ministrant
JF-Expert Member
- Jan 17, 2014
- 754
- 1,478
Nimekuwa nikifuatilia mahojiano kadhaa yanayofanywa na viongozi mbalimbali wa taasisi za Serikali na Wana habari, ila kilichonisikitisha ni kuona mwanahabari anahoji swali ambalo hata uelewa wa hilo jambo hana kiasi kwamba swali likirudishwa kwake kwa ufafanuzi zaidi anabaki kumbwelambwela tu.
Mathalani, mwandishi anamuuliza kiongozi wa Serikali kuwa sheria ya kodi inamtaka ofisa wa forodha anapotekeleza majukumu yake lazima aambatane na ofisa wa Polisi, mwandishi huyo anapoulizwa ni kifungu kipi cha sheria ya kodi kinachoamuru iwe hivyo katika utekelezaji wa majukumu ya ofisa wa forodha kulazimika kuambatana na ofisa wa Polisi anabaki kukosa majibu kwakuwa kichwani hana authority inayotamka hivyo.
Mwanahabari mwingine anasema ndugu walisema mara ya mwisho simu ya ndugu yao ilisoma yuko maeneo ya Chang'ombe Polisi, mwanahabari huyo anapotakiwa aeleze kwa kina kuwa competent authority zenye access na kusoma location ni vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), je, hizo taarifa walizipatia wapi kuwa location ilisoma maeneo hayo? Mwanahabari anakosa cha kueleza.
Binafsi naona wanahabari wengi wamekuwa wakijikita kuhoji maswali ambayo huwa vyanzo vyao ni kutoka kwa whistle blower wa mitandaoni ambapo sio jambo baya, lakini wanakosa weledi wa kuchanganya na zao kwa kwenda deep juu ya kile ambacho kimekuwa kimechapishwa huko mtandaoni,badala yake wao huingia kichwakichwa na kuishia kupigwa za uso kwenye press.
Nadhani haya ni matokeo ya taaluma hii kuvamiwa na vilaza ambao huishia kufanya table investigation na kwenda kwenye press kichwa kichwa.
Wanapaswa kutambua kuwa wakati mwingine hizi taarifa za mitandaoni huwa zinachapishwa kwa watu wenye mrengo fulani kwa maslahi fulani na wao kwa kuwa hawajitambui hujikuta wanaingia kwenye mtego kwa kutozingatia weledi wa taaluma zao na kujikita kuamini umbea bila kuwa na competent information.