A
Anonymous
Guest
Mimi ni mkulima, na ninaomba kufikisha kilio chetu kuhusu kupanda kwa bei ya mbolea, hasa Urea na NPK. Kwa sasa hali imekuwa ngumu sana kwa wakulima kwa sababu hakuna bei inayofanana wala kufuatwa kama tunavyoelekezwa na serikali.
Kwa mfano, Bariadi mbolea hizi zinauzwa hadi shilingi 160,000 kwa mfuko mmoja. Kuna mawakala wanaouza kwa bei kubwa sana, na mmoja wao anatajwa kuwa msambazaji mkubwa anayetoza bei inayozidi mara nyingi zaidi ya ile inayotangazwa na serikali.
Kinachotuuma zaidi ni kuona serikali ikiwa kimya wakati wakulima tunateseka. Tunajiuliza, je, kweli mamlaka hazina taarifa kuhusu hali hii? Mbolea haipatikani kirahisi, na kila wakala anaweka bei yake mwenyewe.
Tatizo hili linaonekana zaidi katika mikoa ya Arusha, Mara na Mwanza, ambako bei zimepanda sana.
Kwa maelezo tunayopata, bei ya serikali inatajwa kuwa karibu shilingi 75,000 kwa mfuko, lakini ukienda sokoni unakuta maduka ya eneo moja yanauza kwa bei tofauti kabisa. Duka moja linaweza kuuza kwa laki moja na elfu ishirini, jingine laki moja na nusu.
Hata Kahama kwa sasa mbolea inauzwa karibu shilingi 120,000, na bado mkulima anabeba gharama za usafiri.
Wakala wengi hawataki tena kuuza kwa bei ya ruzuku; wanadai mbolea za ruzuku zimeisha, lakini ukiwa tayari kununua kwa bei ya juu wanakupatia. Wengine wanasema serikali imekataa kupandisha bei rasmi, hivyo wao wameamua kuuza kwa bei wanazotaka.
Sisi wakulima tunaomba serikali iingilie kati haraka, ifuatilie mawakala wanaopandisha bei kiholela, ihakikishe mbolea zinapatikana kwa urahisi, na bei elekezi za serikali zinatekelezwa kwa vitendo. Bila kufanya hivyo, gharama za uzalishaji zinaendelea kupanda na mkulima mdogo ndiye anayeumia zaidi.
Pia soma ~ TFRA: Tumekamata Wafanyabiashara kwa kuuza mbolea kinyume na maelekezo ya Serikali