilo.

Hivi karibuni niliona habari ya MOI kuhusu yule mgonjwa ambaye alikosa huduma kutokana na uongozi kumkazia kuhusu suala la fedha, kiukweli suala hilo lilinigus, kwani sio huyo tu tupo wengi tulioteseka na hali hiyo.

Nina Mtoto wa miezi mwili ambaye alikuwa amelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, nilifika hapo bila rufaa kutokana na dharura aliyokuwa nayo mtoto, nikapokelewa na kuingizwa katika mfumo wa IPPM (hii ni huduma ya Madaktari Bingwa kufanya Private Clinic katika Hospitali za Umma), huu ni mfumo ambao unakuwa na gharama kubwa tofauti na Wagonjwa wanaofika hapo kwa rufaa.

Nilienda Ofisi za Ustawi wa Jamii kujieleza na kuomba nibadilishiwe mfumo niwe kwenye mfumo wa kawaida, sikufanikiwa hilo nilizungushwa muda mrefu huku matibabu yakiendelea.

Maafisa wa Idara hiyo wakanipa maelekezo ya nini cha kufuata, nikaandika barua ya kujieleza na kuomba lakini kwa miezi miwili nilikuwa anazungushwa tu huku huduma nyingine zikiendelea kama kawaida kwa gharama ya juu.

Mtoto alifanyiwa upasuaji ambao kwa kawaida gharama yake ni Tsh. Milioni 2.5 lakini tulilazimika kujichanga na kulipia Tsh. Milioni 3.5.

Nikaendelea kuomba kupitia Ustawi wa Jamii tena na tena lakini nikawa nazungushwa tu, wale Maafisa wa chini wakawa hawana sauti ya kusema chochote, wanasema kila kitu kinafanywa na Mkurugenzi wao ambao nimekuwa nikisikia wakimuita kwa jina la Danny.

Sikufanikiwa kupata majibu ya kuhamishwa kwenye mfumo hadi Mtoto alipomaliza huduma na kutakiwa kulipa Tsh. Milioni 8.

Nilikuwa nikienda kwa huyo Mkurugenzi simkuti, siku nikimkuta anakujibu kirahisi tu “Barua yako niliiona muda mrefu”, kisha haifanyii kazi.

Kwenye Mfumo wa IPPM gharama ni kubwa na imenisumbua sana, mfano Dawa ya Antibiotics inayouzwa Tsh. 3,500 kule wanaiuza Tsh. 10,000 au 15,000.

Ilibidi kujichanga na kufikisha kiasi hicho cha fedha kilichohitajika (Tsh. Milioni 8+) ndipo Mtoto akatoka hospitali.

Baada ya kutoka hospitali tulipokuwa tunarejea kwa ajili ya Clinic hali ilikuwa ni ileile bado tupo kwenye Mfumo wa IPPM, safari hii nikalazima kwenda tena kwa Mkurugenzi anayetaka ‘kulambwa miguu’ ndipo akakubali kunihamisha.

Lakini kwa macho yangu nimeshuhudia mambo ya kusikitisha kuhusu utendaji wa Idara hiyo, wale maafisa wa chini hawana sauti kabisa, hata wao kuna muda wanalalamika kwa kuwa wanaonekana hawafanyi kazi, wanalalamikiwa na Wagonjwa na wenye uhitaji kwa kiwango cha juu kwa kuwa maombi ya wenye uhitaji hayajibiwi kwa wakati, ni kama yule jamaa wa MOI aliyeandika hapa JF.

Hivyo, inawezekana Mamlaka za Hospitali kama Muhimbili zinaelekeza Wagonjwa waende Ofisi za Ustawi wa Jamii kuomba msaada wa kupunguziwa gharama za matibabu lakini inashindikana kwa sababu ya Mtu mmoja au watu wachache ambao inawezekana ni ujivuni au wana maslahi yao binafsi.

Serikali iangalie idara hii, nilikuwa pale Jengo la Watoto, Ofisi ya Ustawi wa Jamii, kuna Watu wengi wanalalamika na wanateseka, hawana hela ya matibabu na msaada wa Ustawi ni wa jina tu.
 
Pole kwa changamoto mwananchi mwenzetu.
Ni kweli kitengo Cha ustawi wa jamii hospital Muhimbili ni tatizo saana. Mm nilipitia madhira ya usumbufu na kulipa fedha nyingi hapo hospital na mgonjwa wangu alifarikia. Umepoteza mtoto na fedha unadaaiwa, inaumiza saaana
 
Back
Top Bottom