Serikali iingilie kati Makanisa ya Miujiza? Watanzania masikini wa kutupwa wanakamuliwa mamilioni kwa utapeli huku wahubiri wakigeuka mamilionea

broo hujaeleweka apo em, rejea ulichoandika (Watanzania masikini wa kutupwa, wanakamuliwa mamilioni kwa utapeli)
 
umesema ni matajiri tu ndo wanaofanikiwa kumuona pastor au sio! afu maskini anawezaje kutozwa mamilioni ya pesa
 
PM
Hii mada ni impossible kwa sababu serikali haina udhibiti wa hiari za watu.
 
Umenena! Big up!! Kuna kabila fulani wameuza ng'ombe zao, wapo haoa Kawe wanasubiri miujiza. Kuna mwenye kidonda cha kisukari nae anasubiri miugiza. Naomba tu serikali iingilie kwani watu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Ningeomba katika swala la imani tusiweke akili pembeni."faith and reason " better you understand in order to believe.
 
Hili la miujiza maskini wa kutupwa wataendelea kukamliwa hadi mwisho wa dunia. Kuna Mkatoliki mmoja alikuwa akiniambia baada ya misa parokiani kwao Jumapili ukiona mabasi yanayokuja kuwachukua waumini kuwapeleka kwenda kusali kwenye makanisa mengine "ya miujiza" utashangaa. Mimi huwa najiuliza hivi (ingawa sikatai kuombewa), kama Mungu anaweza kumskiliza X na Y wanaoombea, kwa nini hata siku moja asinionee huruma na kunisikiliza mimi ninayeomba kwa shida zangu na pia kuwaombea wengine? Pili, huwa najiuliza hivi: kwa nini Mungu anataka hadi mwombeaji apoteze sauti kwa kutaja "Kwa Jina la Yesu" na asinisikilize mimi ninayeomba nikiwa sober hata bila kupoteza sauti kwa sababu ya kupayukapayuka? Naheshimu imani za watu wengine na naamini kuna njia nyingi za kumwomba Mungu, lakini hili la kupayukapayuka na kusali kama wendawazimu (kuongea lugha isiyoeleweka) huwa nina mashaka nalo kabisa. Sidhani kama Mungu anahitaji yote haya.
 
Basi hata upatu uachwe tu uendelee maana nayo ni imani. Unaaminishwa ukiwekeza sh laki moja baada ya mwezi utavuna laki tatu. Mbona hao wa upatu wanachukuliwa hatua? Kwani imani ni mpaka iwe na neno Mungu?
 
Ni ujinga tu. Wewe kama unahitaji kitu kutoka kwa mzazi wako eti mpaka upitie kwa ndugu yako au jirani yako akakuombee. Huo siyo ukristo ni ushirikina na ushetani tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…