Mambo mengi sana yana interfere kazi ya ualimu na serikali ni kama imeshindwa kukontro.
Mfano; serikali inapochelewa sana kuajiri walimu, inasababisha walimu wengi potential kupotelea kusiko julikana.
Pia, tukiangalia idadi ya wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi ni wachache kweli na hao hao wanatakiwa katika kada mbali mbali zinazo hitaji uelewa wa masomo ya sayansi ( udaktari, uhandisi, statistics, ualimu nk) je waliopo wanatosha?
Ndio walimu wa sayansi ni wachache lakini tujitahidi kuhimiza watoto wetu kusoma masomo ya sayansi ili tupate wanasayansi wengi zaidi.
Pia kuna shule za technical school, zile shule binafsi naziona ndio chemchem ya wanasayansi na mafundi wazuri katika nchi hii, na bahati mbaya shule hizi hivi sasa zimesahaulika na zimelegalega hamna mfano, MIE SHULE HIZI NAZIITA "THE LOST TREASURE"
Jukumu la kuongeza au kupunguza idadi ya wanasayansi ipo mikononi mwetu wenyewe, mie ni mwalimu wa chemistry na biology najitahidi kufanya kazi kadri MUNGU aniwezeshavyo.