Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama hakun hosptali nyingine hii jamani sitotibiwa pale na hakuna nitakaemshauri afikenpale bora ufie hosptali za kata mloganzila ni lango la kifoMnamo tarehe 18 Novemba 2024 nilienda hospitali ya rufaa ya Mloganzila kumtazama shemeji yangu aliyelazwa pale na kichanga wake aliyejifungua kwa oparesheni. Nilipofika getini nilielekezwa na walinzi sehemu ya kusubiria muda wa kuingia kuona wagonjwa. Nikiwa eneo hilo nilipata kusikia mawili matatu ya ndugu na jamaa wenye wagonjwa pale. wengi walikuwa wanalalamikia ukubwa wa gharama na huduma isiyo nzuri ya wahudumu wa pale Mloganzila.
Nilipopata wasaa kuingia wodini nilikuta mgonjwa wetu anaendelea kupambania afya yake lakini mtoto hali yake haikuwa nzuri kabisa. Tuliwauliza wauguzi pale kuhusu maendeleo ya kichanga waligoma kutueleza chochote wakisema mpaka afike baba wa mtoto (kimsingi shemeji alipata ujauzito na mwenye mzigo akalala mbele). Baada ya kunyimwa taarifa za hali ya m toto tukaomba mwenendo wa bill ili tuanze kupunguza. Hapo tulipatiwa bill haraka haraka na nikaketi chini kuchambua gharama kwa items.
Sasa piga hesabu mama amekaa hapo siku tisa huku siku nne akiwa ICU. Na bado mpaka leo yupo wodini.
- Kitanda cha mama bila gharama za matibabu kwa siku analipia Tzs 100,000/-
- kitanda cha mtoto bila gharama za matibabu kwa siku analipia Tzs 100,000/-
- Gharama zingine halali za tiba na madawa.
Nikashuka chini kushauriana na ndugu juu ya gharama zile, Waliniambia kuwa bili hiyo inayozidi 2M imekuwa mzigo mkubwa kwao hivyo tumeanza kukusanya na kupunguza bili ili siku akitoka asipate kash kash.
Nikiwa hapo nje, nikashuhudia baadhi ya watu waliokuja kutembelea ndugu wakitoka ndani wakiwa na vilio, majonzi na lawama. Nilipouliza kwa watu ambao wanaonekana wametoka mikoani na wagonjwa wao, wengi wameweka kambi pale. wanasema kuwa kwa siku pale Mloganzila wagonjwa wanaoaga dunia kwa kiwango cha chini ni 20 au 25. Watu wanalalamikia majibu yasiyo ya staha kutoka kwa wauguzi, na bill kuwa kubwa mno kiasi kwamba hata wakijaribu kuhoji wananyimwa ushirikiano. Nikikumbuka nilinyimwa taarifa za maendeleo ya mtoto kwa demand ya kipumbavu maana huyo baba wa mtoto hajawahi kukanyaga pale na hata sisi hatumjui kwa sura maana alikimbia ujauzito wa shemeji.
Serikali, hususani serikali ya CCM inapaswa kuingilia kati hii biashara ya afya na uhai wa Watanzania inayoendeshwa kibabe na hospitali zetu za umma. Leo hospitali binafsi zimekuwa kimbilio la watu wengi kwa sababu ya reasonable prices zao ingawa zipo nyingi zinatoza ghali kwa huduma zao. lakini hospitali za umma hususan za RUFAA ni janga kubwa kwa wananchi.
Hivi, hizi kodi tunazolipa zinaishia kulipa madeni ya mikopo ya miundombinu pekee?
Iwapo serikali imekosa muhali kwa afya za Watanzania na kuzigeuza mtaji wake, basi itupishe tuweke chama kitakachowakwamu Watanzania kutoka huu mchezo wa kutoza bill kubwa kwa amtibabu kwenye hospitali zetu za umma.
Taifa lisilojali afya za wananchi wake ni taifa linalojimaliza kwa kansa ya kujitengenezea
Soma pia: KERO - Gharama za Kujifungua Hospital ta Taifa Muhimbili MNH (Mloganzila) ni kufuru
Hivi nawaambiaga Baadhi ya ndugu zangu. Suala la afya Tanzania chini ya utawala wa CCM ni biashara kubwa sana. Wanaosikia wanasikiaKama Huna Bima ya kueleweka Na maisha ya chini , Ki ufupi ni kuwa TUNZA AFYA YAKO SANA . Itokee bahati mbaya kufika hospitali na sio kwasababu ya uzembe wa kutunza Afya
Nje na hapo Kwa Hospitali zenu Ni kwa Bahati kwenda na kurudi salama
Ukiona umepewa transfer kutoka muhimbili kwenda Mloganzila ujue uwezekano wa kufa ni zaidi ya 60%Mtu kupata rufaa kutoka Muhimbili -Upanga hadi Mlonganzila ni kwamba hizo hospital zina level mbili tofauti?
Ni kweli, tuliguza pale Kila siku tulikuwa tunalipa 200,000/- na huduma zao zinasuasua.Mkuu
Kama upo Tanzania, fanya kutembelea hospitali ile kuna mengi sijaweza kuyaandika, yanaumiza sana masikio.
Madaktari wengi pale ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili. Pata picha kinachoendelea hapo, yaani hata watu hawajahitimu ethics za utabibu wanapewa dhamana ya kusimamia matibabu ya watu as mabingwa.
Serikali inatuweka rehani sana
90% kabisaaa.Ukiona umepewa transfer kutoka muhimbili kwenda Mloganzila ujue uwezekano wa kufa ni zaidi ya 60%
Wanafunzi wa Muhimbili wale.Ni kweli, tuliguza pale Kila siku tulikuwa tunalipa 200,000/- na huduma zao zinasuasua.
Wamejaa vidaktari vidogovidogi tu
Hospitali ya kuweka Maputo tumboni na kuongeza makalioMnamo tarehe 18 Novemba 2024 nilienda hospitali ya rufaa ya Mloganzila kumtazama shemeji yangu aliyelazwa pale na kichanga wake aliyejifungua kwa oparesheni. Nilipofika getini nilielekezwa na walinzi sehemu ya kusubiria muda wa kuingia kuona wagonjwa. Nikiwa eneo hilo nilipata kusikia mawili matatu ya ndugu na jamaa wenye wagonjwa pale. wengi walikuwa wanalalamikia ukubwa wa gharama na huduma isiyo nzuri ya wahudumu wa pale Mloganzila.