Serikali iingilie kati Makanisa ya Miujiza? Watanzania masikini wa kutupwa wanakamuliwa mamilioni kwa utapeli huku wahubiri wakigeuka mamilionea

Kwaiyo mr mayala kuhani Musa sio tapeli ila hao usiowapenda ww ndo matapeli

Huna jpy na uzi wako hauna baransi kwaiyo makanisa mengne yote yakirokole ni matapeli sabu wanataka malipo kbla ya kaz
Ila kuhani Musa yy sio tapeli sabu anapokea pesa baada ya kutoa msaada
Je inawezekana atawa anatapeli wazungu wanampa misaada ya kuja kuwapa waumini yeye anakuja kuwauzia

Lakin pia kuhani musa akupangii kiwango cha pesa ila anapokea pesa kutoka kwa waumini

CRDB NA NMB zote ni bank ila kla mmoja anakatiba yake na anautaratibu wake wakufanya kaz

Ata ayo makanisa yakirokole yako tofauti tofauti na kla moja lina utaratibu wake wa kufanya kaz
 
Wanabodi

Kama kawa kila nipatapo fursa huja na makala zangu elimishi za kwa maslahi ya taifa. Topic ya leo, ni kutoa wito kwa Serikali yetu kuingilia kati kitu kinachoendelea kwenye baadhi ya makanisa ya wakovu yanayojinasibu kufanya miujiza, kutoa mapepo, kutoa uchawi na kufanya miujiza ya uponyaji?.

Baadhi ya wahubiri hawa wanatumia nguvu za giza za kiini macho kwa kitu kinachoitwa auto suggestion kwa Watanzania Masikini wa Kutupwa, kuaminishwa umasikini wao ni kwasababu wamelogwa, hivyo ili kuuondoa uchawi wa umasikini, unatakiwa kufanya appointment kumuona Mtumishi, ambapo utapangiwa kiwango cha fedha kumuona mtumishi.

Kwenye matangazo yao kupitia redio na TV, unaambiwa njoo na sadaka yako bila kuambiwa kiwango. Ukifika kanisani,
utaandikishwa na kuambiwa kiwango cha kumuona mtumishi akueleze jinsi ulivyologwa na ni nani amekuloga. Kiwango kilianzia 10,000, baadae ikawa 20,000, ikapanda kuwa 50,000, 100,000 sasa ni 200,000.

Unatakiwa kuitafuta hiyo pesa popote ulipe ndipo umuone mtumishi. Hivyo ni waumini wenye pesa tuu ndio watamuona mtumishi!.

Baada ya kuingia kumuona, mtumishi atakuambia prophesy yako na ku conclude matatizo yako yote, ya kiuchumi, umasikini, maradhi, au majanga yoyote, ni umelongwa na watu wa jijijini kwako!.

Baada ya hapo sasa ndio utapewa bili ya sadaka. Mtumishi atajifanya anamuuliza Mungu, then unaambiwa Mungu amesema njoo na sadaka ya milioni 2, 5, 10, 20, kutegemea na ukubwa wa tatizo lako, ya kuleta hiyo sadaka ndipo Mungu atalimaliza tatizo lako!.

Kutokana na wewe kuwa ni tayari umesha pigwa ganzi, utakwenda kuzitafuta hizo pesa na kuzileta cash!.

Watanzania masikini wa kutupwa, wanakamuliwa mamilioni kwa utapeli, na baadhi ya hawa ma Pastor, huku hao ma Pastor na wahubiri wakineemeka na kuageuka mamilionea na mabilionea huku wakivuta mi ndinga ya nguvu!.

Kuna Mama mmoja alifiwa na mtoto wake, the only son, amedanganywa mtoto wake hajafa, amechukuliwa tuu kichawi, mama kaambiwa akatafute sadaka kiasi fulani, arejeshewe mwanae!, huyo mama ana haha kusaka hiyo pesa ili kumrejesha mwanae!.

Japo haya ni mambo ya imani, na waumini wanakwenda wenyewe kwa hiyari yao na wana toa fedha kwa ridhaa zao, na serikali yetu imetoa uhuru wa kuabudu, lakini ikifikia kiwango Watanzania wanatapeliwa, serikali ina wajibu wa kuingilia kati wananchi wake wasiendelee kutapeliwa!.

Namalizia kwa ile hoja ya msingi jee kuna haja ya serikali iingilie kati shughuli za haya makanisa ya wakovu ya miujiza ili Watanzania masikini wa kutupwa, wasiendelee kukamuliwa mamilioni kwa utapeli, huku wahubiri wakizidi kunona kwa kuwa mamilionea!.

Naomba kuwasilisha.

Paskali
Update

Mkuu Mywangu, usimwingize Mtumishi kweli wa Mungu, Kuhani Mussa, kumuona Kuhani Musa ni bure ila unaweza kuleta sadaka yako yoyote.

Kazi ya ujenzi wa Ngome ya Yesu pale Kimara Temboni, inafanyika kupitia kadi zinaitwa Partnership, hupangiwi kiwango, unajifanyia personal assessment ndipo unajaza!.

Watumishi matapeli kumuona ni lazima utoe 200,000, kuna watu walikuwa na 100,000 walitoa na zikapokelewa, watu wa 200,000 walipoongezeka, wale wa 100,000 walirudishiwa fedha zao, wakaambiwa wakadundulize mpaka zitimie 200,000 ndipo warudi.

Ukimuona Kuhani Mussa anakuombea na kukupatia vifaa vya kiroho bure extra utalipia lakini kuwaona matapeli hawa, unatakiwa kwenda kuleta kwanza sadaka, with the amount, from 6 figures ndipo uombewe!.

P
Mimi pia sikubaliani na utapeli unaoendelea kwa baadhi yao. Lakini na wewe mwanasheria usiyejua madhara ya uhuru wa kuabudu; utatumia kigezo gani kujua huyu yuko sawa, huyu hapana?
 
Serikali ianze na kuondoa 'betting', kwani nayo inaongeza umaskini. Halafu, badala ya kuwabana wahubiri hao, iongeze elimu ya kuchanganua mambo kwa kina, mfano, kuweka somo la falsafa kuanzia shule za msingi, na kuanzisha viping redioni na TV ili kuwapa mwanga watanzania walio wengi.
Hakuna anayewakokota hao waamini wao.
Endapo serikali itafanya maisha bora kwa kila mtanzania, hayo mambo ya miujiza hayatakuwepo. Hivyo, hapa wa kuwajibika ni serikali!
 
Emu kaka mkubwa,acha kuuharibu biashara za watu bhana😄😄😄😄😄.
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
Kiufupi hao jamaa hawana tofauti na kautaratiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiibu ka Chama Dola.
CHUPA na Mfuniko.
Hakuna maskini hapa Nchini kwetu mkuu,ndo maana wenye akili wanachuma mifyeza🤔🤔🤔.
Mtaji wa siasa hapa Nchini hauna tofauti na mtaji wa Kiimani.
Kiufupi,Nchi hii Ina MAZOMBI YALIYOCHANGAMKA.🇹🇿💓💓
 
Wanabodi

Kama kawa kila nipatapo fursa huja na makala zangu elimishi za kwa maslahi ya taifa. Topic ya leo, ni kutoa wito kwa Serikali yetu kuingilia kati kitu kinachoendelea kwenye baadhi ya makanisa ya wakovu yanayojinasibu kufanya miujiza, kutoa mapepo, kutoa uchawi na kufanya miujiza ya uponyaji?.

Baadhi ya wahubiri hawa wanatumia nguvu za giza za kiini macho kwa kitu kinachoitwa auto suggestion kwa Watanzania Masikini wa Kutupwa, kuaminishwa umasikini wao ni kwasababu wamelogwa, hivyo ili kuuondoa uchawi wa umasikini, unatakiwa kufanya appointment kumuona Mtumishi, ambapo utapangiwa kiwango cha fedha kumuona mtumishi.

Kwenye matangazo yao kupitia redio na TV, unaambiwa njoo na sadaka yako bila kuambiwa kiwango. Ukifika kanisani,
utaandikishwa na kuambiwa kiwango cha kumuona mtumishi akueleze jinsi ulivyologwa na ni nani amekuloga. Kiwango kilianzia 10,000, baadae ikawa 20,000, ikapanda kuwa 50,000, 100,000 sasa ni 200,000.

Unatakiwa kuitafuta hiyo pesa popote ulipe ndipo umuone mtumishi. Hivyo ni waumini wenye pesa tuu ndio watamuona mtumishi!.

Baada ya kuingia kumuona, mtumishi atakuambia prophesy yako na ku conclude matatizo yako yote, ya kiuchumi, umasikini, maradhi, au majanga yoyote, ni umelongwa na watu wa jijijini kwako!.

Baada ya hapo sasa ndio utapewa bili ya sadaka. Mtumishi atajifanya anamuuliza Mungu, then unaambiwa Mungu amesema njoo na sadaka ya milioni 2, 5, 10, 20, kutegemea na ukubwa wa tatizo lako, ya kuleta hiyo sadaka ndipo Mungu atalimaliza tatizo lako!.

Kutokana na wewe kuwa ni tayari umesha pigwa ganzi, utakwenda kuzitafuta hizo pesa na kuzileta cash!.

Watanzania masikini wa kutupwa, wanakamuliwa mamilioni kwa utapeli, na baadhi ya hawa ma Pastor, huku hao ma Pastor na wahubiri wakineemeka na kuageuka mamilionea na mabilionea huku wakivuta mi ndinga ya nguvu!.

Kuna Mama mmoja alifiwa na mtoto wake, the only son, amedanganywa mtoto wake hajafa, amechukuliwa tuu kichawi, mama kaambiwa akatafute sadaka kiasi fulani, arejeshewe mwanae!, huyo mama ana haha kusaka hiyo pesa ili kumrejesha mwanae!.

Japo haya ni mambo ya imani, na waumini wanakwenda wenyewe kwa hiyari yao na wana toa fedha kwa ridhaa zao, na serikali yetu imetoa uhuru wa kuabudu, lakini ikifikia kiwango Watanzania wanatapeliwa, serikali ina wajibu wa kuingilia kati wananchi wake wasiendelee kutapeliwa!.

Namalizia kwa ile hoja ya msingi jee kuna haja ya serikali iingilie kati shughuli za haya makanisa ya wakovu ya miujiza ili Watanzania masikini wa kutupwa, wasiendelee kukamuliwa mamilioni kwa utapeli, huku wahubiri wakizidi kunona kwa kuwa mamilionea!.

Naomba kuwasilisha.

Paskali
Update

Mkuu Mywangu, usimwingize Mtumishi kweli wa Mungu, Kuhani Mussa, kumuona Kuhani Musa ni bure ila unaweza kuleta sadaka yako yoyote.

Kazi ya ujenzi wa Ngome ya Yesu pale Kimara Temboni, inafanyika kupitia kadi zinaitwa Partnership, hupangiwi kiwango, unajifanyia personal assessment ndipo unajaza!.

Watumishi matapeli kumuona ni lazima utoe 200,000, kuna watu walikuwa na 100,000 walitoa na zikapokelewa, watu wa 200,000 walipoongezeka, wale wa 100,000 walirudishiwa fedha zao, wakaambiwa wakadundulize mpaka zitimie 200,000 ndipo warudi.

Ukimuona Kuhani Mussa anakuombea na kukupatia vifaa vya kiroho bure extra utalipia lakini kuwaona matapeli hawa, unatakiwa kwenda kuleta kwanza sadaka, with the amount, from 6 figures ndipo uombewe!.

P
Huo ndio unaitwa uhuru wa kuabudu!
 
Kweli upofu wa imani ni mbaya sana, na bila shaka ww mzee unazeeka vibaya.
Yn unawashauri watu waachane na manabii wanaojitajirisha kupitia sadaka zao huku wao walibaki watupu halafu tena unakuja kumtetea huyo nabii Mussa au umekuja kumtangazia biashara yake hapa.
Ww mzee hujitambui
 
Kaka paschal ni ngumu sanaa kuingilia Uhuru wa kuabudu....

Secular state & non_secular state

Cc. Bujibuji Simba Nyamaume , Mshana Jr , Kiranga , Mohamed Said , FaizaFoxy
Kila mtu ana haki ya kuamini au kutoamini anachotaka. Hata kama ni uongo na ujinga. Provided that it is in good faith with no malicious intent, which can be hard to disprove.

Hii ni haki ya kikatiba, ni haki ya utu, ipo katika Universal Declaration of Human Rights tangu December 10 1948.

Njia ya kuondokana na imani za uongo za kijinga ni kuongeza elimu kwa watu, si kupiga marufuku imani hizo.

Na hii kazi ni yetu sote, si ya serikali tu.

Ndiyo maana watu wengi hawaelewi kwa nini Kiranga anarudia sana hoja zake kuhusu kutafuta ukweli na kuachana na kwenda kwa imani tu, kila siku.

Tunahitaji elimu hii sana kupambana na haya mambo ya uongo katika jamii yetu.
 
Ndiyo hao hao mkuu 🤣🤣

johnthebaptist, MK254

Wewe cha kumuabudu huyu MTUME MUHAMMAD ALINYONYA ULIMI WA AL HASSANHadith Idadi 16,245

CQGBAI5W8AAi4mc.jpg
 
hivi nikweli mwanamke anaweza kurogwa asiblid miaka miwili na akaombewa muda huohuo akaanza kumwaga midamu yahedhi mazabahuni?
Ni kweli...

Sababu ya Imani ya mwanamke huyo..

Imani huja kwa kusikia na kusikia huja kwa neno la Mungu, Imani ni kuwa na hakika ni bayana ya vitu visivyoonekana.
 
Pascal Mayalla kaka yangu, pole kwa kuumia [emoji23]. Maana watanzania wanatafunwa vibaya mno na wanaojiita watu wa Mungu. Wanatafunwa Mpaka na wewe wa pembeni unaumia unaona kama sinema. Ila huo ndio ukweli.

Kwa namna Fulani nilitaka niwalaumu sana wanaopigwa kwenye huu utapeli..lakini muda ni rafiki mzuri sana. Majibu niliyapata kwa kukawia ila yalinipa mwangaza mzuri...ambao ninadhani unaweza kutupa mwanga wa walau wapi tuanzie mama mpaka sasa rushapigwa na adui wetu ujinga magoli kadhaa.

Shida yetu kubwa Brother Pascal Mayalla ni lishe duni hasa kwa kipindi Cha siku elfu Moja za kwanza za uhai wa watoto tukianzia kutungwa kwa mimba mpaka mtoto anapotimiza miaka 2.

Kwa mujibu wa wanasayansi kipindi hiki ni muhimu sana kwa makuzi ya mtoto na.mtu kuliko.kipindi kingine chochote. Ni kimpindi ambapo silaha kubwa ya binaadamu, UBONGO wake ndiko unajengwa na kufikia ukomo wa ukuaji wake.

Mtoto akidumaa au asipopata virutubisho wa kusaidia ukuaji mzuri wa ubongo katika kipindi hiki ndio tunakuwa tumempoteza kabisa huyo. Atakomea kuwa na.akili za kusikia njaa na kula au kung'amua pini imemchoma.. zaidi ya hapo kumwambia hapa anapigwa utakuwa unampigia mbuzi gitaa.

Wengi baada ya taabu za miaka ya 80 na kuanza kufanya modernization ya maisha, kukimbilia mijini na kadhalika tumekiwa wahanga wa lishe duni. Na ndio sisi Sasa tuko maofisini, ndio madaktari, wakuu wa wilaya wakuu wa vyombo vya usalama na kadhali ambao ukisikia maamuzi yetu unagunda kabisa ubongo Kuna sehemu ulikomea kabla ya kudevelop fully.

Hapa tushajichanganya nadhani nimkukibali kuanza upya na Wamama wote na watoto chini ya mwaka mmoja. Tuboreshe lishe. Hawa.wa Sasa acha tuu wapeleke fedha kwa Manabii na mitume kwa maana hakuna namna utafanya wakuelewe.

Na huo Wito wa serikali hauna tija hata kidogo, maana wanaosimamia hiyo serikali ndio wanaopeleka huko mizigo na mizigo ili waombewe wasitumbuliwe. Tuwe wavumilivu tuu na tuiombe serikali iwekeze kwenye elimu ya Afya na lishe kwa msisitizo ili tuache kizazi chema huko mbele.
 
Back
Top Bottom