Serikali iingilie kati haraka huu uharibifu wa akili unafanywa na Simba na Yanga; wakuu wa shule wameshaingiliwa nao

Serikali iingilie kati haraka huu uharibifu wa akili unafanywa na Simba na Yanga; wakuu wa shule wameshaingiliwa nao

Dr wa Manesi

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2024
Posts
997
Reaction score
1,220
Wanagroup huko linaitwa HMS TANZANIA. Huko tayari limejaa ujinga ujinga mtupu wa habari za Simba na Yanga. Lengo la group kujadili taaluma halipo tena.....muda wote ni mpira tu wa Simba na Yanga Huku Kila upande ukijitahidi kuwa muongo kwa Kadiri ya uwezo wake Ili tu kujifurahisha.

Leo tena limefika suala hili la kughairishwa kwa mechi na tangu asubuhi huko ni habari hizo tu. Hoja hakuna Bali ni ujinga mtupu wa kutetea ujinga. Hii hapa chini ni hoja ya mkuu mmoja huko Iringa (jina limehifadhiwa) akitetea 'sunna' iliyofanywa na Simba ya kukimbia:

"Hivi ni Mwaka Jana au Mwaka Juzi Yanga nao waligoma kwa Sababu ya kubadilisha muda wa mchezo.? Malipo Huwa ni hapa Hapa duniani....UBAYA UBWELAAAAAAA"

Jamani, taifa liko salama kweli kwa Hali hii?!!! Serikali ifanye kitu, tunapotea.

Mlale unono.
 
HMS Tanzania ni kundi la watu vilaza kuwahi kutokea duniani. Hivi nyie si ndiyo mlichukua sijui mlichangia fomu ya u-rais.

Nyie endeleeni kulinda vyeo tu ila suala la kuinua taaluma sio sehemu ya majukumu yenu.

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom