Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
PMWanabodi
Kama kawa kila nipatapo fursa huja na makala zangu elimishi za kwa maslahi ya taifa. Topic ya leo, ni kutoa wito kwa Serikali yetu kuingilia kati kitu kinachoendelea kwenye baadhi ya makanisa ya wakovu yanayojinasibu kufanya miujiza, kutoa mapepo, kutoa uchawi na kufanya miujiza ya uponyaji?.
Baadhi ya wahubiri hawa wanatumia nguvu za giza za kiini macho kwa kitu kinachoitwa auto suggestion kwa Watanzania Masikini wa Kutupwa, kuaminishwa umasikini wao ni kwasababu wamelogwa, hivyo ili kuuondoa uchawi wa umasikini, unatakiwa kufanya appointment kumuona Mtumishi, ambapo utapangiwa kiwango cha fedha kumuona mtumishi.
Kwenye matangazo yao kupitia redio na TV, unaambiwa njoo na sadaka yako bila kuambiwa kiwango. Ukifika kanisani,
utaandikishwa na kuambiwa kiwango cha kumuona mtumishi akueleze jinsi ulivyologwa na ni nani amekuloga. Kiwango kilianzia 10,000, baadae ikawa 20,000, ikapanda kuwa 50,000, 100,000 sasa ni 200,000.
Unatakiwa kuitafuta hiyo pesa popote ulipe ndipo umuone mtumishi. Hivyo ni waumini wenye pesa tuu ndio watamuona mtumishi!.
Baada ya kuingia kumuona, mtumishi atakuambia prophesy yako na ku conclude matatizo yako yote, ya kiuchumi, umasikini, maradhi, au majanga yoyote, ni umelongwa na watu wa jijijini kwako!.
Baada ya hapo sasa ndio utapewa bili ya sadaka. Mtumishi atajifanya anamuuliza Mungu, then unaambiwa Mungu amesema njoo na sadaka ya milioni 2, 5, 10, 20, kutegemea na ukubwa wa tatizo lako, ya kuleta hiyo sadaka ndipo Mungu atalimaliza tatizo lako!.
Kutokana na wewe kuwa ni tayari umesha pigwa ganzi, utakwenda kuzitafuta hizo pesa na kuzileta cash!.
Watanzania masikini wa kutupwa, wanakamuliwa mamilioni kwa utapeli, na baadhi ya hawa ma Pastor, huku hao ma Pastor na wahubiri wakineemeka na kuageuka mamilionea na mabilionea huku wakivuta mi ndinga ya nguvu!.
Kuna Mama mmoja alifiwa na mtoto wake, the only son, amedanganywa mtoto wake hajafa, amechukuliwa tuu kichawi, mama kaambiwa akatafute sadaka kiasi fulani, arejeshewe mwanae!, huyo mama ana haha kusaka hiyo pesa ili kumrejesha mwanae!.
Japo haya ni mambo ya imani, na waumini wanakwenda wenyewe kwa hiyari yao na wana toa fedha kwa ridhaa zao, na serikali yetu imetoa uhuru wa kuabudu, lakini ikifikia kiwango Watanzania wanatapeliwa, serikali ina wajibu wa kuingilia kati wananchi wake wasiendelee kutapeliwa!.
Namalizia kwa ile hoja ya msingi jee kuna haja ya serikali iingilie kati shughuli za haya makanisa ya wakovu ya miujiza ili Watanzania masikini wa kutupwa, wasiendelee kukamuliwa mamilioni kwa utapeli, huku wahubiri wakizidi kunona kwa kuwa mamilionea!.
Naomba kuwasilisha.
Paskali
Update
Mkuu Mywangu, usimwingize Mtumishi kweli wa Mungu, Kuhani Mussa, kumuona Kuhani Musa ni bure ila unaweza kuleta sadaka yako yoyote.
Kazi ya ujenzi wa Ngome ya Yesu pale Kimara Temboni, inafanyika kupitia kadi zinaitwa Partnership, hupangiwi kiwango, unajifanyia personal assessment ndipo unajaza!.
Watumishi matapeli kumuona ni lazima utoe 200,000, kuna watu walikuwa na 100,000 walitoa na zikapokelewa, watu wa 200,000 walipoongezeka, wale wa 100,000 walirudishiwa fedha zao, wakaambiwa wakadundulize mpaka zitimie 200,000 ndipo warudi.
Ukimuona Kuhani Mussa anakuombea na kukupatia vifaa vya kiroho bure extra utalipia lakini kuwaona matapeli hawa, unatakiwa kwenda kuleta kwanza sadaka, with the amount, from 6 figures ndipo uombewe!.
P
Eti kweli, nani kawafanya masikini serikali au Makanisa hayo?broo hujaeleweka apo em, rejea ulichoandika (Watanzania masikini wa kutupwa, wanakamuliwa mamilioni kwa utapeli)
Unatapa tapa hujui unaandika kwa mada ipi. Kuwahusu masheikh washtakiwa Arusha tusome huku kujiridhisha:
Napinga masheikh sita wa Kiislamu kupewa adhabu ya kunyongwa hadi kufa
Narudia rudia kusoma nacheka sana Arusha: Masheikh 6 wahukumiwa kunyongwa hadi kifo
Hoja kujibiwa kwa hoja unajua maana yake?
Hili la miujiza maskini wa kutupwa wataendelea kukamliwa hadi mwisho wa dunia. Kuna Mkatoliki mmoja alikuwa akiniambia baada ya misa parokiani kwao Jumapili ukiona mabasi yanayokuja kuwachukua waumini kuwapeleka kwenda kusali kwenye makanisa mengine "ya miujiza" utashangaa. Mimi huwa najiuliza hivi (ingawa sikatai kuombewa), kama Mungu anaweza kumskiliza X na Y wanaoombea, kwa nini hata siku moja asinionee huruma na kunisikiliza mimi ninayeomba kwa shida zangu na pia kuwaombea wengine? Pili, huwa najiuliza hivi: kwa nini Mungu anataka hadi mwombeaji apoteze sauti kwa kutaja "Kwa Jina la Yesu" na asinisikilize mimi ninayeomba nikiwa sober hata bila kupoteza sauti kwa sababu ya kupayukapayuka? Naheshimu imani za watu wengine na naamini kuna njia nyingi za kumwomba Mungu, lakini hili la kupayukapayuka na kusali kama wendawazimu (kuongea lugha isiyoeleweka) huwa nina mashaka nalo kabisa. Sidhani kama Mungu anahitaji yote haya.Wanabodi
Kama kawa kila nipatapo fursa huja na makala zangu elimishi za kwa maslahi ya taifa. Topic ya leo, ni kutoa wito kwa Serikali yetu kuingilia kati kitu kinachoendelea kwenye baadhi ya makanisa ya wakovu yanayojinasibu kufanya miujiza, kutoa mapepo, kutoa uchawi na kufanya miujiza ya uponyaji?.
Baadhi ya wahubiri hawa wanatumia nguvu za giza za kiini macho kwa kitu kinachoitwa auto suggestion kwa Watanzania Masikini wa Kutupwa, kuaminishwa umasikini wao ni kwasababu wamelogwa, hivyo ili kuuondoa uchawi wa umasikini, unatakiwa kufanya appointment kumuona Mtumishi, ambapo utapangiwa kiwango cha fedha kumuona mtumishi.
Kwenye matangazo yao kupitia redio na TV, unaambiwa njoo na sadaka yako bila kuambiwa kiwango. Ukifika kanisani,
utaandikishwa na kuambiwa kiwango cha kumuona mtumishi akueleze jinsi ulivyologwa na ni nani amekuloga. Kiwango kilianzia 10,000, baadae ikawa 20,000, ikapanda kuwa 50,000, 100,000 sasa ni 200,000.
Unatakiwa kuitafuta hiyo pesa popote ulipe ndipo umuone mtumishi. Hivyo ni waumini wenye pesa tuu ndio watamuona mtumishi!.
Baada ya kuingia kumuona, mtumishi atakuambia prophesy yako na ku conclude matatizo yako yote, ya kiuchumi, umasikini, maradhi, au majanga yoyote, ni umelongwa na watu wa jijijini kwako!.
Baada ya hapo sasa ndio utapewa bili ya sadaka. Mtumishi atajifanya anamuuliza Mungu, then unaambiwa Mungu amesema njoo na sadaka ya milioni 2, 5, 10, 20, kutegemea na ukubwa wa tatizo lako, ya kuleta hiyo sadaka ndipo Mungu atalimaliza tatizo lako!.
Kutokana na wewe kuwa ni tayari umesha pigwa ganzi, utakwenda kuzitafuta hizo pesa na kuzileta cash!.
Watanzania masikini wa kutupwa, wanakamuliwa mamilioni kwa utapeli, na baadhi ya hawa ma Pastor, huku hao ma Pastor na wahubiri wakineemeka na kuageuka mamilionea na mabilionea huku wakivuta mi ndinga ya nguvu!.
Kuna Mama mmoja alifiwa na mtoto wake, the only son, amedanganywa mtoto wake hajafa, amechukuliwa tuu kichawi, mama kaambiwa akatafute sadaka kiasi fulani, arejeshewe mwanae!, huyo mama ana haha kusaka hiyo pesa ili kumrejesha mwanae!.
Japo haya ni mambo ya imani, na waumini wanakwenda wenyewe kwa hiyari yao na wana toa fedha kwa ridhaa zao, na serikali yetu imetoa uhuru wa kuabudu, lakini ikifikia kiwango Watanzania wanatapeliwa, serikali ina wajibu wa kuingilia kati wananchi wake wasiendelee kutapeliwa!.
Namalizia kwa ile hoja ya msingi jee kuna haja ya serikali iingilie kati shughuli za haya makanisa ya wakovu ya miujiza ili Watanzania masikini wa kutupwa, wasiendelee kukamuliwa mamilioni kwa utapeli, huku wahubiri wakizidi kunona kwa kuwa mamilionea!.
Naomba kuwasilisha.
Paskali
Update
Mkuu Mywangu, usimwingize Mtumishi kweli wa Mungu, Kuhani Mussa, kumuona Kuhani Musa ni bure ila unaweza kuleta sadaka yako yoyote.
Kazi ya ujenzi wa Ngome ya Yesu pale Kimara Temboni, inafanyika kupitia kadi zinaitwa Partnership, hupangiwi kiwango, unajifanyia personal assessment ndipo unajaza!.
Watumishi matapeli kumuona ni lazima utoe 200,000, kuna watu walikuwa na 100,000 walitoa na zikapokelewa, watu wa 200,000 walipoongezeka, wale wa 100,000 walirudishiwa fedha zao, wakaambiwa wakadundulize mpaka zitimie 200,000 ndipo warudi.
Ukimuona Kuhani Mussa anakuombea na kukupatia vifaa vya kiroho bure extra utalipia lakini kuwaona matapeli hawa, unatakiwa kwenda kuleta kwanza sadaka, with the amount, from 6 figures ndipo uombewe!.
P
Aisee nimeifurahia comment yako! Yaani binadamu anakuwa na akili ndogo kuliko ya mnyama😆When it comes to belief, i.e. religious beliefs, human beings prove to be the most stupid creatures on this planet.
Basi hata upatu uachwe tu uendelee maana nayo ni imani. Unaaminishwa ukiwekeza sh laki moja baada ya mwezi utavuna laki tatu. Mbona hao wa upatu wanachukuliwa hatua? Kwani imani ni mpaka iwe na neno Mungu?Serikali haina mamlaka kuwapangia wananchi nini cha kuamini na nini cha kutoamini kitendo hicho cha serikali kuingilia uhuru wa kiimani wa jamii fulani ni kinyume na matakwa ya katiba ya JMT.
Ukiruhusu serikali iingilie na kupangia taratibu imani fulani tambua fika na imani yako umeikabidhi mikononi mwa serikali anaweza tokea kiongozi akaona imani yako ni ya kishenzi na akamua lolote atakalo juu ya imani yako na usiwe na nguvu ya kikatiba kupinga hilo.
Tanzania kila mtu yupo huru kiimani kwa kuzingatia katiba ya JMT tuheshimu hilo.
Ni ujinga tu. Wewe kama unahitaji kitu kutoka kwa mzazi wako eti mpaka upitie kwa ndugu yako au jirani yako akakuombee. Huo siyo ukristo ni ushirikina na ushetani tu.Hili la miujiza maskini wa kutupwa wataendelea kukamliwa hadi mwisho wa dunia. Kuna Mkatoliki mmoja alikuwa akiniambia baada ya misa parokiani kwao Jumapili ukiona mabasi yanayokuja kuwachukua waumini kuwapeleka kwenda kusali kwenye makanisa mengine "ya miujiza" utashangaa. Mimi huwa najiuliza hivi (ingawa sikatai kuombewa), kama Mungu anaweza kumskiliza X na Y wanaoombea, kwa nini hata siku moja asinionee huruma na kunisikiliza mimi ninayeomba kwa shida zangu na pia kuwaombea wengine? Pili, huwa najiuliza hivi: kwa nini Mungu anataka hadi mwombeaji apoteze sauti kwa kutaja "Kwa Jina la Yesu" na asinisikilize mimi ninayeomba nikiwa sober hata bila kupoteza sauti kwa sababu ya kupayukapayuka? Naheshimu imani za watu wengine na naamini kuna njia nyingi za kumwomba Mungu, lakini hili la kupayukapayuka na kusali kama wendawazimu (kuongea lugha isiyoeleweka) huwa nina mashaka nalo kabisa. Sidhani kama Mungu anahitaji yote haya.