Serikali iingilie kati Makanisa ya Miujiza? Watanzania masikini wa kutupwa wanakamuliwa mamilioni kwa utapeli huku wahubiri wakigeuka mamilionea

Hayo makanisa na hyo serikali inayoongozwa na ccm hawanatofauti Sanaa .

Hapo n mwingine anakulaa Kwa kuwalaghai hao wanaofata miujizaa Kwa njia ya sadaka .

Na serikali ya CCM inawala Kwa njia ya tozo ,hvyo n ngumu wezi kuingilianaa ktk sekta zao km hakuna anayedhuru maslai ya mwenziee..

Yaan kiufupi hakuna wakututetea km utajiteteaa mwenyewee mkuu[emoji23][emoji23]
 
Mkuu Accumen,
Hayo ni masuala ya imani, unamfunga vipi nabii? unapeleka evidence gani mahakamani kufungwa nabii?

1.watu wameenda wenyewe
2. Wametoa pesa kwa hiari zao
3. Wakiwa na akili zao timamu

Kesi ya zumaridi akituhumiwa kufanya vitendo vya udharirishaji kwa waumini, ni nani walioenda kumtoa kama sio waumini wenyewe.

Bongo kuna hitajika elimu ya ku reason sana kwa vitu.
 
Nd
Ndio hapo labda taasisi za kidini (wakristo) waamue wenyewe ila serikali haina huo uwezo maana ni kuingilia imani za watu.

Kama kuna taasisi zenye mamlaka a juu kwa wakristo wanaweza kuchukua hatua ila sio serikali .
 
Hayo makanisa ni kama CCM yanawanyonya maskini.
 

Wale wafia dini aina za kina johnthebaptist , MK254, Mwaipp Xi anawasalimia
 
Mapastor hawana tofauti na viongozi wa serikali. Wote wanasomana na wote wanakula kwa watz ambao tumekubali kutojielewa
 
Watanzania masikini wa kutupwa, wanakamuliwa mamilioni kwa utapeli, na baadhi ya hawa ma Pastor, huku hao ma Pastor na wahubiri wakineemeka na kuageuka mamilionea na mabilionea huku wakivuta mi ndinga ya nguvu!.
Kwani hili Lina tofauti gani na la wanasiasa mkuu. Unajua tofauti Kati ya siasa na dini. Dini wanakuambia maisha baada ya kufa Kuna adhabu usipofuata wanayotaka Ila siasa wanakuambia maisha ya Sasa na usipofanya Kama wanavyotaka wanakuadhibu Mana majeshi na jela Ni zao pia.

Mbona hukuongea mfano makamba alivyosaini mktaba tanesco wa kukodi software from India ya kufuatilia ama iwe inamwambia Ni wapi umeme umekatika kwa bilioni 69tzs. Unajua hii hela ingesaidia watanzania wangapi masikini na yapo mengi madudu ya wanasiasa.
Hawa wote mtaji wao Ni umasikini na ujinga wa watanzania wa Hali duni. Na ndio wamekataa kuwa hata English isitumike kufundishia from primary Mana watu watakuwa wajanja wengi mno. Mana watapata exposure ya mambo mengi mno na kuwa na Uhuru wa kuhoji. Cheki sheria zetu na Katina zipo kwa English mpaka hospital or banks kila mahala Ni English Ila masikini anazidi kufumbwa macho ili asione.


Please don't be biased acha nao wao watumie ujinga na umasikini wa watu kujineemesha Mana matatizo yako Ni fursa kwa wengine wachache. Yeye Ni kwa Nini asiombe ili apate hizo hela Ila ananiomba mie mtu ameshindwa kujiuliza swali dogo Sana Ilo. Mganga wa kienyeji anakupa dawa ya utajiri na wakati katika Koo yake Hakuna hata tajiri mmoja. Watu Ni wajinga na wavivu wa kufikiria achane waliwe. Kuna prey and predators ndio rule if the jungle and someone having just a slightest edge will survive in long run.
Ukisoma akili na watu na Tabia zao utapata manufaa makubwa mno
 
Serikali yenyewe inaongozwa na washirikina.

Hembu tuambie ule Mwenge unaofanya zindiko nchi nzima,kwa nini ukitaka kuwashwa unawashwa kwa siri sana tena kwa watu wachache tu walioteuliwa?!!

Ukiacha hilo watawala wanajulikana kwa kuroga,kuanzia kwa masangoma,masheikh Hadi kwa wachungaji!!
 
Nd

Ndio hapo labda taasisi za kidini (wakristo) waamue wenyewe ila serikali haina huo uwezo maana ni kuingilia imani za watu.

Kama kuna taasisi zenye mamlaka a juu kwa wakristo wanaweza kuchukua hatua ila sio serikali .
Mkuu ,
Kuna mtu alisema LIKUD kama sikosei.
Alisema ukristo ni IMANI uislamu ni sheria kama nitakuwa nakosea atanirekebisha.

Naona alikuwa sahihi, ukiangalia dhana nzima ya ukristo na uislamu utaona hili jambo.

Taasisi kweli zinaweza kuwepo ila wanazuia vipi hili swala ndio kitendawili kinapoanzia hapo.
 
Hakika, Mwanajopo. Hili ni janga la kitaifa, japo halionekani kushtua mamlaka, na pengine ni kwa sababu liko kiimani zaidi. Naamini Serikali inajua, maana hata baadhi ya viongozi ni wahanga na kimsingi SerIkali inaogopa kuingilia imani za watu wake kwa kisingizio cha uhuru wa kuabudu. Hii ni zaidi ya kausha damu, watu wanaliwa kimya kimya. Kwa mfano mtu anapiga simu kwa 'Nabii' aliyeko kwenye TV, na kisha 'Nabii' huyo anamsimulia shida zake zooote na kuwataja wahusika'''Huko mbeleni tutashuhudia mgogoro mkubwa kwa mazingira haya na hao 'Manabii' watakuwa wamekimbilia nje maana pesa wanazo.. Nayaona yaleee ya Kibwetere!
 
Sijui huwa shida inakuwa wapi kufikiri vitu basic Kama hivi.
 
Hapo ndio mtihani 😁😁maana ukristo mtu anapanga tu afanye nn hamna sheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…