Serikali iingilie kati bei za mayai

20162016

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2011
Posts
206
Reaction score
96
Biashara ya ufugaji wa kuku mayai ipo katika hali mbaya sana. Bei za mayai ya kisasa zimeshuka kiasi kwamba wafugaji wanashindwa kulipia vyakula vya kulisha kuku wao.

Taarifa ambazo hazijathibitishwa ila zinasemwa mitaani ni kuna mayai kutoka malawi na zambia yanaingia kinyume na utaratibu.

Kwa mlio karibu na waziri wa mifugo na viongozi wengine wa serikali tunaomba hili lifikishwe kwa uharaka ili hatua zichukuliwe.

Asanteni
 
Mkuu supply na demand ndo zinaamua bei ya bidhaa sokoni kwahiyo tulia watu wale mayai

Katika biashara kuna kitu kinaitwa opportunities na compititive advantage.
 
Mlipokuwa mnaruhusu vifaranga viuzwe malawi mlitegemea nini?
.Maana maelfu ya vifaranga yalikuwa yanaenda huko, mbona hakupiga kelele?
Pili wanazalisha huko ni watanzania wenzetu kwa nini mnataka wao wasinufaike na soko la kwao?
 
Fugeni wa kienyeji trey 15000 na hayapatikani sana
 
Mambo ya kibiashara hayo, ukiona hupati faida kama zamani achana nayo au tafuta soko jipya.

Kukontroo bei hilo haliwezekani.

Wewe sio domination system kama monopoly😁
 
Huu ni uchawi sasa...wanangu wa Goba pale Goba senta ukitokea makongo unaoaribishwa na mayai trei elfu saba 🔥🔥
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…