Serikali iingilie kati Makanisa ya Miujiza? Watanzania masikini wa kutupwa wanakamuliwa mamilioni kwa utapeli huku wahubiri wakigeuka mamilionea

Wajinga ndio waliwao,acha waliwe maana wanadai wanapata miujiza.
 
Serikali haina mamlaka kuwapangia wananchi nini cha kuamini na nini cha kutoamini kitendo hicho cha serikali kuingilia uhuru wa kiimani wa jamii fulani ni kinyume na matakwa ya katiba ya JMT.

Ukiruhusu serikali iingilie na kupangia taratibu imani fulani tambua fika na imani yako umeikabidhi mikononi mwa serikali anaweza tokea kiongozi akaona imani yako ni ya kishenzi na akamua lolote atakalo juu ya imani yako na usiwe na nguvu ya kikatiba kupinga hilo.

Tanzania kila mtu yupo huru kiimani kwa kuzingatia katiba ya JMT tuheshimu hilo.
 
huko mwanza ZUMARIDI alisema atamrudisha KANUMBA, kamsumbua mama kanumba kwelikweli, mwisho wa siku hamna kanumba wala kayumba
Alisema alipokuwa gerezani alienda mbinguni, akasema mbinguni kuna magorofa na nyumba za chini, ila magorofa ni mengi zaid, akasema alikutana na mtu petro na amemchumbia anataka kumuoa kwa hyo kinachosubiriwa ni siku ya harusi tu.

kanisa likalipuka kwa shangwe na vigelegele, nilishangaa sana.
 
Mimi siwezi kumshangaa,
Ni sawa na mtu anayekuambia nikifa nitaenda kuimba na kuruka katika kiti cha enzi
Mwingine anakuambia nikifa nitaenda kukutana na mabikra 72 na mito ya pombe.

Hio ndio IMANI inapaswa kuwa.
 
Acha wakamuliwe hakuna aliyeshikiwa fimbo au kulazimishwa kwenda huko ni kwa hiari yao!

Kanisa kiongozi ni 1 tu ndo kusema ndo kupanga ndo kila kitu hadi biblia yeye tu ndo kavuviwa kuichambua wengine hamna acha wakome!


Viongozi wa kisiasa wanaona wanchi kama takataka viongozi wa kiimani ndo kabisaaa!
 
Ni kweli kabisa mkuu serikali ikiingilia kati kwa namna yoyote utazuka mgogoro kwa namna moja ama nyingine, ila kama ingekuwa busara kwa serikali kupitia wizara ya maendeleo ya jamii kutoa elimu ama angalizo kwa muktadha wa mada hii
 
Mm nahisi hawa manabii huwa wana tumia magic power kuwapumbaza waumini wao maana hii sio kawaida.

Urokole ni moja wapo ya ugonjwa wa akili hasa barani Africa ,alafu bora Tz ukienda Nigeria ndo top wa ushenzi wa hawa watu,hawa manabii uchwara wanaelekea kuumeza ukrisito kabisa Iwapo wakiristo wasipo chukua hatua kudhibiti huu upuuzi.

Ndio maana Urusi iliupiga marufuku urokole maana ni tatizo.
 
Hili umelithibitishaje ?....halafu serikali haiamini hili, Sasa kwa nini unatumia kujenga hoja yako?


Hawa wanaofanya haya sio watumishi ili matapeli tu wanaotumia imani za watu kuchuma faida , hawa washitakiwe kwa utapeli na kujipatia mali isivyo halali.

Bahati nzuri wapo waliotapeliwa na hao wahuni ni vyema wakashitaki kwenye vyombo husika.
 
Paskali, hakuna kitu kigumu na hatari kuingilia imani ya mtu, kumbuka mamia waliojiua Johnstown, Kibwetere na ujerumani. Unaweza ukapiga marufuku leo kesho ukakuta maiti zaidi ya elfu moja barabarani, wamejiua kwa kile walichokiamini.
Hebu tuangalie upande wa pili, huko nako kunasemekana kulikuwa au nako kunavuta kitu kidogo, haiwezekani serikali ikaachia mali yake itumike kuendesha utapeli hivihivi tu ikiangalia. Serikali imeacha kukirudisha kiwanda cha nyama TP na kuridhika na utapeli unaofanyika hapo, Moshi kulitokea vifo vya watu vilivyosababishwa na utapeli huo, lakini huenda mambo yakamalizwa kimyakimya nipe nikupe.
Kuondoa tatizo hili ni kuwa na mpango nafuu wa tiba za maradhi badala ya hizi za kulazwa hospitali ya Mwananyamala kuwa aghari kuliko Bondeni Gesti, mapokezi na kumuona dakitari kwa malipo, unaishia kushindwa kununua dawa alizokuandikia dakitari na uombe Mungu usifie hosipitali, ukoo utafilisika kwa kuuziwa maiti yenu.
 
Kanisa lako lenyewe lina mlolongo wa sadaka,kuna masikini nako wanaokamuliwa...labda tu serikali ipitie upenyo wa 'tiba' huko kwenye makanisa ya maajabu,kwamba iwatake wathibitishe wanaponyaje
 
Pamoja na udini sana ulionao leo umeongea point sana, kumbe kuna muda huwa unakuwaga na akili.
 
Pascal Mayalla , Sifa ya mwanaume kamili ni kuwa na msimamo, na kusimamia kule unachokiamini

Hivi wewe kama mwandishi... Ni lini utaandika nyuzi zilizojitisheleza na kuacha nyuzi za kuandika kwa kuuliza!?

Wewe ni mwandishi, unakuwa Muoga Muoga unashindwa kuandika kama waandishi wengine!? ... Kisa unaogopa kuitwa na kuhojiwa!?

Umri ulishaenda... Usitegemee uteuzi mkuu!... Punguza uchawa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…