Serikali ifute rasmi masomo ya sayansi sekondari

Serikali ifute rasmi masomo ya sayansi sekondari

mhaka

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2013
Posts
489
Reaction score
253
Inasikitisha ninapoona idadi ya waalim wa masomo ya sayansi (chemistry, biology, physics na mathematics) inazidi kupungua kila mwaka. Mfano hai katika wilaya niliyopo walimu waliopngwa/walioajiriwa mwaka huu ni 90, kati ya hao ni walimu 3 tu ndio wa masomo ya sayansi. WIZARA HUSIKA itoe tamko juu ya hali hii
 
na kwa taarifa yako tu huku mtaani yupo mwalimu wa sayansi eti hajapangwa....
 
hapana walimu wapo ila bado hawajiamin na elimuyao ni kwaxabu mixingi mibovu waliyo pitia tangu hawali,ila pia xelikali haiwawezeshi ipaxavyo ndomana walimu wengu tanzania wame amua kujiajili mitaani na xi kwa xerikali hata ao waxeli kalini wanatumia muda mchache xana kufundisha mashuleni muda mwingi hutumia kufundisha mitaani!
 
Ni kweli.....!
 
Sema waongeze walimu wa sayansi sio kufuta masomo. wakifuta masomo madaktari watatoka wapi mkuu?
 
Kulingana na taarifa za kijasusi..walimu wa sayansi wamekua wachache kuliko ata madaktari wetu na sababu kubwa ni maslahi duni na wengi wa waliokua walimu wa sayansi wamejiendeleza kwenye fani za udaktari,uhandisi,sayansi ya kompyuta nk..serikal inapaswa kuliona hil km janga
 
nilishangaa sana kukuta jamaa aliyesoma PCM then ualimu Dip akaacha akasoma sheria,serikali imeacha kutoa motisha kwa walimu wa sayansi wanategemea wataongezeka kama uyoga
 
hapana walimu wapo ila bado hawajiamin na elimuyao ni kwaxabu mixingi mibovu waliyo pitia tangu hawali,ila pia xelikali haiwawezeshi ipaxavyo ndomana walimu wengu tanzania wame amua kujiajili mitaani na xi kwa xerikali hata ao waxeli kalini wanatumia muda mchache xana kufundisha mashuleni muda mwingi hutumia kufundisha mitaani!

sijakuelewa hizo x ndo unamaanisha nini?
 
sijakuelewa hizo x ndo unamaanisha nini?

Hata mie sijamuelewa huyo dogo na x zake ambapo amezijaza bila sababu ya msingi, mfano xerikali sijaona maana na alikuwa anataka kufanya nini.

Pointi huwenda ikawa nzuri lakini uandishi mbaya ukafanya pointi kutosomwa na wengi/kukataliwa.
 
Mambo mengi sana yana interfere kazi ya ualimu na serikali ni kama imeshindwa kukontro.
Mfano; serikali inapochelewa sana kuajiri walimu, inasababisha walimu wengi potential kupotelea kusiko julikana.

Pia, tukiangalia idadi ya wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi ni wachache kweli na hao hao wanatakiwa katika kada mbali mbali zinazo hitaji uelewa wa masomo ya sayansi ( udaktari, uhandisi, statistics, ualimu nk) je waliopo wanatosha?

Ndio walimu wa sayansi ni wachache lakini tujitahidi kuhimiza watoto wetu kusoma masomo ya sayansi ili tupate wanasayansi wengi zaidi.

Pia kuna shule za technical school, zile shule binafsi naziona ndio chemchem ya wanasayansi na mafundi wazuri katika nchi hii, na bahati mbaya shule hizi hivi sasa zimesahaulika na zimelegalega hamna mfano, MIE SHULE HIZI NAZIITA "THE LOST TREASURE"

Jukumu la kuongeza au kupunguza idadi ya wanasayansi ipo mikononi mwetu wenyewe, mie ni mwalimu wa chemistry na biology najitahidi kufanya kazi kadri MUNGU aniwezeshavyo.
 
hapana walimu wapo ila bado hawajiamin na elimuyao ni kwaxabu mixingi mibovu waliyo pitia tangu hawali,ila pia xelikali haiwawezeshi ipaxavyo ndomana walimu wengu tanzania wame amua kujiajili mitaani na xi kwa xerikali hata ao waxeli kalini wanatumia muda mchache xana kufundisha mashuleni muda mwingi hutumia kufundisha mitaani!

Sijaelewa ulicho andika..
 
Back
Top Bottom