Serikali ifunge ukurasa wa Ben Saanane ukweli ujulikane

Orodha ya waliopotea ni wengi sana maybe kuna siku watakuja kujitokeza miaka ya huko baadae kama kweli walienda kutafuta maisha kama alivyosema Lugola maybe walikufa au waliuawa hakuna anayejua.

Kinachosikitisha zaidi awamu iliyopita mtu mzima angeweza kupotea tu kama sindano iliyotupwa jalalani na asionekane tena, maybe Roma Mkatoliki anajua mengi zaidi kuhusu kutekwa kwake na wengineo
 
Seconded
 
Nami natamani sana ingekuwa kama hivyo unavyopendekeza.

Lakini...

Mkuu, kwani serikali walishasema chochote kuhusu Ben Saanane?

Hivi polisi walishasema lolote kuhusu kupotea kwa huyu kijana katika mazingira ya ajabu hivi?

Wala hata sijawahi kusikia wazazi wa huyu kijana wakiomba msaada wa serikali juu ya upotevu wake; inawezekana walifanya hivyo bila ya mimi kujua.

Licha ya hayo yote,
Hivi Mo 'issue' yake iliishaje na wale jamaa wa Afrika Kusini? Serikali haihitaji kamwe kulifumbua fumbo hilo?

Na, hivi Tundu Lissu kweli hakupigwa risasi nusra ya kuondoa roho yake?
Hivi serikali haina wajibu juu yake?

Haya ni machache tu kati ya mengi yanayohitaji kutolewa maelezo na serikali na kufanyiwa uchunguzi kamilifu kabisa.

Kudonoa hapa na pale hakutaondoa maumivu yaliyosababishwa na utawala wa kidhalimu.
 
Isiishie tu hapo kwenye kumvua hiyo PhD feki, bali hata Profesa mhusika wa uovu huo naye aondolewe hadhi hiyo ya u-profesa.
 
Mkuu The Boss heshima kwako, ingependeza zaidi katika uzi wako ukaanza na masheikh wa UAMSHO halafu ukamalizia na ben saanane.
 
Ohh!.
 

Mwaka 1984 Aboud Jumbe aliwekwa kizuizini pale Mji Mwema Kigamboni na Mwl Nyerere. Nyerere akafa mwaka 1999 lakini Aboud Jumbe aliendelea kuishi kizuizini mpaka alipofariki mwaka 2017.

Labda pengine kufa kwa Magufuli sio sababu ya kuachiwa kwa Ben endapo kama wanamshikilia.

Pamoja na yote, niungane na wewe, wakati umewadia tuwekwe wazi ni wapi alipo Ben Saanane!!!
 
Halafu the same person akathubutu kufukuza wenye vyeti feki!!
Marehemu Baba Jesca hakuwa tu mtu muovu, hakuwa hata na chembe cha utu. Aliwahi kuwaita watoto wa watu vilaza na kuwatimua vyuoni huku yeye akiwapa vilaza vyeo na kuwafuga wengine nyumbani kwake. Ukweli mchungu ni kwamba huwezi ukapanda mchicha ukavuna nyanya na hakuna namna Baba Jesca angeweza kuzaa kipanga huku yeye ni mtupu kabisa kichwani na cheti feki cha PhD, DNA haikubali!

Kwa sasa wengine tunampa Rais Samia Suluhu Hassan muda wa miezi mitatu kama tulivyompa mwendazake kwa shingo upande. Katika hizo siku 100 tunategemea ataonesha utofauti wake na aliyemtangulia kwa kukitegua kitendawili cha hatma ya Ben Saanane na wengineo. Kwa sasa tupo tunaoendelea kumpa Rais wetu mpya benefit of doubt lakini akae akijua siku hazigandi na kufumba na kufumbua likizo imeisha.
 
Kigogo alishasema kuwa meko ndiye aliyemuua ben saanane
Alimuua kwa mikono yake mwenyewe
Bashite anahusike
 
From my own point of view:

Killing someone, regardless of how brutal could be, is just helping him or her to pay his or her debt of nature as early as possible while waiting for your turn with no one around to help you.
"The best thing in life, is not to have been born, and the next best thing is to die quickly" - Silenus
 
Wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…