The Boss
JF-Expert Member
- Aug 18, 2009
- 49,282
- 117,244
Niseme wazi kuwa sikuwahi kuwa fan wa Ben Saanane Kwa lolote lile lakini Kwa sababu alikuwa member mwenzetu hapa nilimuona kama mtu wa karibu au ninaefahamiana nae hivi sababu ya kushiriki pamoja mijadala mbalimbali hapa JF.
Alipoanza kuandikia gazeti la Raia mwema na kuanza kuhoji PHD ya Magufuli binafsi sikuwahi kuwa na interest na huo mjadala. Kwanza niliuona hauna maana sana. Pili niliona hautaweza badilisha lolote Kwa hiyo ni kama anajisumbua.
Ilipoanza kutangazwa kapotea nilistuka sana..binafsi nilifikiri labda kajificha ili apate attention kubwa akiibuka tena. Lakini hadi leo hatuna majibu sahihi hasa nini kilimkuta Ben Saanane.
Alipofariki Magufuli nikahisi labda alikuwa amefungwa rumande kimyakimya na sasa ataachiliwa lakini hadi sasa naona kimya kabisa.
Natamani sasa ukweli ujulikane tuweze funga ukurasa kama yupo hai aachiwe.
Kama alikufa ijulikane alikufaje?
Wahusika kina nani?Mwili upo wapi?
Ilikuwa kusudi au ajali kwenye interogation?
Naaamin familia yake inahitaji kujua ukweli na Sisi wengine tuzungumze kitu kilichothibitishwa.
Nafikiri wakati wa ukweli kujulikana umefika.
Familia na marafiki waombe kumuona Rais asaidie uchunguzi tupate majibu