Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Mnamo tarehe 18 Novemba 2024 nilienda hospitali ya rufaa ya Mloganzila kumtazama shemeji yangu aliyelazwa pale na kichanga wake aliyejifungua kwa oparesheni. Nilipofika getini nilielekezwa na walinzi sehemu ya kusubiria muda wa kuingia kuona wagonjwa. Nikiwa eneo hilo nilipata kusikia mawili matatu ya ndugu na jamaa wenye wagonjwa pale. wengi walikuwa wanalalamikia ukubwa wa gharama na huduma isiyo nzuri ya wahudumu wa pale Mloganzila.
Nilipopata wasaa kuingia wodini nilikuta mgonjwa wetu anaendelea kupambania afya yake lakini mtoto hali yake haikuwa nzuri kabisa. Tuliwauliza wauguzi pale kuhusu maendeleo ya kichanga waligoma kutueleza chochote wakisema mpaka afike baba wa mtoto (kimsingi shemeji alipata ujauzito na mwenye mzigo akalala mbele). Baada ya kunyimwa taarifa za hali ya m toto tukaomba mwenendo wa bill ili tuanze kupunguza. Hapo tulipatiwa bill haraka haraka na nikaketi chini kuchambua gharama kwa items.
Nikashuka chini kushauriana na ndugu juu ya gharama zile, Waliniambia kuwa bili hiyo inayozidi 2M imekuwa mzigo mkubwa kwao hivyo tumeanza kukusanya na kupunguza bili ili siku akitoka asipate kash kash.
Nikiwa hapo nje, nikashuhudia baadhi ya watu waliokuja kutembelea ndugu wakitoka ndani wakiwa na vilio, majonzi na lawama. Nilipouliza kwa watu ambao wanaonekana wametoka mikoani na wagonjwa wao, wengi wameweka kambi pale. wanasema kuwa kwa siku pale Mloganzila wagonjwa wanaoaga dunia kwa kiwango cha chini ni 20 au 25. Watu wanalalamikia majibu yasiyo ya staha kutoka kwa wauguzi, na bill kuwa kubwa mno kiasi kwamba hata wakijaribu kuhoji wananyimwa ushirikiano. Nikikumbuka nilinyimwa taarifa za maendeleo ya mtoto kwa demand ya kipumbavu maana huyo baba wa mtoto hajawahi kukanyaga pale na hata sisi hatumjui kwa sura maana alikimbia ujauzito wa shemeji.
Serikali, hususani serikali ya CCM inapaswa kuingilia kati hii biashara ya afya na uhai wa Watanzania inayoendeshwa kibabe na hospitali zetu za umma. Leo hospitali binafsi zimekuwa kimbilio la watu wengi kwa sababu ya reasonable prices zao ingawa zipo nyingi zinatoza ghali kwa huduma zao. lakini hospitali za umma hususan za RUFAA ni janga kubwa kwa wananchi.
Hivi, hizi kodi tunazolipa zinaishia kulipa madeni ya mikopo ya miundombinu pekee?
Iwapo serikali imekosa muhali kwa afya za Watanzania na kuzigeuza mtaji wake, basi itupishe tuweke chama kitakachowakwamu Watanzania kutoka huu mchezo wa kutoza bill kubwa kwa amtibabu kwenye hospitali zetu za umma.
Taifa lisilojali afya za wananchi wake ni taifa linalojimaliza kwa kansa ya kujitengenezea
Majibu ya Hospitali > Hospitali ya Taifa Muhimbili yatoa ufafanuzi hoja ya Mdau kuhusu "Huduma zake ni janga kwa Wagonjwa"
Soma pia: KERO - Gharama za Kujifungua Hospital ta Taifa Muhimbili MNH (Mloganzila) ni kufuru

- Kitanda cha mama bila gharama za matibabu kwa siku analipia Tzs 100,000/-
- kitanda cha mtoto bila gharama za matibabu kwa siku analipia Tzs 100,000/-
- Gharama zingine halali za tiba na madawa.