Serikali iingilie kati Makanisa ya Miujiza? Watanzania masikini wa kutupwa wanakamuliwa mamilioni kwa utapeli huku wahubiri wakigeuka mamilionea


Serikali ina kazi moja tu na ni ndogo sana. Waige alichofanya Kagame na wala kuiga mazuri sio kosa. Sheria itungwe, mtu asiruhusiwe kufungua kanisa mpaka awe na degree ya theology.

Baada ya hapo watakaokubali kutapeliwa waendelee.
Kwani mwenye degree ya theology hawezi kuwa mpigaji?

Si ndiyo atakupiga ki degree degree ya theology hapo?
 
Inasikitisha sn ndo kwanza viongozi wakubwa wasaka madaraka wanachangia ujenzi wa makanisa hayo.

Yani watanzania wanaishi kwa kubahatisha sana
 
Kwani Kuna mtu huwa anawachapa fimbo ili waende Makanisani kwa lazima???

Watu wanajipeleka wenyewe kuibiwa, wewe unaumia utadhani huwa wanatoa pesa zako.

Acha wajanja akina Lusekelo waendesha ndinga za maana.
 
Serikali haiwezi kuingilia uhuru wa kuabudu. Acha waendelee kupigwa maana ni wabishi sana
Umeiweka kifupi na kibabe lakini ukweli ndio huu.

Unaweza kumdaka mchungaji kama kafanya kosa la jinai, mfano akifanya kosa la money laundering kuchukua pesa chafu na kuzipitisha kanisani makusudi huku akijua hizi pesa chafu, halafu kuwarudishia wahalifu zimetakasishwa kanisani kwenye akaunti za kanisa, ukathibitisha knowledge na intent, hapo unaserereka naye. Na hata hiyo si kesi rahisi, ni kesi complex.

Ila, haya mambo ya kuwapiga watu pesa za sadaka, tena kuzitumia kujenga kanisa, kununua magari ya mchungaji, ku support lifestyle ya mchungaji, hapo ni vigumu sana kumshitaki huyo mchungaji, kwa sababu kimsingi hakuna sheria inayovunjwa. Watu wanatoa hela zao wenyewe bila kulazimishwa, katika jambo complex sana la imani ambalo limepewa kinga kikatiba. Yani kuna kinga ya kikatiba ya mtu mjinga kutoa hela yake na kuliwa na mchungaji wake.

Hapo kitu cha kufanya ni kuongeza elimu kwa watu wayastukie haya makanisa na kujiongeza wenyewe.

Na hii ni kazi yetu sote, si kazi ya serikali tu.

Marufuku za serikali haziwezi kumaliza tatizo hili. Ukipiga marufuku ndiyo kwanza watu wanaenda underground.

Ukristo una uzoefu mkubwa sana wa kukua huku ukipigwa vita na serikali, tangu enzi za utawala wa Warumi.

Ukisoma hata vitabu vya Mtume wa Wakristo Paul, utaona jinsi Wakristo walivyokuwa wanafanyiwa figisu na serikali, na Paul alivyokuwa anawapa moyo wapambanie imani yao.

Serikali ikitunga sheria kuwabana hawa wachungaji, ndiyo kwanza wataenda underground na kuwapa waumini wao aya zinazosema kuwa siku za mwisho atakuwepo mpinga Kristo atakayekuja kulisakama kanisa, watasema serikali ndiye huyo mpinga Kristo. Matokeo yake watapata huruma zaidi kutoka kwa waumini wao ambao watakubali kuwa serikali ni mpinga Kristo aliyetabiriwa kwenye Biblia.

Marufuku ya serikali itawaongezea kiki hawa wachungaji.

Hapa hakuna njia ya kuepuka kuongeza level ya elimu kwa watu wote, na kujenga utamaduni wa kukataa hizi habari za miujuza.

Ndiyo maana kila siku nasisitiza sana watu wajikite kwenye mambo ya uthibitisho, kuachana na habari za kuamini amini mambo tu.
 
Kwani Kuna mtu huwa anawachapa fimbo ili waende Makanisani kwa lazima???

Watu wanajipeleka wenyewe kuibiwa, wewe unaumia utadhani huwa wanatoa pesa zako.

Acha wajanja akina Lusekelo waendesha ndinga za maana.
Ni uhalifu kama uhalifu wa upatu unapaswa kukemewa na kushughulikiwa. Kwa hiyo tapeli akimtaja Mungu basi asichukuliwe hatua? Basi sasa matapeli wote wamepata njia isiyo na usumbufu ya kutapeli kwa raha zao!
 
Ni ujinga tu. Wewe kama unahitaji kitu kutoka kwa mzazi wako eti mpaka upitie kwa ndugu yako au jirani yako akakuombee. Huo siyo ukristo ni ushirikina na ushetani tu.
Of course, kuomba kwa kupitia mtu mwingine ni jambo la kawaida. Kuna baadhi ya familia mtoto anaomba kitu fulani kwa baba yake kupitia mama yake au mtu ambaye baba yake anapenda kumsikiliza. Kuna pia kuomba msamaha kupitia mtu au watu wengine au kuomba kazi kwa bosi kupitia rafiki yake etc. Haya mambo huwa yapo.
 
Well said kaka
 
..,Ndio maana Tapeli ' Kiboko ya Wachawi' aliwaingiza Wengi Mkenge!!!....na badohawakomi. 'Watu wangu wanaamhamia Kwa Kukosa Maarifa' !....Kweli.
 
Respect my comrade! Ila bado tuna safari ndefu sana. Sijui kama kizazi chetu hiki tunaweza kukibadilisha kifikra . Tumejitahidi mno kutoa elimu sijui labda wapo wachache waliobadilika na kuachana na huu upumbavu wa miujiza ambao hata huyo Yesu wanayemwamini alikemea vikali tabia hiyo na kuifananisha na UZINZI.
 
Ni sawa kabisa hata biblia inasema tuombeane lakini sasa imegeuka kuwa ndiyo excuse ya mtu kuacha jitihada za kujiweka karibu na Mungu wake na kutumainia mwanadamu mwingine amuombee. Hii ni ibada ya sanamu na chukizo mbele za Mungu
 
..,Ndio maana Tapeli ' Kiboko ya Wachawi' aliwaingiza Wengi Mkenge!!!....na badohawakomi. 'Watu wangu wanaamhamia Kwa Kukosa Maarifa' !....Kweli.
Na kuna wengine wapo tena hewani kwa style ile ile ya kiboko wa wachawi. Fungulia hivyo viredio vyao utamsikia
 
Mkuu sr
 
Serikali ndo inawapenda hao wajinga na inafurahi wanavyoongezwa ujinga ili iwe rahisi kuwatawala kama mifugo
 
Mkuu we a secular state. You being a lawyer unajua human rights mojawapo ni freedom to religion! Unless kuna mambo ambayo extremist sadaka wacha wakamuliwe wajinga hao.
 
Kama ni hivyo ndio maana matapeli wengi wamepata green pastures. Ukijificha kwenye dini unatapeli kwa raha zako bila bugudha! Hii ni hatari kwa taifa.
 
Mimi Napendekeza SIRIKALI ipitishe kodi ya 30% kwenye makusanyo yanayo patikana kupitia ayo makanisa ili tuweze kupata vyanzo VIPYA vya mapato 🤗🤗
Watoze kodi kwenye mapato haramu? Maana mapato yanatokana na kuwahubiria watu uongo!
 
Kosa ni Kukamuliwa au Kosa ni Makanisa ya Miujiza ?

Ukiniuliza takwambia hizi Imani karibia zote (Opium of the Mass) ni mwendo wa Makamuzi hivyo usingepigilia mstari yapi ya kuingilia kati bali labda useme waangalia ni watu Sheria zetu za Nchi zimevunjwa.... Na katika sheria hizo wasiangalia cha Mhazini, mnadi Sala wala Mswalia Mtume.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…